Sunday, November 29, 2015
Thursday, November 26, 2015
RAIS MAGUFULI AFYEKA BARAZA LA MAWAZIRI....WAJUE WALIO RUDISHWA KUPUMZIKA NYUMBANI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, anatarajiwa
kuzifuta wizara 15 kati ya zilizopo sasa na kubaki na baraza dogo
litakalokuwa na wachapakazi makini ili kutimiza dhamira yake ya kubana
matumizi na kuinua maisha ya Watanzania.
Kadhalika, inaelezwa kuwa Dk. Magufuli aliyeahidi kuleta mabadiliko ya kweli wakati akiomba kura kwa Watanzania kabla ya kuibuka na ushindi wa asilimia 58.46 dhidi ya wapinzani wake katika uchaguzi mkuu Oktoba 25, sasa yuko mbioni kutangaza baraza lake la mawaziri litakalokuwa na wizara 15, idadi inayofanana kwa kiasi kikubwa na ile ya Baraza la Mawaziri la miaka ya 1980 lililoundwa na Rais wa Awamu ya Kwanza, Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete, ilimaliza muda wake Novemba 5, 2015 ikiwa na Wizara 30. Kadhalika, alipoingia kwa mara ya kwanza mwaka 2005, Rais Kikwete alikuwa na serikali kubwa yenye mawaziri na naibu wao zaidi ya 60.
Kufikia leo, Rais Magufuli aliyeapishwa Novemba 5, mwaka 2015, tayari ameshamteua Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa, kuwa Waziri Mkuu wa serikali yake ya awamu ya tano na Ijumaa iliyopita alizindua rasmi Bunge la 11.
Chanzo kimoja cha uhakika kimedokeza jana kuwa hivi sasa, tayari Rais Magufuli kwa kushirikiana na wasaidizi wake, ameshakamilisha sehemu kubwa ya mchakato wa kuunda baraza lake la mawaziri na kwamba, kinachosubiriwa sasa ni kulitangaza wakati wowote kuanzia sasa.
Chanzo hicho kilidai kuwa Dk. Magufuli ambaye amejichimbia mjini Dodoma tangu mwishoni mwa wiki iliyopita, anatarajiwa kutangaza baraza lake dogo la mawaziri wakati wowote kuanzia leo.
“Halitakuwa sawa na hili alilomaliza nalo Rais Kikwete… na wala halitakuwa na watu wengi kama lile aliloingia nalo kwa mara ya kwanza Rais Kikwete mwaka 2005. Ni baraza dogo tu na wizara kadhaa hazitakuwapo,” kilisema chanzo hicho

Kesi ya Pingamizi la Kuuaga Mwili wa Alphonce Mawazo Yaunguruma Mwanza
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza leo imesikiliza
kesi ya iliyofunguliwa na familia ya aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema
mkoa wa Geita marehemu Alphonce Mawazo. Kesi hiyo ilifunguliwa
na baba mdogo wa marehemu, mchungaji Charles Lugiko, huku mlalamikiwa
namba
moja ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.
Mawakili wa upande wa jamhuri wamesema mahakamani hapo kuwa kimsingi
hawapingani na hoja ya mwili wa marehemu Mawazo kuagwa jijini Mwanza. Hata
hivyo, upande huo umeendelea kuonesha mashaka waliyo nayo juu ya kuagwa huko.
Akiwasilisha utetezi wa upande wa mlalamikiwa wa kwanza, wakili
wa serikali Emilly Kiria amesema kuwa wanachopinga ni namna na mazingira ya
uagaji wa mwili wa marehemu huyo. Wakili mwwingine wa upande wa jamhuri, Seth
Mkemwa, alisema kuwa mauaji ya kiongozi huyo yalikuwa ya kikatili, hali ambayo
inaweza kuibua hisia kali kwa waombolezaji wakati wa kuagwa kwake.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa Salum Mwalimu akiongea na waandishi wa habari kuhusu kesi ya kuzuiwa kuuaga mwili wa marehemu Mawazo |
Mawakili wa upande wa mlalamikaji, James Ole Milya, John
Malya na Paul Kipeja waliwasilisha mahakamani hapo maombi ya msingi matatu,
wakiiomba mahakama hiyo kutengua amri ya kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza ya
kuzuia kuagwa kwa marehemu Mawazo jijini mwanza. Amri hiyo ya mkuu huyo wa
polisi ilitaja sababu za zuio hilo kuwa ni kuchukua tahadhari dhidi ya mlipuko
wa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na kuwepo kwa taarifa za kiintelijensia
kuwa kuna tishio la hali ya usalama jijini humo.
Ombi jingine lililowasilishwa na mawakili hao wa mlalamikaji
ni kuiomba mahakama itoe agizo kuwa amri hiyo ya kamanda wa polisi wa mkoa wa
Mwanza ni batili kisheria, kwani tangazo linalohusiha mlipuko wa magonjwa kama
kipindupindu lilipaswa kutolewa na afisa anayetajwa kisheria na linapaswa
kutolewa katika gazeti la serikali au katika gazeti lisilo la serikali lenye mzunguko
mkubwa katika jamii, na si kamanda wa polisi.
Ombi la tatu lililowasilishwa na mawakili hao ni kuiomba
mahakama hiyo itoe agizo la kumkataka kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza
asijihusishe au asiingilie shughuli za msiba na kuagwa kwa mwili wa marehemu
Mawazo.
Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Lameck Mlacha imeahirishwa hadi
kesho saa saba mchana ambapo mahakama itakaa kwa ajili ya uamuzi wa kesi hiyo
ya msingi.
Mtoto wa marehemu Mawazo ambaye siku chache zilizopita alifanya mtihani wa darasa la nne huku mwili wa baba yake ukiwa kwenye jokofu la kuhifadhia maiti |
Wakati hayo yakiendelea, mtoto wa kwanza wa marehemu yupo katika mitihani ya taifa ya darasa la nne iliyoanza jana tarehe 25 Novemba na kutarajiwa kumalizika leo. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), watahiniwa wa darasa hilo jana walifanya mitihani ya masomo ya Maarifa ya Jamii, Hisabati, na Lugha ya Kiingereza. Ratiba hiyo inaonesha kuwa leo watahiniwa hao watafanya mitihani ya Sayansi, Kiswahili, Stadi za Kazi, Haiba na Michezo, na Tehama.
Mtoto huyo anafanya mitihani hiyo akiwa katika wakati mgumu huku akifahamu unyama uliotumika kumkata kata baba yake hadi kufa, na pia akifahamu kuwa mpaka sasa mwili wa mzazi wake huyo umehifadhiwa katika jokofu la maiti katika chumba cha kuhifadhia maiti, huku pia kukiwa na mvutano wa kisheria juu ya shughuli ya kuuaga mwili wake.
Wednesday, November 25, 2015
#YALIYOJIRI............................ JAPO UMEPITA KWA MBINDE..........KAMA UTAENDELEA HIVI......... KURA YANGU UTAPATA 2020.....
PROFESA BAREGU AHOJI BUNGE KUCHANGIWA NA MAKAMPUNI, TAASISI ZA UMMA
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), Profesa Mwesiga Baregu amesema anatilia shaka hatua ya Taasisi muhimu kama Bunge kukusanya michango kutoka kwa Taasisi za umma ili kuendeshea shughuli zake, ikiwamo hafla ya uzinduzi wa Bunge mjini Dodoma.
Aidha, Profesa Baregu ameshangazwa na hatua ya Rais John Magufuli kupokea fedha hizo na kuzibariki kutumika katika kununulia vitanda katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili bila kuhoji malengo na msingi wa mhimili huo wa kutunga sheria kuchangiwa fedha hatua ambayo msomi huyo amedai kuwa ni kumwingiza Rais kwenye mtego wa ufisaji wa kimfumo.
“Bunge ni taasisi nyeti sana kuruhusu kuchangiwa pesa na watu au
taasisi ambazo linapaswa kuzisimamia. Mara kadhaa wakuu wa mashirika
haya hutakiwa kuhojiwa ikiwemo kuwasilisha matumizi yao mbele ya Kamati
za Bunge; Je, kweli Bunge litakuwa na nguvu ya kuzisimamia endapo
linapokea michango kutoka kwenye Taasisi hizo?” amehoji Profesa Baregu.
Profesa Baregu ameelezea kitendo cha Bunge kukusanya michango kwa ajili ya hafla kuwa ni ufisadi wa kimfumo ambao haustahili kuvumiliwa. Aidha msomi huyo amesema anategemea kuwa kwa umakini alionao Rais Magufuli hatalifimbia macho hili na atawataka Bunge wajieleze ni kwa namna gani wameingia kwenye ufisadi huu wa mfumo na ikiwezekana kuwachukulia hatua wote waliohusika.

Uingereza yawafurusha raia 46 wa Nigeria
Ndege moja iliyokuwa imewabeba wahamiaji 46 raia wa Nigeria imetua mjini Lagos kutoka Uingereza.
Wahamiaji hao 46 wametimuliwa na maafisa wa Uingereza baada ya kupatikana wakiishi nchini humo kinyume cha sheria.Wengi wao wameelezea kutoridhishwa kwao na hatua ya kurejeshwa nchini Nigeria kwa nguvu.
Mmoja wao amemueleza mwandishi wa habari wa BBC aliyeko Lagos kuwa polisi nchini Uingereza walimkamata na kumfurusha mara moja pasi na kuma ruhusa ya kutwaa vitu vyake.
Wachache kati yao ambao wamesema hawana jamaa mjini Lagos wamesalia katika uwanja wa ndege wasijue pa kwenda
Hivi majuzi serikali ya Nigeria ilielezea kutoridhishwa kwake na mpango ya utawala wa Uingereza ya kuwafurusha wahamiaji elfu thelathini 30,000 kutoka Uingereza.
Nigeria inasisitiza inataka sheria zifwatwe kikamilifu kabla ya kutimuliwa kwa raia wake 29,000 kutoka Uingereza.
Aidha Nigeria inataka Uingereza ihakikishe kuwa wale wanaorejeshwa ni wenye siha nzuri na wale wanaoweza kusafiri kwa ndege.
Vilevile Nigeria inataka Uingereza ihakikishe kuwa wale wanaopelekwa Nigeria wanaasili na vyeti halali vya Nigeria na kuwa wanaweza kujishughulisha kimaisha kabla ya kuwarejesha Nigeria na kuwabwaga huko.
Source BBC Swahili.
Magufuli aamua sikukuu iwe siku ya kazi
Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli
ameamua hakutakuwa na sherehe za kuadhimisha Siku ya Uhuru mwezi ujao na
badala yake akasema itumiwe kufanya kazi.
Sherehe hiyo huadhimishwa kila Desemba 9.Hatua hii ni moja ya mambo yasiyo ya kawaida ambayo kiongozi huyo ameyafanya katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja tangu kuchukua ungozi.
“Maadhimisho ya Uhuru ya mwaka huu 2015 yatatumika kama kichocheo cha kujenga tabia ya kufanya kazi -Uhuru na Kazi - katika Taifa letu,” ilisema taarifa iliyotumwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya ikulu Gerson Msigwa hapo jana.
“Mheshimiwa Rais ameelekeza Watanzania wote siku hiyo waitumie kwa kufanya kazi mbalimbali kama vile, mashambani, maofisini, sokoni, viwandani na usafi wa miji yao katika kutimiza dhana ya Uhuru na Kazi kwa vitendo.”
Taarifa hiyo ilisema Rais Magufuli ametumia Sheria ya Sikukuu za Kitaifa “pamoja na Sheria zingine zinazompa mamlaka Rais kutangaza siku yoyote kuwa sikukuu au mapumziko.”
Rais alisema kadhalika alisema hatua hiyo italiokolea taifa pesa nyingi ambazo hutumiwa katika maandalizi na kufanikisha sherehe hizo.
“Fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hiyo sasa zitumike kwa shughuli zingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na maradhi hasa kipindupindu, kununulia dawa za hospitali, vitanda vya hospitali n.k. kadri kamati za maandalizi zitakavyoamua,” amesema.
Hata hivyo aliongeza kuwa sherehe hizo zitaendelea kuadhimisha kila mwaka kama kawaida kuanzia mwaka ujao.
Miongoni mwa mambo aliyoyafanya Rais Magufuli ni kufanya ziara za kushtukiza Hazina Kuu na Hospitali ya Muhimbili, kuweka masharti kwa safari za nje za maafisa wa serikali.
Aidha, aliamua fedha zilizochangwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kugharamia hafla ya wabunge zipelekwe katika hospitali ya taifa Muhimbili kwa ajili ya kununulia vitanda na magodoro ya wagonjwa wanaolala chini limetekelezwa.
Wadau mbalimbali walichanga fedha kiasi cha shilingi milioni 225 lakini Dkt Magufuli aliagiza fedha za kutumiwa zisizidi shilingi milioni 15 na masalio yapelekwe hospitali ya Muhimbili.
Source: BBC swahili
Thursday, November 19, 2015
WAZIRI MKUU AWAMU YA TANO WA SERIKALI YA JAMHURI YA MHUNGANO WA TANZANIA APATIAKANA...... SOMA HAPA.....
Waziri
Mkuu mteule Kassim Majaliwa ametangazwa Mshindi wa nafasi hiyo Spika wa
Bunge Job Ndugai kwa kupata kura 258 sawa na asilimia 73.5 ya kura
zilizopigwa na kuthibitishwa na Spika wa Bunge.
-Idadi ya wabunge kikatiba 394,Wabunge waliosajiliwa 369,Akidi 184,idadi ya wabunge waliokuwepo ukumbini wakati wa zoezi la kupiga kura 351,Kura zilizopigwa 351,Kura mbili ziligharibika,idadi ya kura halali 349,
Matokeo.Idadi ya kura za hapana 91 sawa na asilimia 25 .9,idadi ya kura zilizoharibika 2 sawa na asilimia 0.06.

NDUGU AUA MDOGO WAKE BAADA YA KUMKUTA AKIJAMIAANA NA NGURUWE
Mtoto wa miaka 16 mkazi wa kijiji cha Mbwila wilayani Ludewa mkoani Njombe Simon Dastani amefariki dinia baada ya kupigwa kwa fimbo na kaka yake baada ya kukutwa akifanya mapenzi na Nguruwe mali ya mkazi wa kijiji hicho. kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Wilbroad Mtafungwa alisema kuwa kijana huyo aliuwawa baada ya kaka yake kusikia kijana huyo ameizalilisha Familia yao kwa kufanya mapenzi na mnyama na kuanza kumchapa fimbo kitu kilicho sababisha kutoka damu nyingi na kupelekea kifo chake.
source EATV
Waziri Mkuu awamu ya Tano .......apendekezwa......... muda si mrefu atapigiwa kura na wabunge wote
Rais
Dk. John Pombe Magufuli amemteua Majaliwa Kassim Majaliwa, Mbunge wa
Ruangwa kuwa Waziri Mkuu wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Jina lake limetajwa bungeni muda huu.
Mhe. Majaliwa atathibitishwa kwa kupigiwa kura na wabunge wote muda mfupi ujao.
Kassim Majaliwa
Kassim Majaliwa alizaliwa Desemba 22, 1960 na ana umri wa miaka 54.
Ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Saturday, November 14, 2015
Sunday, November 1, 2015
Subscribe to:
Posts (Atom)
BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA
BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm
-
Sasa ni hivi, Kitendo cha kucheza na kisimi kwa utaalamu na mirindimo tofauti mpaka mwanamke anamaliza ndio kinaitwa "katelelo...
-
Katika makala hii tunaanza na kuelezea maana ya fasihi, fasihi fasihi simulizi kwa kutumia wataalam mbalimbali, baada ya kuelewa vizur...
-
The term code of ethics and code of conduct have been used interchangeably by Teachers and organizatio...