Ndege moja iliyokuwa imewabeba wahamiaji 46 raia wa Nigeria imetua mjini Lagos kutoka Uingereza.
Wahamiaji hao 46 wametimuliwa na maafisa wa Uingereza baada ya kupatikana wakiishi nchini humo kinyume cha sheria.Wengi wao wameelezea kutoridhishwa kwao na hatua ya kurejeshwa nchini Nigeria kwa nguvu.
Mmoja wao amemueleza mwandishi wa habari wa BBC aliyeko Lagos kuwa polisi nchini Uingereza walimkamata na kumfurusha mara moja pasi na kuma ruhusa ya kutwaa vitu vyake.
Wachache kati yao ambao wamesema hawana jamaa mjini Lagos wamesalia katika uwanja wa ndege wasijue pa kwenda
Hivi majuzi serikali ya Nigeria ilielezea kutoridhishwa kwake na mpango ya utawala wa Uingereza ya kuwafurusha wahamiaji elfu thelathini 30,000 kutoka Uingereza.
Nigeria inasisitiza inataka sheria zifwatwe kikamilifu kabla ya kutimuliwa kwa raia wake 29,000 kutoka Uingereza.
Aidha Nigeria inataka Uingereza ihakikishe kuwa wale wanaorejeshwa ni wenye siha nzuri na wale wanaoweza kusafiri kwa ndege.
Vilevile Nigeria inataka Uingereza ihakikishe kuwa wale wanaopelekwa Nigeria wanaasili na vyeti halali vya Nigeria na kuwa wanaweza kujishughulisha kimaisha kabla ya kuwarejesha Nigeria na kuwabwaga huko.
Source BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment