Showing posts with label Our News. Show all posts
Showing posts with label Our News. Show all posts

Saturday, March 11, 2017

NAFASI ZA KAZI KWA WALIMU WA SAYANSI NA HISABATI WALIOHITIMU MWAKA 2014/2015 KURUDI NYUMA.



Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawatangazia wahitimu wote wa Stashahada na Shahada ya Ualimu katika masomo ya Sayansi na Hisabati wa mwaka 2014/ 15 na miaka ya nyuma, kuwa bado kuna nafasi za ajira, hivyo, wenye sifa watume maombi yao.
Wahitimu walioomba wakati Wizara ilipotangaza nafasi za ajira mwezi Desemba, 2016 na Januari, 2017 wasiombe tena kwa kuwa mchakato wa ajira kwa wale wenye sifa unaendelea. Wahitimu walioajiriwa Serikalini wasiombe.
Nyaraka zinazotakiwa kuwasilishwa ni hizi zifuatazo:-
  • Elimu ya sekondari (Kidato cha Nne na Sita);
  • Taaluma ya Ualimu (Stashahada, Shahada au Stashahada ya Uzamili katika Elimu -PGDE);
  • ‘Academic Trascript’ ya Stashahada, Shahada au Stashahada ya Uzamili katika Elimu-PGDE);
  • Cheti cha Kuzaliwa;
  • Wasifu (CV) unaoonesha majina matatu. Mwombaji ambaye vyeti vyake vya Elimu na Taaluma havina jina la tatu, akamilishe taratibu za kisheria za kuongeza jina la tatu na kuwasilisha kiapo stahiki pamoja na maombi yake.
UTARATIBU WA KUTUMA VYETI NI KAMA IFUATAVYO:-
  1. Mwombaji anatakiwa ‘ku-scan’ vyeti/nyaraka halisi – (Kidato cha 4, 6, Stashahada, Stashahada ya Uzamili na Shahada) na siyo kivuli (photocopy) na kuhifadhi katika ‘File’ moja la ‘pdf’. File lipewe majina matatu ya mwombaji kuanzia la kwanza, kati na la mwisho ndipo litumwe.
  2. Mwombaji atumie anuani ya barua pepe yake mwenyewe na siyo ya mtu mwingine kutuma nyaraka zake.
TANBIHI:
  1. Tarehe ya mwisho kupokea nyaraka ni 30 Machi, 2017.
  2. Barua pepe za kuwasilisha nyaraka za waombaji zitumwe mara moja tu na si kwa kurudia rudia ili kuepuka usumbufu.
  3. Yeyote ambaye vyeti vyake havitahakikiwa hatafikiriwa katika ajira.
  4. Wahitimu ambao waliomba awali mwezi Desemba, 2016 na Januari, 2017 na nyaraka zao ziliwasilishwa kikamilifu na kupokelewa, majina yao yamewekwa kwenye tovuti ya Wizara www.moe.go.tz. Hao wasiwasilishe nyaraka hizo tena.
  5. Tangazo hili haliwahusu wahitimu waliofaulu mtihani mwaka wa masomo 2015/16 baada ya kurudia masomo waliyoshindwa mwaka 2014/15.
  6. Nyaraka zote ziwasilishwe kwa barua pepe ifuatayo: apa@moe.go.tz
IMETOLEWA NA
Tarish M.K.
KATIBU MKUU
10/03/2017
 

Orodha ya Walimu wa Sayansi na Hisabati Wahitimu ngazi ya shahada 2015>>> Link Hapo Chini

Friday, December 16, 2016

AJIRA ZA WALIMU WA SANA(ARTS) KUSITISHWA

WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, ametoa masharti mapya ya ajira za ualimu nchini, huku akisema Serikali haitaajiri walimu wa masomo ya sanaa (arts) kwa kuwa wapo wa kutosha.

Akizungumza mjini Dodoma jana wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA), Profesa Ndalichako, alisema Serikali kwa sasa haiwezi kuajiri walimu wa masomo hayo kwa kuwa inataka kuajiri walimu wa masomo ya sayansi na hisabati ambao idadi yao ni ndogo.

“Pamoja na uamuzi huo mpya, ajira za walimu wapya wa masomo ya sayansi nazo zimebadilika kwani wale wote waliohitimu ualimu wa sayansi na hisabati, wanatakiwa watume vyeti vyao kabla ya kupangiwa kituo cha kazi.

“Kuhusu wale walimu wa ‘arts’, kule tuna walimu wa ziada ambao tutajaribu kuwapanga kutokana na shule, kwani wengi walikuwa wamepangwa shule moja. Kwahiyo, tutaangalia utaratibu wa kuwapanga kulingana na mahitaji,’’ alisema Profesa Ndalichako.

Akizungumzia suala la ubora wa elimu nchini, Profesa Ndalichako aliwataka walimu wakuu hao kuhakikisha wanasimamia ubora wa elimu kwa kuwa wao ndio wanaowaandaa wanafunzi kabla hawajaenda vyuoni.

“Vilevile pelekeni takwimu sahihi za wanafunzi waliopo katika shule zenu kuisaidia Serikali katika kupanga bajeti ili iweze kutoa fedha sahihi.

“Hapa kuna kimbembe, yaani wakati mwingine huwa najifanya nimepoteza takwimu ya shule fulani, nikiziomba na kutumiwa, zinakuwa ni tofauti na zile za mwanzo.

“Hili nawaomba mkalisimamie ili iwe rahisi kwetu kupanga bajeti yenye tija,’’ alisema.

Kuhusu ujenzi wa maabara katika shule za sekondari, waziri huyo alisema kwamba kutokana na nyingi kukamilika, Serikali itatoa vifaa vya maabara kuanzia Januari mwakani baada ya kuwa vimeingia nchini kutoka vilikoagizwa.

Awali, akisoma risala ya walimu hao, Rais wa TAHOSSA, Bonus Nyimbo, aliiomba Serikali itoe waraka wa kupiga marufuku matumizi ya simu kwa wanafunzi shuleni kwa kuwa zimekuwa zikichangia kushuka kwa ufaulu kwa baadhi ya wanafunzi.

“Ili kuboresha elimu, tunaiomba Serikali itoe waraka wa kupiga marufuku matumizi ya simu kwa wanafunzi kwani simu nyingi tunazozikamata tunakuta mule hakuna taaluma,’’ alisema Nyimbo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik Molel, ambaye pia kampuni yake ilipewa tuzo ya heshima katika kuendeleza elimu nchini, alisema ni jukumu la kila mmoja kutimiza wajibu wake ili kuiendeleza elimu ya Tanzania.

“Kila mmoja anapaswa kutimiza wajibu, wazazi, walezi na walimu, waambieni wanafunzi wasiwe na ‘expectation’ (matarajio) makubwa kwani wanapokuwa na matarajio hayo, wakienda vyuo vikuu wanakuwa wasumbufu,” alisema.

Wakati hayo yakiendelea, juzi taarifa ilitolewa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi, ikisema kwamba, walimu wahitimu wa masomo ya sayansi na hisabati waliohitimu shahada na astashahada mwaka 2015, wanatakiwa kuwasilisha nakala za vyeti vya elimu ya sekondari vya kidato cha nne na sita na taaluma ya ualimu kwa uhakiki.

Pamoja na hayo, hivi karibuni Serikali ilitangaza kusitisha ajira zote nchini ili kukabiliana na wimbi la watumishi hewa.

Sambamba na uamuzi huo, nyongeza za mishahara kwa watumishi wa Serikali nazo zilisimamishwa ili kukabiliana na watumishi hao hewa ambao walikuwa wakiingizia hasara Serikali.
 

Wednesday, August 31, 2016

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe Atangaza Kuahirisha Maandamano ya Oparesheni UKUTA Yaliyokuwa Yamepangwa Kufanyika Kesho

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ametangaza kusitishwa kwa maandamano ya Oparesheni UKUTA yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kesho nchi nzima.

Mbowe ametoa kauli hiyo ya kuahirisha maandamano mchana huu wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya habari.

Amesema sababu kubwa za kuahirisha maandamano hayo ni busara za viongozi wa dini ambao wameiomba Chadema iwape muda wa   kutafuta Suluhu 

Mbowe amesema maandamano hayo yameahirishwa hadi Oktoba Mosi 

SOURCE http://www.mpekuzihuru.com/2016/08/sikiliza-live-mkutano-na-waandishi-wa.html

Wednesday, August 24, 2016

Rais Magufuli ateua Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

http://www.chela-kahama.blogspot.comRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Agosti, 2016 amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Modestus Francis Kipilimba alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Dkt. Modestus Francis Kipilimba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Rashid Othman ambaye amestaafu.

Dkt. Modestus Francis Kipilimba ataapishwa leo mchana tarehe 24 Agosti, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Rais Magufuli amemteua Bw. Robert Msalika kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Robert Msalika alikuwa Afisa Ubalozi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bw. George Madafa kuwa Balozi na nchi atakayopangiwa itatajwa baadaye.

Wakurugenzi na Naibu Wakurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa waliopo wanaendelea na nafasi zao.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
24 Agosti, 2016

Wabunge Wataka Rais Magufuli Atoe Kibali cha Ajira Kwa Walimu Wapya ili Kukabili Uhaba Wa Walimu Uliopo Hivi sasa

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa imeomba Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imuombe Rais atoe kibali cha ajira kwa walimu kukabili uhaba unaoikabili nchi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza alitoa ushauri huo jana mjini Dodoma kwenye kikao kati ya wajumbe wa kamati hiyo na viongozi na watendaji wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakiongozwa na Naibu Waziri, Selemani Jafo.

Kikao hicho kilikuwa ni cha kamati kupokea na kujadili taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa mpango wa ofisi hiyo wa utoaji elimu bila malipo katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu ambako suala la uhaba wa walimu liliibuliwa na wajumbe.

Wednesday, July 13, 2016

Ajira Mpya za Watumishi 71,496 kusitishwa kutokana na WATUMISHI HEWA NCHINI'

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki amesema serikali imelazimika kusitisha ajira mpya za watumishi 71,496 serikalini, mwaka huu hadi pale tatizo la watumishi hewa litakapopatiwa ufumbuzi.

Akifungua mafunzo kuhusu maadili ya viongozi wa umma kwa wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji Ikulu Dar es Salaam jana, Kairuki alisema tangu oparesheni ya kutafuta watumishi hewa ianze hadi sasa watumishi 12,246 wameshaondolewa.

Kairuki alisema tatizo la watumishi hewa nchini bado ni kubwa kwani uzoefu unaonesha kuwa nchi nyingi zilizokumbwa na tatizo hilo, ni asilimia ndogo tu ya watendaji ndio iliyokuwa inawajibika.

Alisema kwa sasa serikali imelazimika kusimamisha masuala mengi ya utumishi wa umma ili ipate taarifa kamili ya aina ya watumishi waliopo, na kwamba ma-DED hao kuhakikisha wanasimamia vyema oparesheni hiyo kwani hadi sasa watumishi hewa waliobainika, takribani asilimia 90 wanatokea katika Serikali za Mitaa.

Aidha, Kairuki alisema pamoja na kugundulika kuwa tatizo la watumishi hewa ni kubwa nchini, pia serikali imebaini kuwepo kwa watumishi watoro wasiotimiza wajibu wao.

“Nawataka mkahakikishe mnawabana hawa maofisa utumishi, haiwezekani kuwepo na tatizo la watumishi hewa kubwa kiasi hiki huku pia kukiwa na tatizo la watumishi watoro, hawa maofisa kwani walikuwa na majukumu gani?” Alihoji Kairuki.

Alisema endapo serikali itabaini kuwa maofisa utumishi hao wamehusika katika matatizo hayo ya watumishi hewa na utoro, wataondolewa mara moja.

 “Serikali haina mchezo kila ofisa katika eneo lake, awe ofisa elimu, afya na kilimo wafanye kazi zao,” alisema.
 
 
 

Wednesday, June 22, 2016

Rais Magufuli aeleza sababu za kusitisha ajira serikalini kwa muda




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali imeamua kusimamisha kwa muda mfupi usiozidi miezi miwili zoezi la utoaji ajira mpya na upandishaji wa vyeo kwa watumishi wa umma kwa lengo la kupisha uhakiki wa watumishi wa umma katika orodha ya malipo ya mshahara na kuondoa watumishi hewa. 
 
Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 22 Juni, 2016 katika Jubilei ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) iliyofanyika katika ukumbi wa Benki hiyo, Mtaa wa Mirambo Jijini Dar es salaam.
 
Dkt. Magufuli amesema zoezi hilo halina nia ya kuwakatisha tamaa watumishi wa umma na amewahakikishia watumishi wote wa umma kuwa serikali itaendelea kuajiri watumishi wapya na kuwapandisha vyeo waliopo kama kawaida mara baada ya kukamilika kwa zoezi.
 
"Serikali ninayoiongoza haina nia ya kuwakatisha tamaa wafanyakazi, lengo lake ni kujipanga kwa makosa tuliyoyafanya, na ndio maana nimesema kwa kipindi cha mwezi mmoja hivi au hata mwezi mmoja na nusu, haitazidi miezi miwili, tusiajiri mtumishi yeyote serikalini, lakini pia katika kipindi cha mwezi mmoja hatutawapandisha vyeo wafanyakazi, ninaomba wafanyakazi waelewe hili, kwa sababu tukiendelea tutakuwa tunawapandisha vyeo hata wafanyakazi ambao hawapo, tunafanya ukaguzi wote tukishamaliza wafanyakazi wataendelea kupandishwa vyeo" amesema Rais Magufuli.
 
Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa kazi kubwa iliyoifanya katika kipindi cha miaka 50 katika kusimamia sekta ya fedha na maendeleo, lakini ameitaka benki hiyo kuchukua hatua za haraka dhidi ya baadhi ya changamoto zinazoyahusu majukumu yake.
 
Miongoni mwa changamoto hizo ni idadi ndogo ya watanzania wanaonufaika na huduma za benki hususani waishio vijijini, benki kutoza riba kubwa na hivyo kusababisha wananchi kuogopa kukopa kwa hofu ya kushindwa kulipa, kuilinda thamani ya Shilingi ya Tanzania, na kukusanya kodi ipasavyo kwa miamala inayofanywa kupitia simu za mkononi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA).
 
Changamoto nyingine ni kusimamia ipasavyo maduka ya kubadilishia fedha (Bureau  de change) ili kuthibiti utakatishaji na utoroshaji wa fedha na kuhakikisha ushukaji wa mfumuko wa bei uliotoka asilimia 28 hadi kufikia asilimia 5.1 katika kipindi cha miaka 15 iliyopita unaonesha matokeo katika nafuu ya maisha ya watanzania.
 
Aidha, Rais Magufuli ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania kuchukua hatua mara moja dhidi ya benki ambazo hazizalishi faida zikiwemo benki za serikali, kufuta account mfu (Domant account) na kuanzisha mara moja akaunti moja ya mapato na matumizi ya serikali (Single Treasury Account)
 
Jubilei hiyo imehudhuriwa na Magavana na Manaibu Gavana kutoka nchi 18 za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC), Mabalozi kutoka nchi mbalimbali, Viongozi wa Taasisi za fedha za Afrika na Makatibu wakuu wa Wizara za Fedha na Mipango wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
22 Juni, 2016 
#TAG FROM>>>>

Monday, June 20, 2016

Serikali yasitisha ajira zote


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SERIKALI imesitisha ajira zote, kama njia ya kukabiliana na wimbi la watumishi hewa.
Kutokana na uamuzi huo hivi sasa hakuna nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa Serikali na wakala zake pamoja na utoaji wa vibali wa likizo ya bila malipo.
Akizungumza na MTANZANIA jana jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro, alisema kuwa Serikali imesitisha kwa muda utoaji wa ajira, ili kupitia upya muundo wa Serikali na taasisi zake.
Alisema utekelezaji wa mkakati huo utakwenda sambamba na kusitisha kwa muda utoaji wa vibali vya ajira zote mbadala pamoja na uidhinishaji wa ajira hizo zilizopo Sekreterieti ya Ajira katika utumishi wa umma na kwenye mfumo wa taarifa za kiutumishi.
“Ni kweli tumesitisha kwa muda ili kupitia mfumo wa Serikali na hata kuangalia ulipaji wa mishahara kama upo katika malipo stahiki.
“…na hili litakwenda sambamba na hata kusitishwa malipo ya mishahara yanayotokana na upandishwaji wa vyeo kwa watumishi. Tukimaliza zoezi hili ndipo tunaweza kuanza kutoa ajira za Serikali,” alisema Dk. Ndumbaro.
Alisema muundo mpya wa utumishi wa Serikali unakwenda sambamba na uhakiki wa malipo ya mishahara, hivyo ni lazima ujue ni nani unayemlipa kuliko ilivyo sasa.
Kwa mujibu wa maelekezo hayo uhamisho na uidhinishaji katika mfumo wa watumishi ambao wamehamishwa kutoka kwa mwajiri mmoja kwenda kwa mwajiri mwingine ambao atalipwa mshahara mkubwa kuliko ule wa sasa pia utaangaliwa kwa lengo la kupata taarifa sahihi za mtumishi husika.
“Baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki watumishi pamoja na tathmini ya muundo wa Serikali na taasisi zake, wote wataarifiwa ni lini utekelezaji utaendelea,” alisema.
Taarifa kutoka maeneo mbalimbali nchini, zililiambia gazeti hili kuwa maelekezo hayo yalitolewa Juni 13, mwaka huu na kusambazwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwa makatibu wakuu wote, makatibu tawala wa mikoa, kwa wakuu wa idara za Serikali zinazojitegemea.
Waliotakiwa kutekeleza maelekeo hayo ya Serikali ni wakurugenzi wote wa majiji, manispaa na miji, wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya, watendaji wa taasisi za umma na watendaji wa wakala za Serikali kwa upande wa Tanzania Bara.

Monday, May 16, 2016

Walimu 35,411 Kuajiriwa Mwezi wa 7 Mwaka Huu


Walimu 35,411 nchini wataajiriwa katika shule za msingi na sekondari katika mwaka wa fedha 2016/2017.

Watakaokaidi kwenda kuripoti katika mikoa ya pembezoni, hawataajiriwa na serikali.

Hatua hiyo imeelezwa kwamba imetokana na serikali kupokea maombi mengi ya kazi kwa walimu, ambao mwaka jana hawakuripoti katika vituo walivyopangiwa pembezoni mwa miji kwa kutegemea kuajiriwa na shule binafsi, lakini hawakufanikiwa.

Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo alisema hayo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF) aliyetaka kufahamu serikali inafanya nini kwa walimu waliopangiwa kwenda mikoa ya pembezoni, ikiwemo Lindi na kwingineko, lakini hawakuripoti.

Jaffo alisema ni kweli kuna walimu wengi ambao hawakuripoti katika mikoa ya pembezoni. Alisema si Lindi peke yake, bali na mikoa mingine, ikiwemo Katavi na Kigoma.

Alisema kwa mwaka huu, wataajiri walimu 35,411, lakini ambaye hataripoti katika mikoa hiyo na kuishia mijini tu, hawataajiriwa tena serikalini, kama wanavyoomba tena baada ya kukosa katika shule binafsi.
 

Friday, February 26, 2016

Makamba, Ndalichako, Mahiga, Kitwanga wapewa masaa



ambapo wamepewa muda mpaka saa 12 jioni wawe wamesharejesha fomu hizo
Mawaziri wanaotakiwa kurejesha fomu za tamko la rasilimali pamoja na hati ya ahadi ya uadilifu ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Charles Kitwanga na Waziri wa Nchi (OMR – Muungano na Mazingira), Bw. January Makamba. Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga ambaye anatakiwa kurejesha hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako ambaye anatakiwa kutoa tamko la rasilmali na madeni.
“Mheshimiwa Rais ameelekeza mawaziri ambao hawajajaza tamko la rasilmali au hati ya ahadi ya uadilifu wafanye hivyo na kuzirejesha kabla saa 12 jioni na Waziri ambaye atashindwa kutekeleza agizo hili atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake,” amesisitiza Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu amesema wakati akifungua mafunzo ya Mawaziri na Naibu Waziri kuhusu Mwongozo wa Maadili ya Viongozi wa Umma na Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu yaliyofanyika Ikulu jana (Alhamisi, Februari 25, 2016) alikabidhiwa majina ya Mawaziri na Naibu Mawaziri ambao hawajawasilisha Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Kamishna wa Maadili.


SOURCE EATV PAGE

Sunday, February 21, 2016

UCHAGUZI UGANDA>>>>DKT BESIGYE KASEMA HAYA

Mmoja wa wapinzani wakuu katika uchaguzi mkuu uliofanyika Alhamis wiki hii nchini Uganda, Dkt Kizza Besigye, amepinga matokeo ya uchaguzi huo.
Dkt. Besigye ambaye amekuwa akizuiliwa nyumbani kwake tangu siku ya Ijumaa amesema kuwa raia nchini Uganda wameshuhudia udanganyifu mkubwa katika uchaguzi huo, ambao haujahi kufanyika katika taifa hilo.
Kanali huyo mstaafu ameuelezea uchaguzi huo kuwa si halali na kuwa ni sawa na mapinduzi ya kijeshi.
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa jana, Rais wa muda mrefu wa taifa hilo Yoweri Kaguta Museveni, alitangazwa mshindi.
Rais Museveni ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka thelathini sasa, alipata zaidi ya asilimia 61 ya kura huku Besigye akijipatia asilimia 35 ya kura.
Waangalizi wa kimataifa wamesema kuwa uchaguzi huo uliandaliwa katika mazingara ya hofu na kudhalalishwa.

 SOURCE STAR TV

Friday, January 22, 2016

MATOKEO YA DARASA LA NNE 2015 YAMETOKA BOFYA LINK HAII HAPA CHINI KUYAONA>>>>>>>>.



NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

                                            SFNA-2015 ASSESSMENT RESULTS


                                                                     


http://www.necta.go.tz/matokeo/2015/SFNA/index.htm

Thursday, January 7, 2016

TAARIFA KUHUSU AJIRA MPYA ZA WALIMU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa anaongea na Wazazi mkoani Ruvuma katika ziara yake ya Serikali mkoani humo. Amesema serikali itamaliza tatizo la uhaba wa waalimu na hasa wale wa sayansi pindi itakapowaajiri julai mwaka huu.
Source: Dira ya Mchana TBC1

Monday, December 21, 2015

YALIYOSEMWA KATI YA Rais Dkt. Magufuli na Maalim Seif walipokutana Ikulu Dar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana naMakamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharrif Hamad,jana tarehe 21 Desemba, 2015 Ikulu Jijini Dar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Maalim Seif Sharif Hamad ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Makamu wa rais wa Jamhuri Samia Hassan Suluhu
Mazungumzo ya Viongozi hao pia yamehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Viongozi hawa kwa pamoja wamejadili hali ya kisiasa Zanzibar na wamefurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, na viongozi wote wanaoshiriki katika mazungumzo ya kuleta hali ya uelewano Zanzibar.
Rais Magufuli pia amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kudumisha amani na utulivu wakati wa mazungumzo baina ya viongozi wa CUF na CCM yakiendelea huko Zanzibar.
Katika Mazungumzo hayo Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad amemueleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya hali ya siasa Zanzibar kadiri anavyoielewa yeye na Rais Magufuli amemshukuru Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa taarifa yake nzuri huku akimsihi waendelee na mazungumzo hadi suluhisho muafaka lipatikane.
Majadiliano yanayoendelea yanatoa fursa ya kudumishwa kwa utulivu na sifa njema ya nchi yetu. Wote kwa pamoja wamewaomba wananchi waendelee kuwa watulivu ili kutoa nafasi ya majadiliano yanayoendelea kufikia hatma njema.
Wameelezea matumaini yao kuwa vyama vya CCM na CUF haviwezi kushindwa kupata suluhu ya mgogoro huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemuhakikishia kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano itahakikisha kuwa amani na utulivu unaendelea kudumishwa Zanzibar.

SOURCE EATV PAGE

BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

 BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm

Logo

Logo Design by FlamingText.com