Walimu 35,411 nchini wataajiriwa katika shule za msingi na sekondari katika mwaka wa fedha 2016/2017.
Watakaokaidi kwenda kuripoti katika mikoa ya pembezoni, hawataajiriwa na serikali.
Hatua
hiyo imeelezwa kwamba imetokana na serikali kupokea maombi mengi ya
kazi kwa walimu, ambao mwaka jana hawakuripoti katika vituo
walivyopangiwa pembezoni mwa miji kwa kutegemea kuajiriwa na shule
binafsi, lakini hawakufanikiwa.
Naibu
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani
Jaffo alisema hayo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa
Mchinga, Hamidu Bobali (CUF) aliyetaka kufahamu serikali inafanya nini
kwa walimu waliopangiwa kwenda mikoa ya pembezoni, ikiwemo Lindi na
kwingineko, lakini hawakuripoti.
Jaffo
alisema ni kweli kuna walimu wengi ambao hawakuripoti katika mikoa ya
pembezoni. Alisema si Lindi peke yake, bali na mikoa mingine, ikiwemo
Katavi na Kigoma.
Alisema
kwa mwaka huu, wataajiri walimu 35,411, lakini ambaye hataripoti katika
mikoa hiyo na kuishia mijini tu, hawataajiriwa tena serikalini, kama
wanavyoomba tena baada ya kukosa katika shule binafsi.
No comments:
Post a Comment