Katika makala hii tunaanza na kuelezea maana ya fasihi,
fasihi fasihi simulizi kwa kutumia wataalam mbalimbali, baada ya kuelewa vizuri
dhana hizi tutajadili vigezo vilivyotumika katika mgawanyo wa tanzu na vipera
vya fasihi simulizi katika makala ya M.M Mulokozi (1989) na hatimaye
tutaangalia ubora na udhaifu wa uainishaji wa tanzu hizo, na kumalizia na
hitimisho, kielelezo na mwisho marejeo
.
.
Fasihi
ni sanaa itumiayo lugha ili kufikisha ujumbe kwa jamii bila kujali kuwa
imeandikwa au haijaandikwa. Fasihi ambayo haijaandikwa ni fasihi simulizi na
fasihi iliyoandikwa ni fasihi andishi.
Ama
kuhusu Fasihi simulizi, Wamitila ( 2002) anaeleza kuwa Fasihi simulizi ni
fasihi ambayo huwasilishwa kwa njia ya mdomo kwa kusimuliwa, kuimbwa ,
kutongolewa au kughanwa.
Naye
Mulokozi (1996) anaelezea kuwa fasihi simulizi ni fasihi inayotungwa au
kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa njia ya mdomo na vitendo bila maandalizi.
Kwa
ujumla fasihi simulizi ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na
kuwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya
mdomo na vitendo bila maandishi.
Katika
makala ya M.M Mlokozi (1989) katika mulika ya 21 amejaribu kuzigawa tanzu za
fasihi simulizi ya Tanzania katika tanzu zake mahususi kwa kuzingatia VIGEZO vifuatavyo;
Umbile na tabia ya kazi inayohusika;upande wa umbile na tabia ya kazi
ya sanaa ameangalia vipengele vya ndani vinavyoiumba sanaa na kuipa mwelekeo au
mwenendo ilionao.Vipengele hivyo ni namna lugha
inavyotumika(kishairi,kinathali,kimafumbo,kiwimbo, kighani nakadharika) pia
muundo wa fani hiyo na wahusika kama wapo.
Kigezo
cha pili ni muktadha na namna ya uwasilishaji wake kwa hadhira (hili
linazingatia pia dhima yake kijamii) hapa Mulokozi amezingatia ukweli wa msingi
kuwa fasihi simulizi ni sanaa inayo pita, isiyofungwa katika umbo maalum, wala
matini maalum yasiyo badilika. Fasihi simulizi inatawaliwa na vitu muhimu
vitatu yaani watu, wakati na mahali. Mwingiliano huu ndio muktadha, na muktadha
ndio unaamua fani fulani ya fasihi simulizi ichukue umbo lipi? Iwasilishe vipi
kwa hadhira, kwenye wakati na mahali hapo.
Zifuatazo ni tanzu na vipera vya
fasihi simulizi kama zilivyoainishwa na M.M.Mlokozi(1989)
katika mulika 21 na jinsi alivyo ziainisha kwa kutumia vigezo hivi viwili,
yaani kigezo cha umbile na tabia ya kazi inayohusika na kigezo cha muktadha na
namna ya uwasilishwaji kwa hadhira, na vipera vyake.
M.M.Mulokozi
ameainisha tanzu sita ambazo ni; mazungumzo, masimulizi, maigizo (drama)
ushairi semi na ngomezi (ngoma). Hivyo ufuatao ni uainishaji wa tanzu
hizi za fasihi simulizi na vipera vyake kwa kutumia vigezo vya Mulokozi katika
mulika ya 21.
Mazungumzo, ni maongezi au maelezo ya mdomo
katika lugha ya kawaida, juu ya jambo lolote lile. Si kila mazungumzo ni fasihi
mazungumzo ili yawe fasihi lazima yawe na usanii wa aina fulani, na uhalisia
baada ya kuunakili.
Tanzu
zinazoingia katika fungu la mazungumzo; Hotuba, Malumbano ya watani, Ulumbu, Soga na
mawaidha.
Katika kuainisha tanzu hizi ndani ya mazungumzo M.M. Mulokozi ametumia vigezo vyote viwili;
Hotuba, malumbano ya watani, ulumbu, soga na mawaidha. Kwa kuzingatia kigezo
cha kwanza kinachozingatia msingi wa umbile na kazi inayohusika, tunaona tanzu
hizi zote zina vipengele vya vinvyoumba sanaa na kuipa muelekeo au mwenendo
ulionao, katika hotuba, malumbano ya watani, ulumbu, soga na mawaidha vyote
vinavipegele vyake. Pia tanzu hizo zote zina maana ya lugha inayotumika. Mfano
katika hotuba lugha rasmi ndiyo inayotumika, katika malumbano ya watani lugha
ya kejeli mara nyingi ndio hutumika zaidi, mawaidha hutumia lugha rasmi au
lugha za kikabila hutumika.
Pia
katika kigezo umbile na tabia ya kazi inayohusika,katika kuainisha tanzu hizi
mulokozi ametumia muundo wa fani na wahusika kama wapo.Tanzu zote hizo katika
mazungumzo zina fani yake. Mfano katika malumbano ya watani ni tanzu inayozingatia
fani zifuatazo; Kuna utani wa mababu, mabibi na wajukuu, utani wa mashemeji,
utani wa kikabila na utanu wa marafiki. Kila kimojawapo kati ya fani hazi huwa
na kanuni zake, miktadha yake na mipaka yake katika jamii zinazohusika.
Pia
katika kuanisha tanzu za mazungumzo Mulokozi ametumia kigezo chake cha pili
yaani kigezo kinachozingatia muktadha na namna ya uwasilishwaji wake kwa
hadhira hili linazingatia pia dhima yake katika jamii kama ifuatavyo;
Ndani
ya mazungumzo kuna hotuba, mawaidha, ulumbu, malumbano ya watani, soga; Tanzu
hizi zote zinazingatia msingi wa fasihi kuwa ni sanaa inayopita, isiyofungiwa
katika umbo maalum, wala matini yasiyobadilika. Mfano Hotuba ni sanaa
inayopita, isiyofungwa katika umbo maaluma na matini yake hubadilika kulingana
na matukio kama vile; matukio ya kidini, sherehe na kadharika. Hotuba hufuata
wakati, watu na mahali. Katika kigezo hiki kinachozingatia muktadha na namna ya
uwasilishwaji wake kwa hadhira huzingatia wakati, watu na mahali.Tunaona katika
mazungumzo na tanzu zake zinazingatia wakati watu na mahali, mfano mawaidha
huzingatia watu gani,wana umri gani, je ni vijana wa kiume au wa kike. Pia
huzingatia mahali yaani tukio linapofanyika, mfano sebuleani au chumbani na pia
wakati gani asubuhi, mchana au jioni.
Tanzu
ya mazungumzo kwa ujumla imeainishwa kwa kutumia vigezo vyote viwili yaani
kigezo cha umbile na tabia ya kazi inayohusika na kigezo kinachozingatia
muktadha na namna ya uwasilishwaji wake kwa hadhira.
Masimulizi; ni fasihi yenye kusimulia
habari fulani. Mulokozi (1989) anasema kuwa masimulizi ni
fasihi ya kihadithi na fani zake huwa na sifa zifuatazo; hueleza atukio katika
mpangilio fulani mahsusi, huwa na wahusika yaani watendaji au watendwaji katika
matukio yanayosimulia, hutumia lugha ya kimaelezo, utambaji wake au utoaji wake
huweza kuambatana na vitendo au ishara, na huwa na maudhui ya kweli au ya
kubuni na yenye mafunzo fulani katika jamii.
Katika
mulika 21 Mulokozi amegawanya masimulizi katika tanzu zifuatazo; za kihadithi na Tanzu za Kisalua.
Katika
tanzu za kihadithi amezigawa katika
makundi yafuatayo;
Ngano
ni hadithi za kimapokeo zitumizo wahusika kama wanyama,miti na watu
kuelezea au kuonya kuhusu maisha.Utanzu huu unajumuisha fani kadhaa kama vile; istiara,mbazi,na kisa.
Tanzu
za kisalua zimegawanywa katika fani
zifuatazo; visakale, tarihi, visasili,.
Hivyo tunaona kuwa katika uainishaji wa tanzu hii ya masimulizi mulokozi
ametumia vigezo vyote viwili kama ifuatavyo; katika msingi wa umbile na tabia
ya kazi inayohusika Mulokozi ameonyesha vipengele vya ndani vinavyoiumba sanaa
na kuipa mwenendo ulionao. Na vipengele hivyo ni kama; lugha ya kimaelezo,
maudhui, matukio na wahusika.Pia ameonyesha namna lugha inavyotumika mfano.
Ngano hutumia lugha ya kimaelezo na visakale, mapisi, tarihi, kumbukumbu na
visasili. Vipera hivi vyote hutumia lugha ya kimaelezo.
Pia
katika msingi wa umbile na kazi inayohusika, kigezo hiki huzingatia muundo wa
fani na wahusika kama wapo.Tanzu ya masimulizi ina fani zifuatazo kutokana na
Mulokozi. Hueleza matukio katika mpangilio fulani mahususi, huwa na wahusika
yaani watendaji au watendwaji katika matukio yanayosimuliwa, utambaji au utoaji
wake huweza kuambatana na vitendo au ishara, huwa na maudhui ya kweli au ya
kubuni na yenye mafunzo fulani na hutumia lugha ya kimaelezo.
Semi ni tungo au kauli fupifupi zenye
kubeba maana fulani au mafunzo muhimu katika jamii, Mulokozi ameaimisha tanzu
za semi kama ifuatavyo:-
Methali ni semi fupi fupi zenye kueleza kwa
muhtasari fikra au mafunzo mazito yaliyotokana na uzoefu wa jamii. Methali huwa
na sehemu mbili kwanza sehemu ambayo huanzisha wazo fulani sehemu ya pili
ambayo hulikanusha au kulikamilisha wazo hilo. Methali ni utanzu tegemezi ambao
kutokea kwake hutegemea fani nyingine mfano maongezi, majadiliano mazito,
muktadha maalum katika methali Mulokozi ameainisha tanzu hii kwa kutumia kigezo
cha umbile na tabia ya kazi inayohusika, katika kigezo hiki Mulokozi ameonyesha
matumizi ya lugha. Mfano methali hutumia tamathali, sitiari na mafumbo. Pia
methali huwa na wahusika wa fani zake zinazojitegemea. Mfano Haraka haraka / Haina Baraka. Wahusika
kuna anayeuliza Haraka haraka na
anayejibu Haina Baraka. Pia lugha
aliyotumia katika methali hii ni lugha ya kinathari na kishairi.
Pia
methali huwa na fani zake. Mulokozi anasema methali ni utanzu tegemezi ambao
kutokea kwake hutegemea fani nyingine, fani hizo ni maongezi au majadiliano
mazito, muktadha maalumu, huwa na sehemu mbili sehemu ya kwanza ambayo
huanzisha wazo fulani na sehemu ya pili ambayo hulikamilisha au kukanusha wazo
hilo.
Ndani
ya kigezo cha muktadha na namna ya uwasilishaji methali huwa na dhima ya kutoa
mafunzo, kuadibisha, kuonya na kuhamasisha jamii. Methali huendana na wakati,
watu na mahali kwa kuzingatia tukio pia huwa na matini yanayobadilika. Mfano Haraka haraka haina Baraka, methali hii
inatoa onyo kuwa ukifanya jambo kwa haraka unaweza kukosea, hivyo polepole ndio
mwendo.
Vitendawili; hizi ni usemi uliofumbwa ambao hutolewa
kwa hadhira ili waifumbue. Fumbo hilo kwa kawaida huwa linafahamika katika
jamii hiyo na mara nyingi lina mafunzo muhimu kwa washiriki mbali na
kuwachemsha akili zao. Vitendawili
hutegemea uwezo wa kutambua, kuhusisha na kulinganisha vitu vya aina mbalimbali
vilivyomo katika maumbile, ni sanaa inayojitegemea, inayotendwa na ina
jisimamia yenyewe.
Katika
kigezo cha umbile na tabia inayohusika vitendawili hutumia lugha ya mafumbo na
huwa na washiriki yaani wahusika ambao ni yule anayetoa kitendawili na
anayejibu. Mfano Mmoja huuliza Kitenawili na mwingine anajibu tega. Mfano; Kaa huku na mimi ni kae kule tumfinye mchawi (kula ugali), Mfano huu
huhamasisha ushirikiano baina ya watu.
Pia
vitendawili huwa na fani kama wahusika (pande mbili) wanaouliza na wanaojibu,
muktadha maalumu (mazingira) katika muktadha na namna ya uwasilishaji Mulokozi
amesema vitendawili huwa na mafunzo fulani zaidi ya chemsha bongo. Vitendawili
huzingatia mazingira (mahali) watu na wakati maalum mfano watoto, mahali
(shuleni au nyumbani) na huwa na wakati maalum.
Misimu, ni semi za muda na mahali maalum
ambazo huzuka na kutoweka kutegemea mazingira maalum. Msimu ukipata mashiko ya
kutosha katika jamii hatimaye huingia katika kundi la methali za jamii hiyo.
Mfano Tamu tamu mahonda ukinila
utakonda.
Katika
kigezo cha muktadha na namna ya uwasilishaji wake kwa hadhira misimu ni sanaa
inayopita isiyofungiwa katika umbo maalum wala matini maalum yasiyobadilika.
Misimu ina dhima ya kutoa mafunzo, kuonya, hutumika katika siasa pia misimu
huenda na wakati, watu na mahali. Mfano Matteru (1987) anasema ‘tamu
tamu mahonda ukinila utakonda’ . Katika
mfano huu unaonyesha madhara ya pombe iliyokuwa inatengenezwa na kiwanda
cha mahonda (Zanzibar). Katika kigezo cha umbile na tabia ya kazi inayohusika
misimu hutumia lugha isiyosanifu kwani huzuka na kutoweka mfano; mdebwedo, utajiju, yeboyebo, buzi na kimeo.
Mafumbo ni semi za maonyo au mawaidha
ambazo maana zake ni za ndani na zimefichika. Fumbo hubuniwa na msemaji kwa
shabaha na hadhira maalum hivyo ni tofauti na methali ambazo ni semi za
kimapokeo. Katika kigezo cha muktadha na namna ya uwasilishwaji mafumbo huwa na
dhima ya kutoa maonyo na mawaidha kwa jamii kwani hubuniwa kwa hadhira maalum.
Mfano ‘Mbele ya bata
kuna bata na nyuma ya bata kuna bata, jumla nina bata wangapi’? Fumbo hili huonyesha umakini katika katika
kufanya kitu. Katika mafumbo ndani ya kigezo cha umbile na tabia ya kazi
inayohisika huangalia namna lugha inavyotumika, katika mafumbo ambayo maana
yake ya ndani imefichika mafumbo huundwa na wahusika na fani yake. Mfano yule
anayetoa fumbo (anasema fumbo mfumbie
mjinga ) Yule anayejibu (mwerevu ataling’amua)
hapa anamainisha mjinga hawezi akalifumbua fumbo ila mwerevu hulifumbua pia
mjinga anaweza akadanganywa ila mwerevu hawezi kudanganywa. Fumbo hili
linahamasisha mtu afanye juhudi katika mambo ili afanikiwe kama mwerevu.
Lakabu ni majina ya kupanga ambayo baadhi
ya watu hupewa au kujipatia kutokana na sifa zao za kimwili, kinasaba, kitabia
au kimatendo. Majina haya huwa ni sitiari. Majina haya huweza kumsifia mtu au
kumkosoa. Mfano Mkuki uwakao – Jomo
Kenyatta, Sakarani – mlevi, Simba wa yuda – Haile sellasie.
Katika
kigezo cha umbile na tabia inayohusika Mulokozi ameonyesha lakabu hutumia
maneno yenye maana iliyofungwa na sitiari, pia lakabu huwa na wahusika yule
anayepewa sifa. Mfano mkuki uwakao – Jomo Kenyatta na anayetoa sifa.
Katika
muktadha na namna ya uwasilishaji lakabu huwa na dhima mbalimbali kama kusifia,
mfano baba wa taifa, inatoa sifa ya utendaji bora wa kazi, simba wa yuda
inaonyesha mshupavu. Mkuki uwakao inaonyesha kiongozi mchapa kazi. Pia lakabu hukosoa na kuonya
mfano sakarani- ulevi hapa inaonyesha kuwa mtu mlevi hafai katika jamii. Lakabu
huwa na matini yanayobadilika, hivyo ni sanaa inayopita, lakabu hufuata watu
wakati na mahali.
Ushairi, ni sanaa ya vina inayopambanuliwa
kama nyimbo mashairi na tenzi. Zaidi ya kuw na vina ushairi una ufasaha wa kuwa
na maneno machache au muhtasari mawazo na maono ya ushairi huvuta moyo kwa
namna ya ajabu. Mulokozi (1989) anasema ushairi hupambanuliwa na lugha ya
kawaida kwa kutumia lugha na mbinu za kimuktadha. Kauli za kishairi hupangwa kwa
kufuata wizani maalumu na mawimbi ya sauti na mara nyingi lugha ya mkato na
mafumbo hutumika ushairi una fani zinazoambatana na muziki wa ala na wakati
mwingine hupata wizani wake kutokana na mapigo ya muziki huo wa ala. Mulokozi
(1989) amegawa ushairi katika mafungu
mawili ambayo ni nyimbo na uwasilishaji.
Nyimbo ni kila kinachoimbwa hivyo hii ni
dhana panainayojumuisha tanzu nyingi za kinathari kama vile hadithi huweza
katika kundi la nyimbo pindi zinapoimbwa . Vipera
vya nyimbo ni tumbuizo, bembea, kongozi, nyimbo za dini, tenzi, tendi,
mbolezi, kimai, nyiso, nyimbo za vita, nyimbo za uwindaji, nyimbo za taifa,
nyimbo za watoto na nyimbo za kazi.
Katika
kuainisha tanzu hiii ya nyimbo Mulokozi
ametumia vigezo vyote viwili, tukianza na kigezo cha kwanza ambacho ni
umbile na tabia ya kazi inayohusika Mulokozi ameonyesha jinsi vipengele vya
ndani vinavyoiumba sanaa na kuipa mwelekeo. Vipengele vilivyo katika nyimbo ni
namna lugha inavyotumika .
Mfano:
nyimbo za maombolezo hutumia lugha za maombolezo yenye maneno ya Kufariji
tofauti na nyimbo za sherehe huwa na lugha ya furaha na kuchangamsha.
Katika
kigezo hiki pia cha umbile na tabia ya kazi inayohusika Mulokozi ameonyesha
muundo wa fani na wahusika katika nyimbo.
Mfano: mambo muhimu yanayotambulisha nyimbo ( fani ya nyimbo) Muziki wa
sauti ya muimbaji au waimbaji( wahusika), Muziki wa ala (kama ipo), Matini au
maneno yanayoimbwa,Hadhira inayoimbiwa,Muktadha unaofungamana na wimbo huo
mfano sherehe, ibada na kilio.
Pia
Mulokozi katika kuainisha tanzu ya nyimbo ametumia kigezo cha pili yaani
muktadha na namna ya uwasilishwaji wake kwa hadhira katika kuainisha tanzu hii
ya nyimbo amezingatia wakati, watu (wahusika) na mahali. Pia nyimbo ina matini
yanayobadilika, yasiyofungiwa katika umbo maalumu yaani ni sanaa inayopita.
Mfano:
kuna nyimbo zinazoimbwa kwa kufuata wakati wake, mahali mahususi, na mahali
maalumu, mfano wawe na vave hizi ni nyimbo za kilimo, mbolezi hizi ni nyimbo za
kilio au maombolezi. Mbolezi huimbwa wakati maalumu, na waombolezaji ambao ni
watu( wahusika) na mahali maalumu (mfano msibani)
Maghani ni ushairi unaotolewa kwa kalima
badala ya kuimbwa. Zipo maghani za aina mbili, kuna maghani ya kawaida, ambayo
huundwa na fani mbalimbali za ushairi simulizi mfano mapenzi, siasa,
maombolezo, kazi za dini na kadhalika. Maghani ya masimulizi hutambwa ili
kusimulia hadithi, historia au matukio fulani ambayo huambatana na nyimbo.
Tanzu za maghani ni sifo, vivugo, tondozi, rara, ngano na tendi.
Maghani
ni tanzu iliyoanishwa kwa kutumia kigezo cha muktadha na namna ya uwasilishwaji
wake kwa hadhira. Molokozi ameonyesha maghani huwasilishwa kwa kalima badala ya
kuimba, pia dhima za maghani ni kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa kuzingatia
matukio
Mfano uhuru kesi za
mauaji
Mulokozi
anasema maghani huundwa na fani mbalimbali za ushairi simulizi mfano mapenzi,
siasa, maombolezo, kazi na dini. Zifuatazo ni fani za ushairi simulizi ambazo
ni, Masimulizi hutolewa kishairi, huhusu matukio muhimu ya kihistoria au jamii,
huelezea habari za ushujaa na mashujaa, huwasilishwa kwa kughanwa (ala ya
muziki), hutungwa papo kwa papo.
Pia
maghani huwa na wahusika, na huambatana na muziki wa ala. Mulokozi anasema
mutambaji wa ghani hizi huitwa Yeli au Manju na kwa kawaida huwa ni bingwa wa
kupiga ala fulani ya muziki (mtambaji huyu ndiye mhusika mkuu)
Maigizo, (drama) ni sanaa inayotumia
watendaji kuiga tabia au matendo ya watu na viumbe wengine ili kiburudisha na
kutoa ujumbe fulani. Maigizo ni sanaa inayopatikana katika makabila mengi.
Mulokozi anasema drama (maigizo) ya kiafrika huambatana na ngoma mtambaji wa
hadithi au matendo ya kimila. Kwa mfano
jando na unyago , yapo maigizo yanayofungana na michezo ya watoto, uwindaji ,
kilimo, na kadhalika. Drama hutumia maleba maalumu kama vizuizui (mask).
Katika
kuainisha tanzu hii mulokozi ametumia vigezo viwili,kwa kuanza na kigezo cha
kwanza Mlokozi ameainisha,mambo na vipengele vinavyopatikana ndani ya maigizo
ambavyo ni maigizo yanayohusu matendo ya kimilana michezo ya watoto,matanga,
uwindaji, kilimo na nyinginezo.
Kwa
msingi wa umbile na tabia inyohusika vipengele vya ndani vinavyoiumba sanaa na
kuipa muelekeo tanzu hii ya maigizo ni lugha inavyotumika katika kuigiza fani
na wahusika mfano wahusika wa maigizo wapo na hawa ndio watendaji wakuu katika
kufikisha ujumbe. Maigizo hutumia lugha mfano lugha ya kejeli na hata lugha
rasmi pia maigizo huwa na fani inayotendwa.
Mulokozi
Pia katika kuainisha tanzu hii ya maigizo ametumia kigezo cha pili
kinachozingatia muktadha na namna ya uwasilishaji wake kwa hadhira, maigizo ni sanaa
inayopita isiyofungiwa kaika umbo maalum wala matini yasiyobadilika ila maigizo
hubadilika kutokana na tukio linaloigigwa na kuzingatia wakati, watu na mahali
mfano maigizo huhitaji sehemu maalumu (jukwaa au uwanja wa kutendea) , wahusika
ambao ndio waigizaji wakuu na pia maigizo huenda na wakati.
Ngomezi ni midundo Fulani ya ngoma
kuwakilisha kauli Fulani katika lugha ya kabila hilo. Mara nyingi kauli hizo
huwa ni za kishairi au kimafumbo
Mulokozi
ametumia vigezo vyote viwili katika kuainisha tanzu hii, kwa kuanza na umbile
na tabia ya kazi inayohusika ameangalia vipengele ndani vinavyoiumba sanaa na
kuipa mielekeo na mienendo ulionao.Vipengele hivyo ni namna lugha inayotumika,
kishairi, kinathari, kimafumbo, kiwimbo au kighani. Mfano, katika ngomezi hutumia
lugha na kauli za kishairi au kimafumbo.
Pia
kigezo hiki huangalia fani na wahusika kama wapo, katika ngomezi huwa na
wahusika ambao hupiga na kuandaa ngoma hizo.hii hujionyesha katika utofauti wa upigaji wa ngoma hizi kutokana
lengo lake ambapo inaweza kutoa taarifa,
tahadhari au ngomezi za uhusiano.
Katika
kigezo cha pili muktadha na namna ya uwasilishaji wake kwa hadhira Mulokozi
ameonyesha jinsi ngomezi ilivyo ni sanaa ambayo huandaliwa kwa matukio maalum.
Pia ngomezi hutawaliwa na vitu vitatu muhimu katika kigezo hiki ambavyo ni
watu, wakati na mahali.
M.M
Mulokozi katika mulika amejitahidi kuelezea na kuzigawa tanzu na vipera vya
fasihi simulizi kwa kuzingatia vigezo vyote viwili, yaani umbile na tabia ya
kazi inayohusika na kigezo cha muktadha na namna ya uwasilishaji wake kwa
hadhira.
Pamoja
na kujitahidi huko, kuna baadhi ya mapungufu ambayo yamejitokeza kama;
Mulokozi
ameonyesha utenzi wa ngomezi, ila hajayuonyesha vipera au vitanzu
vinavyojitokeza au kupatikana katika utanzu huu.
Mulokozi
ameainisha na vipera vya fasihi simulizi lakini yeye mwenyewe anakiri kuwa bado
hakuna wataalamu walioshughulikia suala hili undani zaidi kwani tanzu za fasihi
simulizi hutifautiana kati ya jamii na jamii, Hivyo Mulokozi ameonyesha udhaifu
wa kitaaluma
Mulokozi
ameshindwa kutofautisha istilahi ya Tanzu na Vipera. Badala ya kutumia vipera
yeye ametumia tanzu: vipera vya hadithi yeye anasema fungu au tanzu za
kihadithi.
Mulokozi
pia ameonyesha udhaifu pale anaposema misimu ikipata mashiko huingia kwenye methali,
wakati misimu ikipata mashiko ya kutosha si lazima kuingizwa kwenye methali tu
bali huingizwa kwenye msamiati wa lugha sanifu mfano: ngunguli, ngangali na
ulanguzi
Kwa
kuhitimisha tunaweza kusema kuwa, uainishaji wa tanzu na vipera vya fasihi
simulizi kama vilivyoainishwa na Mulokozi vinaingiliana kifani na kimaudhui.
KIELELEZO
KINACHOONYESHA TANZU NA VIPERA VYA FASIHI SIMULIZI.
MAREJEO
Mulokozi,
M.M. (1989) Tanzu za Fasihi Simulizi
Mulika 21:1-24, Dar es salaam: TUKI.
Mulokozi,
M.M. (1996) Fasihi ya Kiswahili, Chuo
Kikuu Huria cha Dar es salaam
Publishers Ltd.
NADHARIA ZA UCHAMBUZI WA FASIHI
Wataalamu
mbalimbali wameainisha nadharia mbalimbali za uchambuzi wa kazi yoyote ya
fasihi. Miongoni mwa nadharia hizo ni pamoja na;
Nadharia ya umuundo (structuralism)
Umuundo ni nadharia inayojibainisha kwa kuangalia Ujumla wa
uhusiano wa sehemu moja kwa nyingine katika kufanya kitu kizima. Kwa mfano
muungano wa maneno hufanya sentensi na sentensi zikiungana zinaunda aya au
onesho na onesho kuunda tamthiliya.
Ntarangwi (2004) anasema kuwa umuundo waweza kuelezwa kama mtizamo
wa kitathimini ambao huzingatia zaidi miundo inayojenga kazi binafsi.
Mwasisi anayetajwa sana katika nadharia hii ni Ferdinard De
saussure aliyependekeza mtizamo mpya kuhusu lugha. Kinyume na wataalamu wengine
walioshughulikia historia na sura maalum za lugha fulani, Saussure alivutiwa na
miundo inayohimili lugha zote, huku akijaribu
kuonyesha kwamba lugha zote za ulimwengu zaweza kutathiminiwa kwa kaida maalum
za umuundo. Alizua istilahi `parole' na `langue' kueleza maoni yake: `Parole'
au uzungumzi ni lugha katika matumizi
na hiki ndicho walichokizingatia wanaisimu wa awali, lakini Saussure alivutiwa
na mfumo wa kinadharia unaounda lugha zote au `Langue' - yaani masharti au kaida zinazoiwezesha lugha
kuwepo na kuweza kufanya kazi.
Hata hivyo, kazi ya Saussure ilikuwa imetengewa wanaisimu peke
yao. Katika miaka ya 1950, mtizamo huo wa Saussure ulianza kusambaa katika
masomo mengine hasa wakati mawazo yake yalipozingatiwa na Mwanaanthropolojia
Claude Levi-strauss. Kwa kuchukua maoni ya isimu ya Saussure na kuyaingiza
katika sayansi ya kijamii . Hasa alichotaka kuendeleza kidhana ni kwamba pana
viwango viwili katika kuelewa maisha ya jamii, isimu, lugha na chochote kingine
kile. Viwango hivi ni cha juu juu (surface) na cha ndani (deep).
Mkondo huu wa mawazo ya umuundo kuhusu sayansi za jamii ulianzia
ulaya na kuathiri mtazamo wa elimu mbalimbali (duniani) kama vile: Falsafa,
Anthropolojia, Historia, Uhakiki wa kifasihi na Sasiolojia.
Kwa hivyo twaweza kuangalia jamii katika muundo wake wa kijuu juu
na kuielewa lakini tukitaka kupata maana mwafaka lazima tuchunguze muundo wake
wa ndani ambao hupatikana katika kila jamii ya wanadamu. Kwa hiyo hata katika
kuielewa fasihi lazima tuifahamu lugha yake.
Katika kupata maana lazima kuwe na uhusiano wa kipembetatu yaani
kuna DHANA, ALAMA na KITAJWA.
UMUUNDO NA FASIHI
Kama vile muundo wa lugha ulivyo mfumo, muundo wa fasihi pia una
vipengele vinavyotegemeana na vinavyoelezwa katika muktadha wa vipengele
vingine. Katika kazi ya fasihi kuna kitengo cha kisanaa kama vile maudhui,
ploti, wahusika, muktadha na lugha. Hakuna kipengele cha fasihi kati ya hivi
kitakachoelezwa katika upekee wake. Lazima kielezwe kwa kuzingatia kuwepo kwa
jukumu la vipengele vingine. Kwa mfano katika kueleza au kuzungumzia ploti,
wahusika watashirikishwa na lugha yao kuzingatiwa.
Kwa hiyo nadharia ya umuundo husisitiza vipengele vya kazi ya
sanaa, jinsi vinavyohusiana hadi kuikamilisha kazi hiyo. Huangalia namna sehemu
mbalimbali za kazi za sanaa zilivyofungamana. Yaani Neno halihitaji urejelezi
ili lipate maana, na Kazi yenyewe ilivyoundwa ndivyo hutoa maana. Yaani maana
inavyoumbwa ina dhima kubwa kuliko maana yenyewe.
Wafula na Njogu (2007) wanasema kuwa Umuundo unapinga wazo la
kijadi linalodai kwamba fasihi ni tokeo la mchango wa maudhui na fani. Dhana ya
kimapokeo kuhusu fasihi inadai kwamba fasihi ni umbo lenye viungo viwili,
maudhui na fani na kwamba viungo hivi vyaweza kutenganishwa.
Wahakiki wanoegemea mkondo wa Saussure huzingatia kwamba matini
husika ni mfumo unaojisimamia na hivyo
basi huwa hamna haja ya kutumia mambo ya nje ili kuhakiki kazi ya fasihi.
Wahakiki huzingatia matini kama kiungo kamili kinachoweza kuhakikwa kivyake.
Hivyo basi mhakiki wa umuundo hujaribu kuweka sarufi ya matini pamoja na sheria
za jinsi matini hiyo hufanya kazi.
Mhakiki anayezingatia zaidi muundo wa lugha ya matini bila shaka
hupuuza dhana ya jadi kuhusu kile matini hiyo huweza kutueleza kuhusu maisha;
na hivyo basi hufanya mtindo wa kazi
yenyewe kiini cha uhakiki wake.
Kwa hivyo wahakiki wanaotumia nadharia ya umuundo hujaribu kuzingatia matini
peke yake huku wakiepuka kuifasiri kazi ile kulingana na kaida zilizowekwa
kuhusu jinsi matini hufanya kazi.
Hata hivyo, huenda njia hii isiwe ya kufaa sana kwa sababu huwa
inachukulia kwamba kila kitu kimeundwa katika mpangilio halisi usiotatanika na
usiotegemea mambo mengine yaliyo nje yake. Ama kwa hakika, hata lugha yenyewe
haiwezi kabisa kufanya kazi bila kuathiriwa na mambo mengine kama vile
mazingira yake (Ntarangwi 2004).
Nadharia ya umarx (marxism)
Kwa maana rahisi kabisa, tunapoongelea kuhusu nadharia ya U-Marx
tuna maana ya kurejelea mikabala mbalimbali ambayo misingi yake mikuu ni mawazo
yanayohusishwa na Carl Marx na Friedrich Engels. Katika kitabu cha The Germany Ideology,
Marx na Engels walisema kuwa kitu cha msingi katika maisha ya binadamu ni kula na kunywa, kupata malazi na mavazi
na mambo mengine. Tendo la kwanza la kihistoria kwa hiyo ni kutafuta njia ya
kuyakidhi mahitaji haya ya msingi. Ili kufanikiwa katika lengo hilo, binadamu
hulazimika kujiunga pamoja au kuunda umoja ili kuimarisha umoja na wepesi wa
kuizalisha mali ya kukidhi mahitaji hayo. Muungano huo huwa na ugawaji wa
majukumu au kazi ambayo ndiyo msingi wa kuundwa kwa matabaka katika jamii.
Hatua ya juu ya mwendelezo huu ni uzukaji wa mfumo wa ubepari. Katika mfumo
huu, mali inamilikiwa na idadi ndogo ya watu. Watu hao wanaipata mali yao
kutokana na unyonyaji wa umma na hasa wafanya kazi (Wamitila 2002:).
Kwa mawazo ya Marx,
maendeleo ya jamii huthibitika katika vipindi vya maisha ambavyo kizazi
cha binadamu kimepitia. Kutokana na Marx tabaka la jamii hutoweka na lingine
huchipuka kwa sababu ya mgongano wa kitabaka. Mgongano huu hutokea kwa sababu
kuna tabaka la wanyonyaji na wanaonyonywa. Hivyo, inabidi kuwa na mapinduzi
dhidi ya mifumo ya kuzalisha mali inayohimili unyonyaji. Mapinduzi yanayotokea
baadaye yanaongeza tumaini la ujenzi na uimarishwaji wa jamii inayozingatia
usawa. Marx anamwona binadamu kuwa kiini cha historia yote na matendo yote
yanayotendeka humu duniani. Umarx unamwabudu binadamu, hivyo humpa tumaini
binadamu la kung’oa mizizi yote ya unyonyaji na unyanyasaji na kujenga
ulimwengu wa kinjozi usiokuwa na madhila (Wafula na Njogu 2007). Vidato ambavyo
jamii ilipaswa kupitia kabla ya kufikia ukamilifu wa kinjozi ni vifuatavyo: Ujima,
Utumwa, Umwinyi, Ubepari, Ujamaa na Ukomunisti
Kwa jumla, twaweza kusema kwamba mhakiki wa Ki-marx hukita
nadharia yake kwenye itikadi za Karl Marx na Fredrick Engels, na hasa kwenye
madai ya hao wawili kuwa, katika tathimini ya mwisho kabisa maendeleo ya
historia ya binadamu pamoja na taasisi zake, yatakuwa ni tokeo la mabadiliko
katika njia za kimsingi za uzalishaji mali. Kwamba mabadiliko kama hayo
husababisha mageuko katika muundo wa matabaka ya kijamii ambayo katika kila
kipindi huendeleza kung'anga'aniwa kwa uwezo wa kiuchumi, kisiasa na kijamii;
na kwamba dini, fikra na utamaduni wa jumuiya yoyote (zikiwemo sanaa na fasihi
kwa kiwango fulani) huwa ni `itikadi'
na miundo maalum ya `kitabaka' ambayo
ni zao la miundo na matabaka ya kijamii yaliyomo wakati huo.
Umarx huchukulia kwamba jamii zote za kitabaka huzalisha mkururo
wa miundo ya urazini inayokinzana na kushindana. Katika jamii ya kikapitolisti,
kwa mfano, aina tofauti za mitizamo kuhusu maisha huwakilisha haja tofauti za
kitabaka ambazo hutegemea hasa mikinzano kati ya mapato na nguvu za kutenda
kazi. Kwa hivyo Umarx huhusisha itikadi na uzalishaji mali na jukumu lake
katika mivutano ya kisiasa katika jamii. Jinsi watu binafsi wanavyoelewa msingi
wa maisha yao hutokea kuwa kamba ya mvutano ambapo wanaweza ama kubadilika au kuendelezwa.
HOJA
ZA UMARX KWA UFUPI
i/ Katika historia ya mwanadamu, jamii na mahusiano yake, taasisi
zake namna yake ya kufikiri; mambo yote hayo hutegemea mabadiliko ya mfumo wa
uzalishaji mali. Yaani jinsi uchumi, uzalishaji, mgawanyo na umilikaji mali
unavyoendeshwa.
ii/ Mabadiliko ya kihistoria katika msingi wa uzalishaji mali
yanaathiri mabadiliko ya muundo wa matabaka ya jamii, na hivyo hutokeza (kwa
kila wakati) tabaka tawala na tawaliwa ambayo huwamo katika mapambano na
harakati za kugombea uchumi, siasa na faida za kijamii.
iii/ Urazini wa mwanadamu umeundwa na itikadi. Imani, thamani ya
kitu, namna za kufikiri na kuhisi. Ni kupitia hivi, mwanadamu huuona ulimwengu
wake, na huelezea yale yaliyomzunguka na yale anayoyaona kuwa kweli.
Kwa hiyo wazo kuu la U-Marx ni kwamba hata waandishi wa mkondo huo
huandika kwa kutumia falsafa ya Marx jinsi alivyoiona historia ambapo wazo kuu
ni kuwa: harakati za matabaka ndio msingi mkuu unaofanya mambo yawe kama
yalivyo.
Umarx katika Fasihi
§ Usanii ni uumbaji wa Ukweli katika maisha.
§ Ukweli unaooneshwa katika kazi za fasihi hiyo ni usahihi wa mambo
katika jamii? Kama ni Riwaya, Tamthilia, Ushairi na kadhalika inawakilishaje
ukweli?
§ Kazi za kisanaa zinatakiwa kuonesha mivutano iliyopo katika jamii
hasa kati ya wanyonyaji na manyonywaji.
Nadharia ya urasimi
Kwa
mujibu wa Njogu na Wafula (2007) Urasimi ni wakati maalumu ambapo misingi ya
kazi za sanaa huwekwa na kukubalika kuwa vipimo bora kwa kazi nyingine. Hii ina
maana kwamba kila jamii ina urasimi wake. Urasimi katika Kiswahili ulikuwepo
kati ya karne ya 18 na karne ya 18. Nao urasimi wa Kigiriki ulikuwepo baina ya
karne ya nne (KK) na takriban karne ya nne (BK). Ieleweke kuwa si sahihi
kuamini kama baadhi wanavyodhani kuwa unapozungumzia urasimi, huwa na maana ya
msingi ya kitaaluma iliyowekwa na Wagiriki na Waroma wa kale.
Sifa za urasimi kwa ujumla
Pamoja
na kwamba imeshatajwa hapo mwanzo kuwa kila jamii ina urasimi wake, lakini bado
tunaweza kutoa sifa za jumla za urasimi mahali popote ulipo. Kwa mfano:
·
Kazi
ya kirasimi huwasilishwa katika lugha inayoeleweka kwa urahisi. Hii ina maana kuwa wazo
linaelezwa moja kwa moja. Mitindo ya Kinjozi (mf. Nagona, Mzingile, Bina-Adamu,
Walenisi) haitumiwi. Uhalisia
unasisitizwa.
·
Kazi
nyingi za kirasimi hazichoshi kusoma. Hii ni kwa sababu kazi hizi ni kazi bora.
Husomwa mara nyingi na watu wengi na kila unapoisoma wazo jipya hupatikana.
·
Fani
na maudhui katika kazi za kirasimi ni mambo yaliyofinyangwa kwa kutumia mbinu
kamilifu na teule. Daima kuna ufungamano uliokamilika kati ya kinachoelezwa na
jinsi kinachoelezwa.
Katika
urasimi wa Kigiriki watu mashuhuri ambao walikuwa wanarejelewa sana ni kama Plato, Aristotle, Horace na Longino. Kazi maarufu kwa upande wa Tamthilia
inayoweza kutumika kama mfano wa urasimi wa enzi hizo ni kama ile ya Sofokile
iitwayo Mfalme Edipode (1971)
iliyotafsiriwa na Samuel Sateven Mushi.
URASIMI WA KISWAHILI
Njogu
na Wafula (2007) wanasema kuwa kazi za kirasimi katika fasihi ya Kiswahili
zipo. Hata hivyo uhakiki wa kirasimi
kuhusu kazi hizo ni nadra kupatikana. Msomaji wa kazi za kirasimi katika fasihi
ya Kiswahili anapaswa kuhitamidi uhakiki wake kutokana na utunzi wenyewe. Urasimi
wa Kiswahili ulifikia kilele chake katika karne ya 18 na 19. Kazi zinazodhaniwa
kuhusishwa na urasimi wa Kiswahili ni pamoja na hizi: Utenzi wa Al-Inkshafi, Utenzi wa Hamziyya, Utenzi wa Mwanakupona. Kazi za watunzi wa mashairi ya
unne (tarbia) kama Muyaka wa Muhaji, Mohammed Mataka na Ali Koti, “Sheria za kutunga mashairi na Diwani ya
Amri” (1954) (Amri Abeid).
Kazi
zingine za kirasimi kwa mujibu wa Njogu na Wafula (2007:21) ni kama vile riwaya
za; Kiu
(M.S.Mohamed, 1972), Utengano (S.A. Mohamed, 1980), Harusi
za Buldoza na Hadithi nyingine (S.A. Mohamed,
2005)
Pia
tamthilia kama: Kinjeketile, Mashetani (E.N. Hussein, 1969, 1971), Kilio
cha Haki (A.M Mazrui, 1982), Sauti ya Dhiki (A.Abdalla, 1973).
Sifa
ya fasihi ya Kiswahili katika misingi ya Kirasimi
· Huu ni wakati ambapo misingi ya
ushairi andishi wa Kiswahili ilipowekwa.
· Mengi ya mashairi ya kirasimi
yalipokezwa kwa mdomo na uhakiki pia ulifanywa kwa njia ya kimasimulizi.
· Mashairi yalitumia lugha teule
· Warasimi wa Kiswahili walitumia
lugha rahisi iliyoeleweka na ujirani wao bila shida yoyote.
· Masimulizi marefu kama vile utenzi
yana mwazo, katikati na hatimayake.
JE
ONTOLOJIA YA KIAFRIKA INAWEZA KUTUMIKA KAMA NADHARIA YA KUCHAMBULIA KAZI ZA
FASIHI ZA KIAFRIKA?.
Katika
kueleza mada hii tutaanza na ufafanuzi wa maana ya falsafa.
Wikipedia
kamusi elezo huru wanasema,falsafa ni neno linalotokana na neno la kigiriki
lenye maana ya upendo na hekima,wanaendelea kusema kuwa falsafa ni jaribio la
kuelewa na kueleza ulimwengu kwa kutumia akili inayafuata njia ya mantiki
.Falsafa huchunguza mambo kama vile kuweko,au kutokuweko,ukweli,ujuzi
,uzuri,mema, na mabaya,lugha na haki.
Kwa
mujibu wa Wamitila (2003 ) anasema, falsafa ni mawazo anayoyaamini mtu au
mwandishi kuwa yana ukweli unaotawala misingi
ya maisha.
Hivyo,
Falsafa ni taaluma au mtazamo unaochunguza matumizi ya dhana,kupima hoja,mbinu
za ujengaji hoja,kufanya uhakiki au tathimini,kuthibitisha au kutoa ushahidi wa
hoja zinazozungumzwana nadharia mbalimbali zinazohusu maisha.Mfano,kuua ni
tendo zuri au sio zuri?
Pia
fasihi ya Fasihi ya Afrika, tunaweza kusema inamaanisha maandiko kuhusu na
kutoka Afrika. Kama George Joseph
anavyodokeza katika ukurasa wa kwanza wa sura yake katika kitabu chake cha ‘understanding
contemporary Afrika’ wakati mtazamo wa fasihi ya ulaya kwa ujumla
inahusu herufi zilizoandikwa, dhana ya Afrika inahusu fasihi simulizi.Pia
ansema fasihi inaweza kuashiria matumizi ya maneno kisanaa kwa ajili ya sanaa
pekee.
Kwa
ujumla Fasihi ya Afrika ni sanaa yoyote, au fashi yoyote ile inayopatikana
katika bara la Afrika.
Pia
istilahi Nadharia, Kwa mujibu wa TUKI (2004), Wanasema nadharia ni mawazo,
maelezo, mwongozo uliopangwa ili kusaidia kueleza,kutatua au kutekeleza jambo
fulani.
Nao
Njogu na Rocha (2008), wanasema nadharia ni kioo cha kumulika kila jambo au
tendo limuhusulo binadamu ulimwenguni
inakuwa ngumu gizani.
Pia
Wamitila (1996), Anasema kuwa, nadharia ni maarifa ya kitaalamu ambayo msomaji
au mhakiki anapaswa kuyajua na kuyafahamu kabla ya kuanza kazi zake.
Hivyo
basi sisi tunakubaliana na TUKI, kwa kusema nadharia ni mawazo,
maelezo,mwongozo uliopagwa ili kusaidia kueleza,kutatua au kutekeleza jambo
fulani.
Ama
kuhusu Ontologia huu ni moyo wa falsafa. Ontologia ni tawi la falsafa
ambalo huchunguza asili ya vitu, (binadamu ametoka wapi?,dunia imetoke
wapi?,shetani ni nini?) Pia huchunguza uwepo wa vitu mbalimbali,vitu vilivyo
hai na vitu visivyokuwa hai, vinavyoonekana na visivyoonekana.
Maana
ya Ontologia tunaweza kusema ni falsafa ya utafiti wa asili nya kuwa wakati wa
kuwepo au ukweli.wanaendelea kusema neno ontolojia asili yake ni kigiriki.
Ontolojia, pia ni nadharia ya vitu na mahusiano
yao,inatoa vigezovya kubainisha aina tofauti ya vitu (halisi na
kufikirika,uwepo na haipo,kweli na bora,kujitegemea na tegemezi) na mahusiano
yao.
Naye
Mihanjo A, (2010) akimnukuu Anselm katika nadharia yake ya
kiontolojia,anselmamethibisha ontolojia kwa kuonyesha uishi wa Mungu.Anselm
ameelezea na kuonyesha asili na uishi wa Mungu.
Kwaujumla
Ontolojia ni tawi la falsafa ambalo huchunguza
asili ya vitu,(binadamu ametoka wapi?,dunia imetoke wapi?,shetani ni nini?)pia
huchunguza uwepo wa vitu mbalimbali,vitu vilivyo hai na vitu visivyokuwa
hai,vinavyoonekana na visivyoonekana.
Mkondo
tulioutumia ni mkondo wa falsafa za kijamii na kisiasa . Mkondo huu unazingatia
na kuangalia falsafa za jamii na siasa. Mkondo huu umefafanuliwa na kuelezwa na
Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere, Keneth Kaunda
na Kwame Nkurumah.
Tukianza
na ; Mwalimu Julius Kambalage Nyerere ambaye anatetea mkondo huu kwa
vigezo vifuatavyo;
Anadai
kuwa ujamaa wa kiafrika ni kama Afrika pana ujamaa ambao unakuwa mwendelezo wa
kifamilia na kuishi vizuri na watu vilevile anadai kuwa si ujamaa wa kimax
ambao unatetea mgogoro wa kitabaka.Yeye anaona asili ya ujamaa ni jamii za
kiafrika.
Sera
ya mipango inajadiliwa na kurekebishwa na watu wote.Kila mtu alifanya kazi katika ardhi ya jamii nzima na kila mtu
alipata matunda kulingana na kazi yake.
Anaendelea
kusema, ujamaa ni tofauti na ubepari unaolenga kumnyonya mtu.Hivyo wito wake ni
kuishi katika umoja kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni.
Mtaalamu
mwininge ni Kwame Nkurumah ambaye ametumia vigezo vifuatavyo;
Anadai
kuwa ujamaa ulikuwa msingi wa jamii za
kiafrika kuliko ubinafsi hivyo ubepari utaiharibu Afrika, Afrika haita kuwa huru
ikiwa itaendelea kuwa chini ya ubepari wa kimagharibi.
Huyu
aliathiriwa na falsafa ya kimarx na renin lakini hakutaka kuitumia kama ilivyo
alitaka uimalishwe ujamaa wenye asili ya kiafrika na vipengele vya kiislam na
kikristo vya ulaya.
Keneth
Kaunda alisema waafrika walifanikiwa
kuushinda ukoloni kwa sababu ya utu na sio nguvu katika kufikia
ukamilifu wa utu binadamu lazima alenge kufanana na mungu. Mungu ni usawa wa
kila kitu,mungu ni amani,upendo na utu,utu unavileta pamoja dini na siasa na
kuzaa taifa la watu wanaopendana.
Anamalizia
kwa kusema kuwa nguvu katika kujikomba si mbinu sahihi ya ukombozi bali nguvu
inaweza kutumika katika kujilinda
aliandika African humanism.
Baada
ya kueleza mkondo na vigezo vya wataalam wa falsafa za kijamii na siasa
,tunachambua riwaya ya kufikirika ambayo ni kazi ya fasihi ya kiafrika kwa
kutumia mkondo wa falsafa za kijamii na
kisiasa.
Riwaya
ya kufirika ameandikwa na Shahban Robert chapa ya nne mwaka (2008) kufikirika
ni riwaya inayohusu maisha na maswaibu yaliyo mkuta mfalme na malkia wa
kufikirika kwa kuchelewa kupata mototo.
Uchambuzi
wetu unaanza kama ifuatavyo;
Suala
la imani, imani ni kuwa uhakika wa mambo yatarajiwayo. Nyerere anasema kuwa
kila mtu alifanya kazi katika ardhi ya jamii nzima na kila mtu alipata matunda
ya kazi yake. Katika riwaya hii( uk3-4), unaonyesha jinsi ,mfalme anavyoamini
kuwa na watoto wengi ndio nguvu ya ufalme wake pia mfalme aliamini waganga,
kafara,ramli,hirizi,mazinguo,mashetani na watabiri.(Uk 8-11), ndio maana mfalme
aliwaita waganga wote wafike kwake ili waweze kuagua na kutabiri juu ya utasa
na ugumba wao.
Utawala,
katika riwaya hii mwandishi ameeleza suala la utawala kwa kumtumia mfalme kama
mfano wa mtawala mwenye uongozi mbovu wenye mabavu “(uk 4) mfalme alipoamua
waitwe waganga wote wa jadi mfano waganga wa
mashetani,makafara,watabiri,hirizi,wa mizizi,mazinguo na mashetani asiye
hudhulia apewe adhabu pia katika uk(23-25) mfalme anamfukuza mwalimu kazi.
Suala la ukombozi,ukombozi ni hali ya kujitoa kutoka
hali fulani kwenda hali nyingine .Katika
riwaya hii kuna ukombozi wa kisiasa,mwandishi amemtumia mjinga,ameonyesha jinsi
mjinga alivyosimama kisheria dhidi ya kifo kilichokuwa kinawakabili,kifo ambacho hakikuzingatia utu wa binadamu
(uk38.)KenethKaunda ansema, waafrika walifanikiwa kuushinda ukoloni kwa sababu
ya utu sio nguvu,katika kuufikia ikamilifu wa utu binadamu lazima alenge
kufanana na Mungu.
Matabaka katika jamii, matabaka ni mgawanyiko wa makundi
ya watu (kiuchumi,kisiasa,kielimu na
kijamii) katika jamii. Katika riwaya hii kuna matabaka makuu mawili,tabaka la
kwanza ni tabaka tawala,ambalo liliundwa na viongozi wa serikali,
wanasheria,mahatibu na wafanya biashara,tabaka tawaliwa lilikuwa ni
wakulima,(tabaka la mwisho),(uk 35-36).Matabaka katika jamii hayafai kwani
huondoa umoja,Nyerere anapinga matabaka hivyo wito wake ni kuishi katika umoja
kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni.
Athari za uongozi mbaya, huu ni uongozi usiofuata haki za
raia wake, baada ya maamuzi ya mfalme kuwaruhusu waganga mfano;waganga wa
mizizi walichimba mzizi ya mti,walitoa magome na kukata matawi ya miti,hali
iiliyopelekea ukame wa nchi na uharibifu
wa mazingira na makazi ya wanyama,waganga wa kafara walitumia pia kwa moto na
walihitaji damu za wanyama kwa ajili ya kafara,hivyo wanyama wengi walikufa.Ni
vizuri kufikiri jambo kabla ya kutenda.
Umuhimu wa uzazi, katika riwaya hii mfalme aliona
fahari yake yote si kitu kwani alikosa kuwa na mtoto (uk 1-3) anasema, “Nina
majeshi ya askari walioshujaa, waongozi hodari raia wema,watii ambao
hawalingani na Taifa lolote jingine katika maisha yake yote nashukuru kwa Bwana
vitu vya faraja,visivyokwisha lakini nina sikitiko kubwa kwa kukosa mtoto”.
Jamii ya kufikirika waliamini kuwa na watoto wengi ndio ujenzi wa nguvu wa
Taifa lao. (uk 3) Mfalme anaamini watoto ndio nguvu ya ufalme wake.
Mapinduzi ya kisiasa,na
kiutamaduni,mapinduzi
ni kufanya mabadiliko, yaani kuondoa utawala au siasa ya kwanza na kuingia
siasa mpya.katikas riwaya hii mjinga alitumia utu wake kufanya mapinduzi kwa
kumsaidia mototo wa mfalme kupata dawa hospitalini,na kupona,wanakijiji wa
kufikirika walizoea utamaduni wa kuwaamini waganga wa jadi na sio hospitali.Pia
katika siasa mjinga alijaribu kutetea haki na sheria ya utu,kwa kuzuia kafara
ya watu kutalewa kwani haina umuhimu.
Kazi
nyingine ya fasihi ipatikanayo Afrika ni
ushairi wa fungate ya uhuru.Fungate ya uhuru ni diwani iliyoandikwa na Mohamed
S. khatibu mwaka (1988). Diwani hii inajadili mambo yanayokwamisha ujenzi wa
jamii mpya katika nchi zetu za Afrika. Katika diwani hii tutachambua mambo hayo
kwa kutumia mkondo wa jamii na siasa. Uchambuzi wetu unaanza kama
ifuatavyo;
Kuwa na uongozi bora ,uongozi mbaya
ni kikwazo cha ujenzi wa jamii mpya.Katika diwani hii inaonyesha jinsi viongozi
wanavyotumia madaraka yao vibaya
kuwanyonya wananchi wa kawaida.Nyerere anasema sera ya mipango inajadiliwa
nakurekebishwa na watu wote.Pia ujamaa ni tofauti na ubepari unaolenga
kumnyonya mtu,hivyo yeye anasisitiza kuishi katika umoja kama ilivyokuwa kabla
ya ukoloni.Diwani inaonyesha kuwa uongozi mbaya ni kikwazo cha ujenzi wa jamii
mpya(uk15-16) shairi la “Viongozi wa
Afrika”,hapa mwandishi amekemea viongozi wanaotumia madaraka vibaya.Mashari
mengine yanayozungumzia uongozi mbaya ni “Fungate”,
“Waja wa Mungu”, “Wizi”, “Utawala”, “Njama”,
“ujamaa”.
Kupinga
vita ukoloni mamboleo,ukoloni mamboleo ni ile hali ya nchi kupata uhuru kisiasa
lakini njia nyingine za uchumi hutawaliwa au hubaki mikononi mwa mabepari
aunyingine.Kwame Nkurumah anasema ujamaa ni msingi wajamii za kiafrika kuliko
ubinafsi,hivyo ubepari utaiharibu Afrika,Afrika haitakuwa huru ikiwa itaendelea
kuwa chini ya ubepari wa kimagharibi.Katika shairi la “Ruya”,anonyesha kuwa wazungu ndio waliondoka katika ardhi ya Afrika
lakini unyoyaji bado upo.Pia katika shairi la “kunguru”,mwandishi ameonyesha athari za ukoloni mamboleo.
Kufanya mageuzi,mageuzi huleta mafanikio katika
ujenzi wa jamii mpya.Keneth Kaunda anasema waafrika walifanikiwakuushinda
ukoloni kwa sababu ya utu na sio nguvu,pia nguvu katika kujikomboa si mbinu sahihi
ya ukombozi bali nguvu inaweza kutumika katika kujilinda.Mwandishi naye ametoa
njia mbalimbali ili kufanikisha ukombozi katika shairi la “Unganeni”,pia mwandishi anapendekeza kutumia silaha katika mageuzi
ikiwa unyonyaji hautaondoka kwa njia ya amanimfano katika shairi la “Siku itafika” (uk 30) na “Nikizipata bunduki).
Umoja na Ushirikiano, hii ni mbinu mojawapo ambayo
mwandishi amependekeza kama mojawapo ya
njia ya ujenzi wa jamii mpya.Nyerere asisitiza watu kuishi katika umoja kama
ilivyokuwa kabla ya ukoloni.Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.Katika shairi
la “unganeni” (uk 1) mwandishi
anawataka waafrka wote tuungane ili kuendeleza mapambano ya kuleta haki na
usawa.
Kujenga
nchi itayofuata mfumo wa ujamaa, Nyerere anasema,ujamaa wa kiafrika ni kama
Afrika pana, ujamaa ambao unakuwa mwendelezo wa kifamilia na kuishi vizuri na
watu na sio ujamaa wa kimax unaotetea migogoro yakitabaka,mwandishi anashauri
ujamaa kuwa ni sululisho la wanyonge,shairi la “Ujamaa” shairi hili linajadili wapinzani wa ujamaa.Mwandishi ansema
ujamaa umeumbuliwa,umethiliwa,umekashifiwa na umesalitiwa.
Kupiga vita wizi wa mali ya umma,sehemu nyingi zimeoza kwa
wizi,ikulu na viongozi wamejiunga na wahalifu.Katika shairi la “Wizi” na “Kunguru” (uk19) ameeleza wezi waliotimuliwa na kutawanywa, shairi
la “Joka la mdimu” mwandishi
anatanabaisha watu kuhusu uwezekano wa wakoloni kurudi kwa umbotofauti lakini
athari ni zile zile,pia katika shairi la “Naona” (uk 33) anoonyesha taabu
wazozipata wakulima na malipo duni wanayopewa kwa mazao yao.
Kitabu
cha tamthiliya ya “Nguzo mama”
iliyoandikwa na Penina Mhando(1982).Tamthiliya hii
inasawiri na kuyaelezea matatizo mbalimbali yanayowakabili na kuwaelemea
wanawake wengi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.Kwa kutumia mkondo wa kisiasa
na kijamii tumechambua tamthiliya hii kama ifuatavyo;
Uongozi
mbaya, katika tamthiliya hii mwandishi ameonyesha umuhimu wa uongozi bora, na
kiongozi bora. Nyerere anasema ujamaa ni tofauti na ubepari unaolenga kumnyonya
mtu, anasisitiza kuwa kuishi katika umoja kama ilivyokuwa kabla ya
ukoloni.Katika kijiji cha patata kulikuwa hakuna ujamaa. Katika jamii kiongozi
anaweza kuipeleka jamii yake kwenye neema au kwenye mdomo wa simba kutegemeana
na uongozi wake anavyoupeleka (uk 22), kijiji cha patata kilikuwa na uongozi
mbaya wa kidikteta, mfano; Mwenyekiti, kamati ya halmashauri,wanatumia vitisho
kumlazimisha Bi nane kusema asichokijua (uk24).
Uvivu na Uzembe, huwa haufai katika jamii,katika
mkondo huu Nyerere anasema kila mtu alifanya kazi katika ardhi na kila mtu
alikula matunda ya kazi yake hivyo mtu
akiwa mzembe atakula matunda ya uvivu na uzembe ambayo si mema.katika kijiji
cha patata watu hawa walikuwa ni wavivu na wazembe,ndio maana ilipekea kufifia
na kushindwa kuinua “Nguzo mama”. Wanawake hawa walikuwa
hawawajibiki, mfano;(uk 34)
Mapenzi na ndoa, katika “Nguzo mama”kuna mapenzi
yasiyokuwa ya kweli,yanayoyojali pesa na usaliti kati ya wanandoa.Mapenzi haya
hayana utu kwani ndani ya utu kuna amani na upendo wa kweli.Usaliti huleta hali
ngumu katika familia mfano;familia ya Bi tano wanalala njaa kwa kukosa chakula
na mahitaji muhimu kwa kuwa Maganga baba yao anamaliza pesa zote kwa
wanawake.mfano ;
“Wee
Bi sita mshenzi unanichukulia mume wangu hivihivi kimachomacho”(uk 39)
Umoja na ushirikiano, hiki ni kitu muhimu sana katika
jamii Nyerere anasisitiza kuwa na umoja kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni .Asili
ya ujamaa ni Afrika na si ujamaa wa kimarx unaotetea matabaka.Kijiji cha patata
watu wake walikosa umoja na ushirikiano ndio maana walishindwa kuinua nguzo
mama kwani kila mtu anajali mambo yake Bi moja anaacha kazi anaenda kuangalia
khanga (uk 34
Dhuluma, hii imeghubika jamii yetu ya
leo,katika tamthiliya hii ya Nguzo mama mwandishi amejaribu kutuonyesha jinsi
jamii ya Patata kama zilivyo jamii iliyooza kwa dhuluma hasa pindi wanawake
wanapofiwa na waume zao,mfano Bi saba anaoonyesha jinsi gani wanawake wengi wa
kiafrikawanavyodhulumiwa mali na ndugu wa mwanaume zao pindi wanapofariki.Bi
saba baada ya kufiwa tu shemeji walikuja kugawana vitu.mfano( uk 43);
.
Kwa
kuhitimisha tunaweza kusema kumba riwaya hii ya kufikirika,tamthiliya ya nguzo
mama na ushairi wa fungate ya uhuru zimeweza kuchambuliwa vizuri na tawi hili
la ontolojia.Tumeweza kuona ni jinsi gani vitu halisi na vingine vya kufikirika
vikitendeka katika kazi hizi,vilevile suala zima la falsafa za kijamii na siasa
kama zilivyokwisha elezewa hapo mwanzo.Ujamaa unaonekana kuwa ni hali inayopelekea
maendeleo katika jamii,ontolojia ya kiafrika hutumika kuchambulia kazi za
fasihi za kiafrika.
MAREJEO
1.Mihanjo
A,(2010)Falsafa na ufunuo wa maarifa.Toriam.Morogoro
Tanzania.
2.Mohamed
S.k (1988)Fungate ya uhuru.Dar-es-salaam
university place(DUP).
3.Muhando
p (1982) Nguzo mama. Dar-es-salaam
university place(DUP).
4.Njogu
na Chimera R(1999)Ufundishaji wa
fasihi,Nadharia na Mbinu.Jomo Kenyatta.Nairobi
5.Tuki(2004)Kamusi ya Kiswahili sanifu.Taasisi ya
Uchunguzi wa Kiswahili.Dar-es-salaam.
6.Robert,S.(2008) Kufikirika.Mkuki na
nyota:Dar-es-salaam Tanzania.
7.Wamitila
K.W (1996) Utangulizi wa Kiswahili.Chuo
kikuu cha Dar-es-salaam.Dar-es-salaam.
CHIMBUKO LA RIWAYA YA KISWAHILI.
Katika
kujadili mada hii, mjadala huu, utajikita zaidi kutoa maana ya riwaya kutoka
kwa wataalamu mbalimbali, maana ya riwaya ya Kiswahili, maana ya chimbuko,
Kisha mjadala huu utaelekea zaidi katika kuelezea chimbuko la riwaya ya
Kiswahili kutokana na wataalamu mbalimbali waliopata kueleza asili ya riwaya
hiyo ya Kiswahili, na hicho ndio kitakachokuwa ni kiini cha swali. Mwisho
tutahitimisha mjadala wetu.
Kwa
kuanza na maana ya riwaya imejadiliwa kama ifuatavyo:
Wamitila
(2003), anasema riwaya ni kazi ya kinathari au kibunilizi ambayo huwa na urefu
wa kutosha, msuko uliojengeka vizuri, wahusika wengi walioendelezwa kwa kina,
yenye kuchukua muda mwingi katika maandalizi na kuhusisha mandhari maalumu.
Muhando
na Balisidya (1976), wanaeleza riwaya ni kazi ya kubuni, ni hadithi ambayo
hutungwa kufuatana na uwezo wa fanani kuibusha mambo kutokana na mazoea au
mazingira yake.Wanaendelea kusema kuwa riwaya yaweza kuanzia maneno 35000 hivi
na kuendelea.
Nkwera
(1978), anasema riwaya ni hadithi iliyo ndefu kuweza kutosha kufanya kitabu
kimoja au zaidi. Ni hadithi ya kubuniwa iliyojengwa juu ya tukio la kihistoria
na kuandikwa kwa mtindo wa ushairi iendayo mfululizo kwa kinaganaga katika
kuelezea maisha ya mtu au watu na hata taifa. Anaendelea kusema kuwa riwaya ina
mhusika mkuu mmoja au hata wawili.
Senkoro,
anasema riwaya ni kisa ambacho urefu wake unakiruhusu kitambe na kutambaa
vizingiti vingi vya maisha kama apendavyo mwandishi wake. Anaendelea kusema
kuwa ni hadithi ndefu ya kubuni, yenye visa vingi, wahusika zaidi ya mmoja na
yenye mazungumzo na maelezo yanayozingatiwa kwa undani na upana wa maisha ya
jamii.
Hivyo
inaonyesha kuwa ili kujua maana ya riwaya ni vyema kuzingatia mambo kadhaa
ambayo ndiyo ya msingi, na mambo hayo ni; lazima riwaya iwe na lugha ya kinathari,
isawiri maisha ya jamii, iwe na masimulizi ya kubuni na visa virefu, wahusika
zaidi ya mmoja, iwe na mpangilio na msuko wa matukio, lazima na maneno kuanzia
elfu thelathini na tano na kuendelea, na mwisho riwaya ni lazima ifungamane na
wakati yaani visa na matukio ni lazima viendane na matukio.
Baada
ya kuangalia maana ya riwaya kutokana na wataalamu mbalimbali sasa ni vyema
kutoa maana ya riwaya ya Kiswahili kabla ya kujadili chimbuko la riwaya.
Riwaya
ya Kiswahili ni ile ambayo inafungamana na utamaduni wa jamii ya waswahili
katika lugha ya kiswahili ambao hupatikanakatika nchi ya Afrika mashariki. Pia
ni ile riwaya ambayo inawahusu waswahili wenyewe.
TUKI
(2004) inasema chimbuko la maana yake ni mwanzo au asili.
Tanzu
za asili zinaonyesha kuwa ndio zilichangia kwa kiasi kikubwa sana katika kuibua
riwaya za Kiswahili.Na yafuatayo ni mawazo ya wataalamu mbalimbali juu ya
chimbuko la riwaya ya Kiswahili.
Madumulla
(2009), ameeleza kuwa riwaya ilitokana na nathari bunifu simulizi kama vile
hadithi, hekaya, na ngano inayosimuliwa kwa mdomo. Anaendelea kusema kuwa
fasihi ilitokana na maandiko ya fani ya ushairi hususan ni tendi za Kiswahili
katika hati za kiarabu kwa sababu ndiyo maanadishi yaliyotamba katika pwani ya
afrika mashariki. Wazungu na waarabu hawakubadilishana maarifa kwa urahisi na
hivyo pakapelekea kuwa na majilio ya taratibu za maandiko ya kinathari.
Mwanzoni riwaya zilitafsiriwa kwa Kiswahili toka katika lugha za ulaya na
kufanya riwaya za Kiswahili kutokea. Mfano wa riwaya hizo ni kama vile; Habari za mlima iliyoandikwa na Sheikh
Ali Bin Hemed (1980).
Senkoro
(2011) anaeleza kuwa riwaya zilizuka kutokana na maendeleo na mageuzi ya
kiutamaduni, uchangamano wa maisha ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, na
kiutamaduni yaliyopelekea haja ya kimaudhui zaidi ya ngano na hadithi fupi.
Anaendelea kusema kuwa riwaya za kwanza zilitafsiriwa toka riwaya za kizungu
mpaka za Kiswahili. Anasema riwaya mojawapo ni ile ya James Mbotela ya Uhuru wa Watumwa.
Ndiyo riwaya ya kwanza kutafsiriwa kwa Kiswahili. Pia anaeleza kuwa riwaya ni utanzu uliozuka kutokana na hali mahususi za kijamii. Riwaya
kama ile ya kiingereza ya Robinson Crusoe iliyoandikwa na Daniel Defoe ni miongoni mwa riwaya za mwanzo. Anasema
riwaya ilizuka kutokana na maendeleo na mageuzi ya kiutamaduni na viwanda.Suala
la ukoloni na uvumbuzi pia liliumba hali
ambazo zilihitaji kuelezwa kwa mawanda mapana zaidi ya yale ya ngano na hadithi fupi. Kupanuka
kwa usomaji hasa wakati wa vipindi vya mapinduzi ya viwanda huko ulaya
kilifanya waandishi waandike maandiko marefu kwani wakati huo ndipo walipoibuka
wasomaji hasa wanawake waliobaki majumbani wakati waume zao walipokwenda
viwandani kufanya kazi.
Mulokozi
(1996) anaeleza kuwa chimbuko la riwaya ya Kiswahili lipo
katika mambo makuu mawili ambayo; ni fani za kijadi za fasihi pamoja na mazingira
ya kijamii.
Fani
za kijadi
za
fasihi, Mulokozi anaeleza kuwa riwaya haikuzuka hivihivi tu bali
ilitokana na fani za masimulizi yaani hadithi, na ndipo zikapatwa kuigwa na
watunzi wa riwaya wa mwanzo. Fani hizo zilizopata kuchipuza riwaya za mwanzo ni
kama vile; riwaya za kingano, tendi,
hekaya, visakale, historia, sira, masimulizi ya wasafiri, insha na tafsiri.
Ngano, Mulokozi anasema, kuwa ni hadithi
fupi simulizi pia huwa ni hadithi za kubuni na nyinga hasa zinawahusu wanyama
wakali, pia zinahusu malaika, binadamu, mazimwi na majini. Anasema kuwa mara
nyingi ngano huwa na msuko sahihi na wahisika wake ni bapa na wahisika hao ni
mchanganyiko wa wanyama, mazimwi na binadamu. Anatolea mfano wa ngano zilizo
chukua visa vya kingano kuwa ni kama vile riwaya ya Adili na Nduguze ya Shaban Robart (1952), Lila na Fila ya Kiimbila (1966), Kusadikika ya Sharban Robart (1951) na baadaye yakafuata machapisho
mengine kama vile; Mfalme wa Nyoka
ya R.K. Watts. Dhamira za riwaya za
kingano ni kama vile choyo, mgongano wa kimawazo na tama.
Hekaya,ni hadithi za kusisimua kuhusu
masaibu na matukio ya ajabu yaani yasiyokuwa ya kawaida. Mara nyingi masaibu
hayo hufungamanishwa na mapenzi. Pia hekaya ni ndefu kiasi yaani sio ndefu
kiasi cha kama riwaya. Katika jamii ya waswahili hekaya zilikuwa zimeenea sana
kipindi cha kabla ya ukoloni.Mifano ya hekaya ni kama vile; Hekaya za Abunuasi ya C.M.C.A. 1915, Sultan Darai (1884), Kibaraka ya (1896) na hekaya ya Jonson,
F. na Brenn, E.W. Katika hekaya ya Alfa-Lela-Ulela ya kuanzia 1929. Hizo ndizo
baadhi ya hekaya za mwanzo lakini baadaye ziliathili riwaya za Kiswahili kama
vile; Hekaya ya Adili na Nduguze ya
Sharban Robart (1952), hekaya ya Ueberu
Utashindwa ya Kiimbila (1971), na Hekaya ya A.J.Amiri, ya Nahodha Fikirini,
(1972).
Tendi
(utendi),
ni hadithi ya kishairi kuhusu mashujaa wa kihistoria na wa kubuni, ambao waweza
kuwa ni wa kijamii au kitaifa. Kwa kawaida baadhi ya tendi zina sifa za
kiriwaya ila tu badala ya kuwa na umbo la kinathari zenyewe zina umbo la
kishairi. Kuna tendi za aina mbili ambazo ni tendi andishi na tendi simulizi.
Riwaya pevu kama tendi husawiri mawanda mapana ya kijamii na kihistoria. Huwa
na wahusika wababe yaani mashujaa wenye kuwakilisha pande zinazopingana. Mfano
wa tendi ni kama vile; Utendi wa Vita vya
Wadachi Kutamalaki Mlima ya Hemedi Abdallah, (1895), Utendi war as (Ghuli), utenzi
wa Fumo liyongo wa Mohamed Kijumwa K. (1913).Tendi katika riwaya za
Kiswahili imetumia wahusika wawili tu ambao ni wahusika wa kubuni na wale wa
kijadi wa kiafrika.
Visasili, hizi ni hadithi zinazohusu asili na
hatima ya watu, vitu, viumbe, ulimwengu na mataifa, na pia huangalia uhusiano
wa wanadamu na mizimwi pamoja na miungu. Hadithi za kivisasili zinapoonyeswa
huaminika kuwa yakweli tupu hasa kwa kusimulia matukio mengi ya kiulumwengu.
Mfano
wa visasili; Lila na Fila ya Kiimbila
(1966) ambayo imekopa motifu ya asili ya ziwa ikimba huko Bukoba. Hadithi ya Mungu wa Kikuyu huko Kenya. Roza Mistika ya Kezilahabi (1971), Nagona (1987) na Mzingile (1991), Siku ya
Watenzi Wote ya Sharban Robart.
Visakale, ni hadithi ya kale kuhusu mashujaa
wa taifa,kabila au dini. Mara nyingi visa kale huchanganya historia na
masimulizi ya kubuni, na hadithi hizi hupatikana karibu katika kila kabila kila
lugha.Baadhi ya visakale vya Kiswahili masimulizi huhusu chimbuko la miji ya
pwani, mijikenda, mwinyi mkuu huko Zanzibar.Visa kama hivi ndivyo
vinavyopelekea kuandikwa kwa riwaya za kiswahili. Mfano wake ni riwaya ya
Abdalla Bin Hemed bin Ali Ajjemy (1972) katika kitabu cha Habari za Wakilindi, Kisima
cha na Giningi ya M.S.Abdulla (1968) na ile Hadithi ya Myombekela na Bibi Bugonoka na Ntulanalwo na Buhliwali (1980) ya A.
Kitereza.
Visasuli, hizi ni hadithi zozote ambazo
huelezea chimbuko au asili ya kitu chochote, na maranyingi visasuli havina
uzito wowote kulinganisha na visasili.mfano wake ni; kwanini paka anapenda
kukaa jikoni (mekoni), Kwa nini mbuni hana mabawa yaani hapai angani, kwa nini
kima anamuogopa mamba, kwanini mbwa kuishi na binadamu, kwa nini fisi hupenda
kula mifupa. Katika hadithi hizi watu huwa hawaamini sana bali wanachukulia
kuwa ni utani tu.
Masimulizi
ya kihistoria,
haya ni masimulizi ya matendo ya, mwanadamu katika muktadha wa wakati, na ni
fani muhimu sana katika jamii yeyote ile. Masimulizi halisi ya kihistoria
yaweza kuwa ni ya mdomo au hata maandishi na yote huwa ni chemichemi nzuri ya
riwaya. Mfano wa riwya hizo ni; Habari za
pate za Fumo Omari Nabhany (1913) ambayo yalikuwa ni maandishi ya
masimulizi na uchambuzi. Riwaya zingine zilizoathiriwa na matukio ya kihistoria
ni; Uhuru wa Watumwa ya J. Mbotela
(1934), Kifo cha Ugenini ya O. Msewa
(1977), Kwa Heri Iselamagazi ya B.
Mapalala (1992) na Miradi Bubu ya
Wazalendo ya G. Ruhumbika (1992).
Sira, ni masimulizi ya kweli kuhusu maisha
ya mtu au watu. Sira huweza kuwa wasifu yaani zinazohusu habari za maisha ya
mtu zikisimuliwa na mtu mwingine au zaweza kuwa tawasifu yaani habari za maisha
ya mtu zikisimuliwa nayeye mwenyewe. Sira iliathiri kuchipuka kwa riwaya hasa
kwa kuonyesha masilimulizi ya maisha ya mtu toka utotoni mpaka uzeeni.
Masimuliza ya riwaya hizi yalikuwa katika masimulizi na hata katika maandishi
pia kwa maana kabla ya ukoloni yalikuwepo maandishi yaliyohusu maisha ya mitume
na masahaba.Mifano ya hadithi hizi ni; Kurwa
na Doto ya M. S.Farsy (1960),Rosa
Mistika ya Kezilahabi (1971),Kichwa
Maji ya Kezilahabi (1974) pamoja na
Dunia Uwanja wa Fujo (1975),Mzimu wa
Baba wa Kale ya Nkwera (1967),na riwaya ya Maisha Yangu baada ya Miaka Hamsini ya Sharban Robart (1951).
Msimulizi
ya wasafiri,
hizi ni habari zinazosimulia masibu nya wasafiri katika nchi mbalimbali. Hekaya
za riwaya chuku za kale zilisaidia kukuza riwaya. Mfano Alfa –Lela –Ulela na hadithi ya Robinson Kruso huko 1719
ilihusu safari ya baharini ya mhusika mkuu ambaye baadaye merikebu aliyokuwemo
ilizama, ndipo akalazimika kuishi peke yake katika kisiwa kidogo. Na katika
riwaya za Kiswahili kuna baadhi ya riwaya za masimulizi kama vile; Mwaka katika Minyororo ya Samweli Sehoza
(1921), Tulivyoona na Tulivyofanya Uingereza
(1932) ya Martin Kayamba. Na uhure wa Watumwa na Kwa Heri Eselamagazi.
Insha,
ni maandiko ya kinathari yenye kuelezea, kuchambua au kuarifu kuhusu
mada Fulani.Zipo insha za zina nyingi kama vile, makala, hotuba, tasnifu, michapo, barua, sira maelezo n.k
insha nyingi ni fupi mfano kuanzia maneno kama 500 na 10000 japo zingine zaweza
kuwa ni ndefu kiasi cha kuwa tasnifu za kufikia kiwango cha kuwa kitabu. Mfano
wa insha ni Siku ya Watenzi Wote ya
Sharban Robert na Kichwa Mji ya
Kezilahabi.
Shajara, ni kitabu cha kumbukumbu za
matukio ya kila siku. Uandishi wa shajara ulianzia huko Asia na baadaye ndio
ulipopata kuibuka ulimwenguni kote.Jadi hii ya kiasia iliathiri utunzi wa
riwaya hasa zile za kisira. Mfano wa shajara ni ile iliyotungwa na Lu Shun iitwayo Shajara ya Mwendawazimu
(1918).
Romansia
(chuku) hii ni hadithi ya
mapenzi na masaibu ya ajabu.Zikua maarufu sana huko Uingereza hasa karne ya 6
na 12 na Ufaransa pia zilikuwepo na pamoja na China ambapo hadithi zilizofanana
na riwaya zilitungwa.mfano hadithi za Hsiao-shuo
.Watunzi wa riwaya za kisasa zimekuwa na mafanikio makubwa sana kutokana na
riwaya hizo za chuku hii ni kwa sababu watunzi wengi wlikuwa wamesoma kazi
nyingi za riwaya za wakati ule.
Drama, maigizo mengi hasa ya tamthiliya
yaliathiri sana riwaya hasa kwa upande wa usukaji wa matukio na uchanganyaji wa
ubunifu na uhalisia. Mfano ni riwaya nyingi za Charles Dickens zina
msuko uliosanifiwa kwa uangalifu kama msuko wa tamthiliya.
Baada
ya kujadili fani za kijamii hatuna budi sasa ya kujadili mazingira ya kijamii kama yalivyopatwa kuelezwa na Mulokozi.
Anaeleza kuwa, kufikia karne ya 16 fani za kijamii zilikuwa zimekwisha enea na
kufahamika katika maeneo mengi, hivyo kulihitajika kuwe na msukumo wa kijamii,
kiteknolojia na kiuchuni. Msukumo huo wa kundeleza fani za kijadi ulikuwa ni wa
aina tatu ambao ni;
Ukuaji
mkubwa wa shughuri za kiuchumi huko ulaya, ukuaji huo ulifungamana na biashara ya baharini ya
mashariki ya mbali na kuvumbuliwa kwa mabara mawili ya amerika na ukuaji wa
viwanda hasa vya nguo huko ulaya. Mabadiliko haya yalizua tabaka jipya la
mabwanyenye waliomiliki viwanda na nyenzo nyingine za kichumi.Tabaka hilo
lilihitaji fani mpya za fasihi, lilikuwa na wakati wa ziada wa kujisomea, uwezo
wa kifedha wa kujinunulia vitabu na magazeti. Hivyo tangu mwanzo ilitawaliwa na
ubinafsi uliojidhihirisha kiitikadi. Kwa mfano Robinson Kruso ni riwaya
ilyosawili ulimbikizaji wa mwanzo wa kibepari. Ilimhusidhs muhusika asiye
staarabika aitwaye Fraiday au Juma. Ubinafsi huu ulijitokeza pia katika
utungaji wake, na haikusomwa hadharani bali kila mtu alijisomea mwenyewe
chumbani mwake.
Mageuzi
ya kijamii na kisiasa, mabadiliko haya yalifungamana na mabadiliko ya kiuchumi. Mataifa ya
ulaya yalianza kujipambanua kiutamaduni na kisiasa yaliyojitenga na dola
takatifu ya kirumi. Mabadiliko hayo yalianza kujenga utamaduni wa kitaifa na
mifumo ya elimu iliyo hiyaji maandishi katika lugha zao wenyewe. Mfano wa
mageuzi ya kijamii na kisiasa iliyofanyika ni kama vile; Misahafu ya Dini Kama
Biblia ilanza kutafsiriwa kwa lugha za ulaya, Martin Lther alichapisha Biblia kwa lugha za kidachi miaka ya 1534.
Hivyo basi inaonyesha kuwa kadiri elimu ilivyopanuka na nduvyo wasomaji wa vitabu
walivyoongezeka na kufanya kuwe hadhira kubwa nzuri ya wasomaji na watunzi wa
riwaya.
Ugunduzi
wa teknolojia ya upigaji chapa vitabu, yaani kwa kutumia herufi
iliyoshikamanishika.Ugunduzi huu uliofanywa na Johnnes Gutenberg huko ujerumani
mwaka 1450 uliorahisisha kazi ya uchapaji vitabu katika nakala nyingi nakuondoa
kabisa haja ya kunakili miswada kwa mikono. Bila ugunduzi huo kufanyika
haingewezekana kuchapisha riwaya nyingi na kuzieneza kwa bei nafuu.Nmifano ya
riwaya hizo ni kama vile; Pamela ya Samwel Richardson (1740).
Kutokana
na wataalamu mbalimbali kuelezea chimbuko la riwaya ya Kiswahili, inaonekana
kuwa, riwaya ni utanzu wa fasihi ambao kuzuka kwake kulifungamana na fani za
kijadi pamoja na mazingira ya kijamii. Fani za kijamii kama vile, ngano,
visasili, visasuli, visakale, insha, na nyinginezo zizosimuliwa bila ya
kuandikwa kabla ya karne ya 16, zilichochewa na kupewa mwendelezo baada ya
kukua kwa sayansi na teknolojia huko ulaya,hasa baada ya ugunduzi wa mitambo ya
kupiga chapa kazi za fasihi.
MAREJEO
Madumulla,
J.S. (2009), Riwaya ya Kiswahili,
Historian a Misingi ya Uchambuzi. Nairobi: Sitima Printer and
stations L.td.
Mulokozi,
M.M. (1996), Utangulizi wa Fasihi ya
Kiswahili. Dar es Salaam. TUKI.
Mhando,
P. na Balisidya, (1976), Fasihi na Sanaa
za Maonyesho. Dar es Salaam: Tanzania Publishing
House.
Nkwera,
F.V. (1978), Sarufi na Fasihi Sekondari
na Vyuo. Dar es Salaam: Tanzani Publishing House.
TUKI,(2004),Kamusi ya Kiswahili Sanifu.Nairobi.Kenya:Oxford
University Press.
Senkoro,F.E.M.K.(2011),
Fasihi Andishi.Dar es Salaam.Kauttu
L.t.d.
Wamitila,K.W.(2003),Kamusi ya Fasihi, Istilahi na Nadharia.
Nairobi: Focus Publication.
DHANA NA DHIMA
YA USHAIRI WA KISWAHILI
Katika makala hii tutaeleza
historia fupi ya ushairi na mawazo ya wataalamu mbalimbali juu ya ushairi.
Tukianza na Mulokozi (1996)
anasema, wataalamu wengi wamekubaliana kuwa asili ya ushairi wa Kiswahili ni
tungo simulizi, hasa ngoma na nyimbo zinazofungamana na ngoma.
Kabla ya karne ya 10 BK ushairi wa Kiswahili ulikuwa
ukitungwa na kughanwa kwa ghibu bila
kuandikwa. Wataalamu hao waliojadili
historia ya ushairi ni kama (Chiraghdin 1971: 7:10, Massir 1977:1 Ohly 1985:467).
Dhana ya ushairi imejadiliwa kwa kuangalia makundi mawili ya waandishi wa mashairi
ya Kiswahili, makundi hayo ni kundi la
wanamapokeo, na kundi la wanausasa.
Tukianza na
kundi la wanamapokeo. Wataalamu
mbalimbali wamejadili dhana ya ushairi kama ifuatavyo:
Kwa mujibu wa Shaaban Robert (1968) anasema kuwa Ushairi ni Sanaa ya vina inavyopambanuliwa, kama nyimbo, mashairi na tenzi zaidi ya kuwa sanaa ya vina, ushairi una
ufasaha wa maneno machache au muhtasari,
uliza swali wimbo, shairi na tenzi ni
nini? Wimbo ni shairi dogo na shairi ni
wimbo mkubwa na utenzi ni upeo wa ushairi pia anauliza kina na ufasaha huweza
kuwa nini? Anasema kina ni mlingano wa sauti za herufi, na kwa
maneno mengine huitwa mizani ya sauti, na ufasaha ni uzuri wa lugha, mawazo,
maono na fikra za ndani zinapoelezwa kwa
muhtasari wa ushairi huvuta moyo kwa namna ya ajabu. Hivyo
katika ufafanuzi wake wa ushairi inaonesha dhahiri kuwa Shaaban Robert
anagusia vipengele viwili maalumu yaani fani ya ushairi na maudhui ya ushairi.
Naye Mnyampala (1970) kama alivyonukuliwa na Massamba
D.P.B. katika Makala ya Semina ya
Kimataifa ya waandishi wa Kiswahili
(2003) anasema ushairi ni msingi wa maneno ya hekima tangu kale. Ndicho kitu kilicho bora sana katika maongezi
ya dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata iliyopangwa
kwa urari wa mizani na vina maalumu kwa shairi.
Hapo tunaona dhahiri kuwa Mnyampala anauona ushairi ukiwa
umejengwa na vitu viwili mahususi, ambavyo ni maneno ya hekima na sanaa yenyewe.
Tena Mnyampala katika dibaji hiyo hiyo anasisitiza juu ya sanaa ya
ushairi kwa kusema:
(i)
Shairi liwe na
“poetical Swahili” yaani Kiswahili
kinachohusu mwendo wa mashairi bora.
(ii)
Shairi liwe na
urari wa mizani kamili zinazohusika na ushairi wa kawaida waka lugha ya
Kiswahili kisichokuwa na kashfa au matusi
ndani yake.
(iii)
Shairi
liwe na vina vinavyopatana hususani
mwishoni mwa kila ubeti kwa shairi lolote zima ingawa vina vya katikati
vikosane kwa utenzi wake.
(iv)
Shairi lazima
liwe na muwala
(v)
Lisizidi mno
maneno ya kurudia rudia.
Kwa mujibu wa Abdilatifu Abdalla (1973) katika makala ya
semina ya kimataifa ya waandishi wa
Kiswahili anasema maana ya ushari ni utungo ufaao kupewa jina la ushairi ni utungo wowote tu bali ni utungo
ambao katika kila ubeti wake kuna ulinganifu wa vina vitukufu vilivyopangwa
kimoja baada ya chenziye, wenye vipande vilivyoona ulinganifu wa mizani
zisizo pungufu wala kuzidi na vipande hivyo viwe vimetandwa na maneno ya mkato
maalumu na yenye lugha nyofu, tamu na
laini, lugha ambayo ni telezi kwa ulimi wa kutamka, lugha ambayo ina uzito wa
kifikra, tamu kwa mdomo wa kuisema, tambuzi kwa masikio ya kuisikia, na yenye
kuathiri moyo uliokusudiwa na kama ilivyokusudiwa.
Kutokana na
hayo yaliyokwishasemwa, tunaona kuwa dhana ya ushairi ya wana jadi imefinywa
kwenye umbo maalumu lenye utaratibu wa vina na urari wa mizani ambayo kwa kweli
ni dhana ya kimaandishi.
Kundi la pili ambalo limefafanua dhana ya ushairi ni kundi la wanausasa. Hawa wamejadili dhana ya ushairi kama
ifuatavyo:
Kwa mujibu wa Wamitila (2010) anasema ushairi ni sanaa
inayotambulishwa na mpangilio maalumu wa sentensi au vifungu, mpangilio ambao
una mdundo maalumu au ruwaza fulani
inayounda wizani, lugha ya mkato na mafumbo pamoja na mpangilio usio wa kawaida
wa vifungu fulani.
Mulokozi, (1989) anasema ushairi ni sanaa ya lugha
inayoonesha au kueleza jambo, wazo au
tukio kwa namna inayovuta hisia kutokana na mpangilio maalum wa maneno yaliyoteuliwa, kauli za
mkato, picha na tamathali na
inayowasilishwa kwa hadhira kwa njia ya nyimbo au maandishi. Kwa mujibu wa ufafanuzi huo ushairi hueleza
tu, bali hudhihirisha, au huonyesha kusawiri,
anaendelea kusema ushairi huwajumuisha watu wawili au zaidi. Kihisia katika tukio linalowagusa wote, ukawatosa katika dimbwi la uchungu, au
furaha, hasira au ridhaa, na kuwatoa tena wakiwa wameburudika na kuelimika.
Kwa sababu hii ushairi
ndiyo sanaa ya fasihi inayokaribiana
zaidi na muziki na mara nyingi
sanaa hizi mbili hufungamana.
Mulokozi na Kahigi (1979) wanamnukuu Kezilahabi kwa
kusema kuwa ushairi ni tukio, hali au wazo ambalo limeonyeshwa kwetu kutokana
na upangaji mzuri wa maneno fasaha yenye
mizani kwa ufupi ili kuonyesha ukweli fulani wa maisha jambo ambalo halikutiliwa maanani katika
fafanuzi la wataalamu hawa ni dhima ya fasihi na ushairi kama vyombo vya
kuburudisha na kustarehesha watu.
Wataalamu hawa wanaendelea kusema kuwa ushairi lazima
uguse hisi, lazima umsisimue yule anayeusema, kusoma au kuimba na yule ausikilizaye. Hivyo shairi lisilogusa hisi ni kavu na butu hata kama limetafsiriwa katika vina na urari wa
midhani, shairi hilo litaishia kuhubiri tu.
Kwa ujumla wanausasa wanadai kuwa
ushairi ni sanaa inayopambanuliwa kwa
mpangilio maalumu wa maneno fasaha na
yenye muwala, kwa lugha ya mkato, picha au stiari au ishara.
Katika usemi, maandishi, au mahadhi ya wimbi ili kueleza wazo au mawazo,
kujifunza au kueleza tukio au hisi fulani.
Kuhusu maisha au mazingira ya binadamu kwa njia inayogusa moyo.
Kutokana na mawazo hayo ya washairi mbalimbali wa
kimapokeo na wana usasa wote wameonesha
mambo fulani ambayo yamefanana kwa
namna moja ua nyingine.
Wote wanakubaliana kwamba katika ushairi fani na maudhui
ni vitu vya muhimu kabisa na kwamba kila kimoja
kati ya vitu hivyo kina wajibu maalumu.
Pia washairi wengi huamini kwamba lugha ya ushairi lazima
iwe ya mkato, yaani iweze kusema mambo mengi kwa kutumia maneno machache.
Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa ushairi ni sanaa ya lugha yenye ughunaji na yosawiri,
kueneza au kuonesha jambo lenye hisi au
hali fulani kwa namna ya kuvutia hisia
katika mpangilio mahususi wenye urari wa
vizani na sauti.
Baada ya kuangalia
wataalamu mbalimbali walioelezea dhana ya ushairi, zifuatazo ni dhima za ushairi wa
Kiswahili.
Ushairi husaidia kurithisha maarifa kwa jamii, kupitia
ushairi jamii inaweza kujifunza mambo mbalimbali kama vile namna ya kuepukana
na magonjwa, umuhimu wa kutunza mazingira.
Mfano: shairi la
Binti katika diwani ya dhifa iliyoandikwa na Kezilahabi e, Mwandishi
anarithisha jamii maarifa kwa kusisitiza jamii izingatie umuhimu wa elimu:
anasema
Soma
soma kwa kujiamini.
Elimu ni kikata kiu,
Huondoa pia ukungu,
Pasipo njia pakawa
Fanya kazi utayopata,
Kazi ni kinga ya heba
Sasa umekuwa na uwe,
Huu usinga na kupa
Na unyoya nakuchomekea
nyweleni.
Ushairi husaidia kuhamasisha jamii, ushairi
hutumiwa kama njia ya kuwahamasisha wanajamii katika shughuli mbalimbali.
Mfano: katika utendi wa Fumo Loyongo ubeti wa kumi na tatu, anahamasisha wanajamii kuwa na nguvu kama
simba, anasema:
“Ni mwanaume Swahili
Kama simba unazihi
Usiku na asubuhi
Kutembea ni mamoya.
Pia katika diwani
ya Wasakatonge, shairi la Wanawake wa Afrika, mwandishi anawahamasisha
wanawake kujikomboa, anasema:
Wanawake
wa Afrika
Wakati
wenu umefika,
Ungeneni
Shikaneni
Mjitoe
utumwani,
Nguvu
moja!
Ushairi husaidia kudumisha na
kuendeleza utamaduni katika jamii, kupitia ushairi wanajamii wanadumisha
na kuendeleza utamaduni wao na kwa njia
hii huhakikisha kuwa unabaki hai. Mfano
katika tohara huwa kunakuwa na nyimbo
zenye mafunzo kwa vijana wanaofanyiwa jando na unyago, kama vile kuandaa
wanaohusika kwa majukumu ya utu uzima.
Ushairi huburudisha hadhira, ushairi ni
nyenzo kuu ya burudani, katika jamii licha ya majukumu mengine ya nyimbo,
msingi mkuu ni uwezo wake wa kuweza
kuathiri hisia za wasikilizaji au washiriki wake na kuwaburudisha. Mfano katika shairi la watoto wawili kutoka
kwa mwandishi Kezilahabi Kichomi (1974 uk. 62):
Mtoto wa
tajiri akilia hupewa mkate,
Mtoto wa
tajiri akilia hupewa picha ya kuchezea,
Akilia
mtoto wa tajiri huletewa kigari akapanda,
Akiendelea
kulia hupanda mgongo wa yaya,
Akikataa
kunyamaza ulimwengu mzima hulaumiwa.
Ushairi husaidia kukuza lugha kwa kawaida
ushairi hutungwa kwa lugha nzito yenye ishara
na jazada zinazoeleweka na wanajamii wanaohusika, na kwa njia hii hutusaidia kukuza hisia za kujitambua kwao
kama watu wa kundi fulani lenye mtazamo, imani na mwelekeo fulani.
Hivyo kwa kuhitimisha tunaweza kusema kwamba aidha
ushairi uwe wa kimapokeo au wa kisasa
unaonesha mambo muhimu yanayoilenga jamii husika. Mfano katika mambo ya kidini, kisiana na
kiutamaduni.
MAREJEO
Abdilatifu, a (1973), Sauti ya Dhiki, Oxford London.
Kezilahabi, E (1974), Kichomi, Heinemann; London.
Massamba, D.P.B. (2003), Utunzi wa
Ushairi wa Kiswahili katika makala za Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa
Kiswahili (III). Fasihi. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Dar es
Salaam.
Mulokozi, M.M na Kahigi K.K. (1979), Kunga za Ushairi na Diwani Yetu, TPH,
Dar es Salaam.
Mulokozi, M.M. (1989) Uchambuzi wa
Mashairi: Mulika Namba 21; TUKI,
Dar es Salaam.
Mulokozi, M.M. (1996), Fasihi ya
Kiswahili, chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dar es Salaam.
Robert, S (1968) Kielelezo cha Insha. Nelson
London.
TUKI, (2003), Makala za Semina ya Kimataifa ya
Waandishi wa Kiswahili III : Utunzi wa Ushairi wa Kiswahili, TUKI Dar es
Salaam.
Wamitila, K.W. (2010) Kichoche
cha Fasihi Simulizi na Andishi, English Press. Nairobi.
CHIMBUKO LA USHAIRI; UBORA NA
UDHAIFU WAO.
Dhana
ya ushairi imejadiliwa na wataalamu mbalimbali huku kila mmoja akitoa fasili
yake. Baadhi ya wataalam hao ni kama ifuatavyo:
Mssamba,
D.P.B. (2003) akimnukuu Shaban Robert, anasema; “ushairi ni sanaa ya vina
inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi zaidi ya kuwa na sanaa ya vina
ushairi unaufasaha wa maneno machache au muhtasari.”
Mnyampala
(1970) anasema kuwa “ushairi ni msingi wa maneno ya hekima tangu kale ndicho
kitu kilichobora sana maongozo ya Dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha
nzito yenye kunata iliyopangwa kwa urari wa mizani na vina maalum.”
Amri
Abeid (1954:1) anasema kuwa “ushairi au utenzi ni wimbo, hivyo kama shairi
haliimbiki halina maana.”
Encyclopedia
American (EA) inaeleza kuwa ushairi ni kauli zenye hisia na ubunifu, mpangilio
fulani wenye urari, uwasilishaji wa tajiriba au mawazo ya mtunzi kwa maana
ambayo huibua tajiriba kama hiyo katika nyayo za wasomaji au wasikilizaji na
kutumia lugha ya picha yenye wizani wa sauti.
Mulokozi
na Kahigi (1982) wanasema ushairi ni “sanaa inayopambanuliwa kwa mpangilio
maalum na fasaha na wenye muwala, kwa lugha ya picha, sitiari au ishara katika
usemi, maandishi au mahadhi ya wimbo ili kuleta wazo au mawazo, kufunza au
kueleza tukio au hisia fulani kuhusu maisha au mazingira ya binadamu kwa njia
inayogusa moyo.”
Hivyo
basi tunaweza kusema kuwa ushairi ni kazi ya sanaa yenye kuandikwa au kuimbwa
kwa kufuata kanuni za ushairi au kutofuata kanuni za ushairi ikiwa na maana
kuwa ushairi waweza kuwa wa kimapokeo au wa kisasa ilimradi ushairi huo uwe na
ujumbe.
Dhana
ya chimbuko inafasiliwa na TUKI (2004) kuwa ni mwazo au asili ya kitu.
Baadhi
ya wataalamu wameweza kuelezea chimbuko la ushairi wa Kiswahili kwa kuzingatia
mitazamo au nadharia mbili ambazo ni kama zifuatazo:
Nadharia
ya kwanza inadai kuwa; Chimbuko la ushairi wa Kiswahili ulitokana na ujio wa
Waarabu.
Na
nadharia ya pili inasema kuwa; Chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni zao la jamii
ya waswahili wenyewe.
Kwa
kuanza na nadharia ya kwanza isemayo kuwa chimbuko la ushairi wa Kiswahili
ulitokana na ujio wa Waarabu ambayo inaungwa mkono na wataalam mbalimbali kama
vile Lyndon
Harries (1962) na Knappet (1979)
Kwa
kuanza na Lyndon (1962) “Swahili Poetry” anatoa hoja tatu ambazo ni ushairi wa
Kiswahili umetokana na Uislamu, ushairi ulianzia kwenye upwa wa kaskazini mwa
Kenya hususani Lamu. Na maudhui ya ushairi wa Kiswahili yalitokana na ushairi
wa Kiarabu. Utungo wa kwanza wa ushairi andishi wa Kiswahili ni Tambuka,
Mwengo bin Athmani (1728)
Ubora
wa nadharia hii au mtazamo wa Harries kuhusu chimbuko la ushairi wa Kiswahili
ni kwamba umesaidia wengine kuendelea kuchunguza zaidi kuhusu chimbuko la
ushairi wa Kiswahili.
Udhaifu
wa nadharia hii ni kuwa si kweli kwamba ushairi wa Kiswahili uliletwa na
Uislamu bali ulikuwepo hata kabla ya ujio wa Uislamu, kwani ushairi
hautenganishwi na jamii husika. Hivyo jamii za waswahili walitumia Nyanja
mbalimbali za ushairi katika shughuli zao mbalimbali au shughuli zao za kila
siku, kama vile; shughuli za kilimo na ufugaji.
Pia
ushairi wa Kiswahili ulianza karne ya 10BK na ushairi wa Kiswahili ulikuwa
ukitungwa na kughanwa kwa ghibu bila kuandikwa. Wataalam wengi wanakubaliana
kuwa asili ya ushairi wa Kiswahili ni tungo simulizi hasa ngoma na nyimbo.
Udhaifu
mwingine katika mtazamo wake wa kusema kuwa ushairi ulianzia pwani ya kaskazini
ya Kenya si kweli kwa kuwa waswahili walikuwepo hata sehemu nyingine kama vile
Kilwa na Bagamoyo ambapo ushairi wa Kiswahili ulitumika.
Hoja
ya kusema ushairi wa Kiswahili ulitokana na Kiarabu haina mashiko kwa kuwa
waswahili walikuwepo hata kabla ya waarabu na walikuwa na ushairi wao isipokuwa
ujio wao ulileta athari kubwa kwa kuwa ulichanganya na mambo ya dini ya
kiislamu na hati.
Knappert
(1979) “Four centuries of Swahili verse” anasema; “Ushairi wa Kiswahili
ulichipuka kwenye upwa wa Kenya kutokana na nyimbo na ngoma za waswahili na
ulianza katika karne ya 17 na pia ni ushairi wa Kiislamu wenye kuchanganya sifa
za tungo za kiafrika na za kiajemi.
Ubora
wa hoja hii ni kwamba, ni kweli Knappert amekubali kuwa, ushairi wa Kiswahili
ulitokana na waswahili wenyewe.
Hata
hivyo hoja yake ina udhaifu kwa kuwa ushairi wa Kiswahili ulianza kabla ya
karne ya 10 BK na pia amejikita katika maudhui ya mambo mengine kama vile
siasa, uchumi na kijamii. Vilevile amechanganya chimbuko la ushairi wa
Kiswahili na Uarabu.
Nadharia
ya pili inasema kuwa ushairi ni zao la waswahili wenyewe. Nadharia hii imejadiliwa na
wataalam mbalimbali akiwemo Shaban
Robert, Jumanne Mayoka (1993) na F.E.M.K. Senkoro, Mulokozi na Sengo.
Jumanne,
M. Mayoka (1993) anasema ushairi umetokana na jamii ya wanadamu wenyewe na
umesheheneza ukwasi mkubwa wa lugha ambayo imekuwa ikitumika katika hatua zote
za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni katika historia ambayo mwanadamu amepitia,
Kwa mfano kuwa msamiati uliotumika tangu enzi za kuishi mapangoni, enzi za
uwindaji, ujima, utumwa, vita vya makabila, uvamizi wa wageni, ukoloni na
harakati za kupambana na ukoloni hadi kupata uhuru na maendeleo yake.
Ubora
wa hoja hii ni kwamba ina mashiko ndani yake kwa sababu, kila jamii ina sanaa
yake na ushairi ni moja kati ya sanaa hizo ingawa inaweza ikaathiriwa na sanaa
ya jamii nyingine. Pia ushairi umekuwa ukikua na kuendelea kadri jamii
inavyokuwa na kuendelea.
Udhaifu
wa hoja hii ni kwamba si kweli kuwa katika kipindi hicho ushairi ulikuwa tayari
umesheheni ukwasi mkubwa wa lugha, na kama ulikuwa kweli umesheheni huu ukwasi
wa lugha alipaswa kutuonesha huo utajiri wa lugha anaouzungumzia katika
ushairi.
Senkoro
(1988) anasema kuwa ushairi uliibuka
pale lugha ilipoanza katika kipindi cha uhayawani (kipindi ambacho mwanadamu
alipoanza kupambana na mazingira yake) kwenda katika kipindi cha urazini
(maana) ili kumwezesha binadamu na mazingira yake kwa mfano, zana za kazi
zilizotumika ziliwafanya waimbe kwa kufuata mdundo wa zana hizo.
Ubora
wa hoja hii ni kwamba unathibitisha kuwa chimbuko la ushairi ni waswahili wenyewe,
kwani umefanikiwa kueleza kuwa katika jamii yoyote ile maendeleo ya kiuchumi,
kisiasa na kijamii huambatana au huenda sambamba na maendeleo ya sanaa
mbalimbali ikiwemo ushairi uliotumika katika harakati mbalimbali za maisha ya
mwanadamu.
Pamoja
na kuwa nadharia hii imeonesha kukubalika na wataalamu mbalimbali kama vile Senkoro, Mayoka na Shekhe Amri Abeid, lakini bado ina mapungufu. Hii ni kwa sababu
imeshindwa kuonesha muda maalumu ambapo ushairi wa Kiswahili ulianza na ni wapi
ulianza kutumika. Hili ni suala ambalo linaumiza vichwa vya wataalamu
mbalimbali hadi hivi sasa, kwani hakuna mtaalamu yoyote aliyefanikiwa kuonesha
ni wapi na ni lini ushairi wa Kiswahili ulianza.
Hivyo
basi, kutokana na nadharia hizo mbili tunaungana na nadharia inayosema kuwa,
chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni zao la waswahili wenyewe, kwa sababu
waswahili wana utamaduni wao ambao ulikuwepo kabla ya ujio wa Waarabu. Na
waliutumia ushairi huo katika shughuli mbalimbali za kijamii, kwa mfano katika
harusi, jando na unyago.
MAREJEO:
Knappert,
J. (1979). Four centuries of Swahili
Verse. Heinemann. London.
Mayoka,
J.K. (1993). Mgogoro wa Ushairi na Diwani
ya Mayoka. Ndanda Mission
Press.Tanzania.
Mulokozi,
M.M. (1996). Fasihi ya Kiswahili.Chuo
Kikuu cha Dar-es-Salaam.
Senkoro,
F.E.M.K. (1987). Ushairi, Nadharia na
Tahakiki. DUP. Dar-es-Salaam.
TUKI.
(1983). Makala ya Semina ya Kimataifa ya
Waandishi wa Kiswahili. (Toleo la III) TUKI.Dar-es-Salaam.
TUKI.
(2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu.TUKI.Dar-es-Salaam.
UTHIBITISHO USHAIRI WA KISWAHILI
UMEPITIA MIHULA ANUAI
Maana ya ushairi.
Massamba
(2003) akimnukuu Shaaban Robert (1968) anasema Ushairi ni sanaa ya vina
inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi. Zaidi ya kuwa sanaa ya vina na
mizani, ushairi una ufasaha wa maneno machache au muhtasari.
Senkoro
(1988) Katika kitabu chake cha Ushairi, “Nadharia na Tahakiki” anasema ni
utanzu wa fasihi utumiao mpangilio wa lugha ya mkato, picha, iliyopangwa kwa
njia iletayo mapigo mahususi au yaliyomo ndani yake.
Kezilahabi,
(1974) katika kitabu chake cha “Kichomi”
anadai ushairi ni tukio, hali, au wazo, ambalo limeoneshwa kwetu kutokana na
upangaji mzuri wa maneno fasaha yenye mizani kwa ufupi ili kuonesha ukweli
fulani wa maisha.
Wamitila, (2008) ushairi ni utungo wa sanaa ya lugha na
mpangilio maalum wa mishororo, ama kisauti na kwa maneno mateule kwa kubuni
mbinu za lugha zenye mnato na mbinu nyingine za kibalagha na kimtindo
zinamwezesha mtunzi kuwasilisha ujumbe kwa kifupi na kwa mkokotezo mkubwa unaoelezea
hisia, tukio, ama hali kwa lugha ya mvuto.
Kwa
ujumla ushairi ni sanaa ya lugha ya mkato yenye ughunaji inayosawiri, kueleza
au kuonesha jambo, hisia au katika mpangilio mahususi wa maneno wenye urari wa
vina na wizani wa sauti.
Baada
ya kuangalia tofauti ya ushairi ifuatayo ni tafsiri ya ushairi wa Kiswahili.
Ushairi wa kiswahili umeelezwa na Senkoro (1988) kuwa ni ule ushairi unaotumia
lugha ya Kiswahili katika kuwasilisha mawazo, fikra na vionjo vya moyo wa watu
wanaotumia lugha ya Kiswahili.
Ushairi
wa kiswahili umefafanuliwa tena katika mitazamo mingine miwili. Mtazamo wa
Kimapokeo na mtazamo wa Kisasa.
Katika mtazamo wa Kimapokeo wanadai kuwa ushairi wa kiswahili ni
ule unaotungwa kwa kufuata kanuni za urari wa vina na mizani, ambazo ni kanuni za
ushairi wa Kiswahili. Miongoni mwao ni wazee na vijana wa UKUTA ( Chama cha
usanifu wa Kiswahili na ushairi Tanzania) Amri Abedi.
Mtazamo wa wanausasa; Ushairi wa Kiswahili si lazima
ufuate kanuni za utungaji wa mashairi. Vina na mizani si vya lazima katika
ushairi. (Kezilahabi, E, Mulokozi, M.M na K. Kahigi) maelezo haya yanayofafanua
maana ya ushairi wa Kiswahili yana mapungufu
kadhaa kama ifuatavyo;
Wanamapokeo
wameshindwa kuelezea vipengele vya maudhui. Wamejikita zaidi katika vipengele
vya kifani (urari wa vina na mizani) hawajaeleza waswahili ni watu gani?
Mashairi haya yanazungumzia mawazo yapi?
Wanausasa
wamepinga hoja tu ya wanamapokeo kuwa ushairi wa kiswahili si lazima ufuate
kanuni za urari wa vina na mizani. Hawajatoa maana yao kuhusu ushairi wa
Kiswahili.
Kwa
hiyo, ushairi wa Kiswahili ni utungo unaotumia lugha ya kiswahili kuelezea
maisha ya waswahili (watumiaji wa lugha ya kiswahili) katika Nyanja mbalimbali
za maisha, wenye kusheheni fani na maudhui yanayohusu watumiaji wa kiswahili
Ama
kuhusu Muhula ni kipindi fulani katika mwaka kinachohusishwa na tukio fulani
pia huzingatia kigezo cha mwaka muafaka.
Mihula ya ushairi wa kiswahili. Kwa
mujibu wa Kezilahabi (1983) amebainisha Mihula ifuatayo;
Muhula wa Urasimu (hadi 1885). Katika kipindi hiki
kanuni za utunzi ziliwekwa na ushairi ulitawaliwa sana na mitazamo ya kidini na
Kimwinyi. Mfano; wa tungo za ushairi zilizokuwepo kipindi hiki ni utenzi wa tambuka 1728 kilichoandikwa na Bwana Mwengo, utenzi wa Hamziyyah 1690 Sayyid Abdarus , utenzi wa Al-Inkishafi
utenzi uliojadili maswala ya matatizo na mazingira yaliyohusu Afrika Mashariki
(1810-1820). Uliandikwa na Sayyid Abdalah A. Nassir. Makala za semina ya
Kimataifa ya waandishi wa Kiswahili (uk. 148-150)
Muhula wa Utasa 1885-1945. Kipindi hiki ni kipindi
cha mabadiliko ya kiutawala na kielimu. Kubadilika kwa hati ya maandishi kutoka
Kiarabu kwenda Kirumi. Kipindi hiki maandishi machache yaliandikwa wakat huu,
mengi yakiwa maandishi ya Hemed Abdallah. Baadhi ya tenzi zilizopatikana ni
Utenzi wa Vita vya Majimaji. Kanuni za uandishi wa mashairi zilianza kupotea.
Makoloni ya Ulaya yalikuwa yakigawanwa Afrika (uk. 149-150)
Muhula wa Urasimi mpya (1945-1960) kipindi hiki kilikuwa
ndicho kipindi cha kufufua kanuni za utunzi. Shaaban Robert, Amri Abeid Khamis
Amani, M. Mnyampala, Ahmmed Nassir na wengineo. Kipindi hiki ndipo kitabu cha
sheria za kutunga mashairi kiliandikwa wakati ambao kilikuwa kinahitajika sana
ili kuweka kiungo kizuri na wakati uliopo. Yaani kueleweka vizuri katika wakati uliopo (1954)
Mtindo
uliotumika sana ni ule wa mizani 16 yaani 8+8 kwa kila kipande cha mshororo
katika mishororo minne . Mtindo uliotumika sana na Muyaka bin Haji katika karne
ya 18
Wanamapokeo
waliamini kuwa shairi liliandikwa ili liimbwe wakati huo mghani Radioni
Athumani Khalfani alikuwa amezoea kuimba mtindo huo na katika mahadhi ya aina
moja.
Muhula wa Usasa (1967-hadi leo) ni muhula wa
mtazamo mpya kimawazo kisanaa, hivyo kuna mgogoro katika uwanja wa ushairi.
Kipindi hiki washairi walikuwa wanatafuta uhuru wa kisanaa.
Mgogoro
juu ya kanuni uandishi wa ushairi uliongezeka zaidi.
Muainisho
huu wa mihula ya ushairi kwa mujibu wa Kezilahabi, unamapungufu yafuatayo
yaliyobainika;
Hujahusisha
usimulizi na usimulizi, inaaminiwaka kuwa asili ya ushairi wa kiswhili ni tungo
simulizi hasa nyimbo zinazofungamana na ngoma. Wataalam wanaounga mkono hoja
hii ni Chiraghdin (1971), Shariff (1988), Nassir (1977) na Ohly (1985).
Pia
haja zungumzia ushairi kabla ya karne ya 17. Kutokana na wataalam inaonekana
ushairi wa kiswahili ulianza kutungwa na kughanwa kwa ghibu/kuandikwa karne ya
10BK.
Hajabainisha
wazi muhula wa Utasa uko vipi? Kwa sababu bado washairi wengi walikuwepo kutoka
Tanga, Mombasa mfano; Shaabani Robert.
Kwa
mujibu wa Anord, R. (1973) mtaalam huyu ameainisha mihula ya ushairi katika
vipindi vitatu kama ifuatavyo;
Kipindi cha kabla ya Ukoloni: yeye alitumia mtazamo wa matabaka.
Ushairi uliokuwepo ni ule ulioakisi hali ya watu, mamwinyi na ufalme. mfano;
ushairi wa Mwanakupona ulisisitiza kuwatukuza mamwinyi na wafalme. Ushairi huu
wa Mwanakupona uliandikwa na Bi Mwanakupona binti Mshamu.
Muhula wa Upinzani: ni kipindi ambacho upinzani
ulijitokeza katika utetezi wa Uislam na mila za jadi dhidi ya Ukristo baada ya
vita vya majimaji. Kipindi hiki ushairi ulipo na hadi kilipofika kipindi cha
mwaka (1930). Kipindi hiki kiliwakilishwa na Shaaban Robert.
Kipindi cha baada ya Uhuru: hiki ni kipindi ambapo washairi
wengi walitunga mashairi kushughulikia
masuala ya ujenzi wa jamii mpya. Hii ni kutokana na mabadiliko ya fani
ya ushairi. Mfano; mashairi ya Mohammed S. Khatibu ya Fungate la Uhuru na
Wasakatonge yanasisitiza juu ya ujenzi wa jamii mpya.
Mapungufu ya Anord.R (1973) katika
uainishaji wa mihula ya ushairi wa kiswahili;
Hajaonesha
muda halisi kwani anaweka muda katika majumuisho. Mfano; anasema “Kipindi kabla
ya uhuru” kuanzia lini hadi lini, kipindi cha upinzani ni lini hadi lini na
kipindi baada ya uhuru kuanzia mwaka gani hadi mwaka gani na lini?
Hajahusisha
ushairi wa kiswahili na usimulizi kama ndicho chanzo (asili) ya ushairi wa
Kiswahili, kwani nyimbo zilizofungamana na ngoma.
Kwa
mujibu wa Ohly,R. (1973) mtalaam huyu amegawa mihula ya ushairi katika vipindi
vifuatavyo;
Kipindi
cha kabla ya mwaka 1888 kwa mujibu wa Ohly; anasema kipindi hiki kilibainisha
mashairi/ushairi wa aina tatu. Ushairi wa Kidini uliozungumzia masuala ya
kidini. Mfano; utenzi wa Hamziyya,
pamoja na ule wa Inkishafi. Ushairi wa kawaida ni ushairi ambao ulikuwa
haufungamani na upande wowote isipokuwa unatoa maadili ya dunia. Ushairi wa tungo
za Jadi ambazo zipo 13 baadhi ya hizi tungo za jadi ni shairi, utenzi, wimbo,
ukwafi, zivindo, kimai, Hamziyya, Inkishafi au Dura mandhuma.
Kipindi
cha 1888-1918;
mtalaam anaeleza kuwa katika kipindi hiki kumekuwapo na ushairi wa maelezo
usiofungamana na siasa. Ushairi wa kutathimini, ushairi wa kupinga ukoloni
mfano; Saadan Kandoro, Amri Abeid pamoja na Shaaban Robert. Mashairi ya
vikaragosi ambayo ni ya wale wenye hali ya chini/duni. Mfano; mashairi ya
Shaaban Robert, mashairi ya S. A. Kandoro.
Kipindi cha 1918-1949; Ohly anasema kuwa kipindi hiki
kilitawaliwa na fasihi ya ukoloni. Mikondo ya ushairi iliyokuwepo kipindi hiki
ni ushairi wa maadili, ushairi wa malimwengu, na tafsiri kama aliyoifanya
Nyerere J.K. (1968) katika ushairi wa kidrama wa kazi ya Shakespeare ambazo ni
kazi za mabepari wa Venis. Mfano wa ubeti;
Nerissa: Naam nitampa bure bila
ficha,
Poveeni na Jesika kutoka kwa myahudi,
Hati maalum ya hiba baada ya kifo chake,
Ataacha kwenu nyingi kila atakacho.
Mapungufu
ya uainishaji wa Ohly (1973) yanakumbwa na changamoto zifuatazo;
a. Hajatueleza uhusiano uliopo kati ya
ushairi simulizi na ushairi aliouainisha katika vipindi vyake.
b. hajaeleza baada ya muhula wa
1918-1949 mashairi yaliyoendelea mapaka leo yana maudhui gani
Baada
ya kuangalia wataalam hawa katika kuainisha vipindi vya ushairi tunabaini kuwa
mihula ya ushairi inaweza ikagawanywa kama ifuatavyo;
Muhula wa usahiri simulizi mpaka
1500. Muhula huu unatueleza kuwa asili
ya ushairi unaonyesha kuwa ni Ngoma na nyimbo ambazo zinafungamana na ngoma.
Mfano; utenzi / tungo za Fumo Liyongo.
Muhula wa Urasimu 1500-1890; kipindi hiki cha ushairi
kilitambulika kwa kuwepo kwa tungo za utenzi wa Tambuka 1728, Utenzi wa Hamziyya 1644 na utenzi wa Al-Inkishafi 1820. Hiki kipindi
ambacho kanuni za utunzi wa ushairi zilitumiwa kwa kiasi kikubwa. Kutokana na
sababu hiyo pia kipindi hiki kilipewa jina la kipindi cha Utasa hii ni kwa
mujibu wa Kezilahabi.
Muhula wa Mzinduko na Urasimi mpya
1946-1967 kutoka
kipindi cha utasa ufufuo wa kanuni na mwongezeko wa kazi za ushairi
zilionekana. Mfano; 1957 kitabu cha sheria
za kutunga mashairi cha Amri Abeid kilichapishwa. Washairi kama vile M. M.
Mlokozi na M. Mnyampala, Kandoro. S. Hivyo ikaonekana kazi za ushairi
zimezinduka.
Muhula wa Mageuzi na Majaribio
1968-hadi leo.
Kipindi hiki kinaonesha majaribio na migogoro mbalimbali juu ya kujadili kanuni
za kutunga mashairi (ushairi). Majaribio hayo yamefanya kuzuka kwa ushairi mpya
ujulikanao kama ushairi wa Mavue (masivina, huru, mlegezo) aina ya Bongo Flava,
ambapo kuna uimbaji na utendaji.
NADHARIA ZA FASIHI SIMULIZI YA
KIAFRIKA
Katika taaluma ya fasihi simulizi, suala la kuwa na
mitazamo tofautitofauti miongoni mwa wataalamu ni kitu cha kawaida tangu kale.
Fasihi simulizi kiulimwengu imekuwa ikitazamwa na kuchambuliwa kwa nadharia
kadhaa tangu zamani. Katika bara la Afrika kuna wataalamu wengi kutoka ndani na
nje ya bara hili waliotoa michango yao kadhaa katika kuichambua fasihi simulizi
ya kiafrika (hasa kipengele cha ngano). Kwa ujumla nadharia hizi zinaonekana
kujumuisha hata ngano za Kiswahili. Kwa hiyo hapa katika kuzijadili nadharia
hizo tutachukulia kuwa nadharia hizo baadhi kati yake zinaweza kutumika katika
kuchambua ngano za Kiswahili. Okpewho (1992:164-181) na pia Finnegan
(1970:315-334) wanajadili nadharia mbalimbali zinazolinda fasihi simulizi za
kiafrika hasa ngano kama ifuatavyo:
Mosi, nadharia ya ubadilikaji taratibu, (Evolutionism).
Nadharia hii iliasisiwa na mwanabiolojia wa Kiingereza Charles Darwin na baadaye kuungwa mkono na wananadharia wa
Kiingereza kama Edward Burnet Tylor,
James George Frazer na Andrew Lang. Pamoja na kwamba asili ya nadharia
hii ni mawazo ya kisayansi hasa biolojia, wanafasihi simulizi wanaitumia
wakidai kuwa masimulizi tunayoyasikia hivi leo ni ubadilikaji wa taratibu kwa
miaka mingi. Wataalamu hudai kuwa tafiti nyingi zinaonesha kuwa masimulizi
mengi ya kiafrika hasa ngano hufanana kwa kiasi fulani, hii ni uthibitisho kuwa
masimulizi haya yana asili moja kwa miaka mingi iliyopita. Inasemekana kuwa
usimulizi wa msingi wa ngano hizi ulikuwa mmoja lakini kutokana na ubadilikaji
taratibu kila jamii imekuwa ikiongeza vikorombwezo kadhaa katika masimulizi
kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Ili kuhahikikisha kuwa masimulizi haya
yanabaki imara, jamii zimekuwa zikiaminishwa kuwa masimulizi mengi ni ya kweli
lakini katika hali halisi, masimulizi haya hutokana na kuendelea kukarabati
masimulizi ya mwanzo.
Nadharia hii ina udhaifu katika kuamini kuwa fasihi
simulizi za kiafrika zinachukuliwa kuwa hazina mwenyewe, lakini ukweli ni
kwamba fasihi simulizi za kiafrika ni mali ya jamii nzima, japo si kweli kwamba
kila mtu katika jamii anaweza kuwa fanani kwa kiwango kile kile sawa na fanani
mwingine.
Nadharia ya msambao
au uenevu (Diffusionism).
Nadharia hii iliasisiwa na wataalamu kama Jacob na Wilhelm Grimm, baadaye mawazo yao yakaendelezwa na Max Muller. Mtaalamu mwingine ni Mmarekani Steve Thompson. Pamoja na
kuwepo tofauti ndogondogo za wataalamu wa nadharia hii, mawazo yao yanalenga
kueleza kuwa kuna kitovu cha fasihi simulizi dunia nzima. Kwa sababu ya jamii
kuingiliana kutokana na sababu mbambali, masimulizi haya yalianza kuhama kutoka
jamii moja hadi nyingine hasa kutoka kwenye jamii zilizostaarabika kimaisha
kwenda kwenye jamii ambazo hazijastaarabika. Waataalamu hawa walisema kwamba
kukitokea kufanana kati ya hadithi moja toka jamii mbili tofauti basi jamii
hizo zilipata kuwasiliana na kuathiriana kwa upande wa utamaduni. Hapa
wataalamu kama Jacob na Wilhelm walisema kuwa kama kuna kufanana kokote kwa
ngano za kiafrika na ulaya, basi ngano za kiafrika ni chipukizi toka kwa wazazi
wenye utamaduni wa India na Ulaya.
Tukichunguza ngano za Kiswahili kwa jicho la
nadharia hii, tunaweza kusema kuwa ngano nyingi zinaonekana kufanana kutoka
jamii mbalimbali za waswahili hivyo kuna uwezekano wa kuwepo kwa kitovu cha
usimulizi huu katika jamii fulani. Lakini nadharia hii ina upungufu mkubwa hasa
kwa kupuuza utu na utamaduni wa mwafrika, inapodai kuwa mwafrika alikopa ngano
kutoka kwa mzungu na mhindi inaelekea kusema kuwa mwafrika kabla ya kuwa na
mahusiano na watu hawa hakuwa na utamaduni suala ambalo ni la kibaguzi zaidi.
Nadharia
ya kisosholojia.
Nadharia hii iliasisiwa na Bronislaw Malinowski (1922, 1926) na
kuwa na wafuasi kama Edmund Leach, Raymond Firth, William Bascom
na kadhalika. Mtazamo wa nadharia hii ni kuwa ngano za kiafrika zipo na
kuibuka kwa sababu ya utumizi katika jamii. Watafiti hawa kama wanasosholojia,
waliamua kuchunguza vipera vya fasihi simulizi (na ngano zikiwemo) kwa upekee
wa kila jamii. Walichunguza mila na desturi kwa kuzingatia uamilifu wake katika
jamii. Wataalamu mbalimbali kwa kutumia nadharia hii waligundua kuwa ngano za
kiafrika zina majukumu muhimu katika jamii husika kwa mfano, Jan Vansina katika
kuzijadili simulizi za utawala wa Waganda aligundua kuwa simulizi hizo
zinaakisi utawala wa kurithi unaolinda umoja wa jamii ya Waganda. R.G. Willis katika kuchanganua ngano za
kihistoria za Wafipa wa Tanzania, anatumia ufafanuzi wa kiishara kugundua
mihimiri miwili ya kimaendeleo katika jamii. Adward Shorter (1969) alifanya utafiti kwa Wakimbu wa Tanzania
akagundua kuwa ngano za Wakimbu ni muhimu sana kwa kuhifadhi vipindi mbalimbali
vya kihistoria katika jamii husika.
Nadharia
hii katika ngano za Kiswahili tunaweza kusema kuwa maisha ya jamii za waswahili
ndiyo yanayozifanya ngano ziwepo kutokana na matumizi mbalimbali kijamii. Kazi za
ngano katika jamii za waswahili huwa mhimili wa kuwepo ngano hizo bila kupotea.
Nadharia
ya urasimi (formalism). Kwa
kiasi kikubwa nadharia hii ilikuja kupiku ile ya msambao au uenevu. Zote
zililenga kuvunjavunja ngano ili kuona vipengele vinavyoiunda. Wakati nadharia
ya msambao ikilenga kuivunjavunja ngano katika vipengele vyake na hatimaye
kuanza kutafuta mahali ilipoanzia na hatimaye kuunda ngano chanzi, nadharia ya
urasimi yenyewe iliona huu ni upotezaji wa muda na nguvu kwani yote haya
yaliishia kuleta utata kimgawanyo. Wanaurasimi wao waliona kuna haja ya
kuchunguza jinsi vipengele hivi vya ngano vimepangika kimfuatano katika kuiunda
ngano yenyewe kuliko kuanza kuhangaika kutafuta dhamira na hatimaye kusema
chimbuko la ngano. Mwaasisi wa nadharia hii ni mrusi aitwae Vladimir
Propp (1928) na baadae kufuatiwa na Eleazer Meletinsky, Marion Kilson
na Alan Dundes. Kwa kupanua mawazo ya Propp, Dundes (1971)
baada ya kuzichunguza ngano za Uganda hasa zile zinazohusisha wahusika wajanja
kama sungura na kobe, aligundua kuwa ngano hizi zina dhima tano. Mosi, zile za
urafiki zinazoonesha umoja na mshikamano katika kudumisha urafiki, pili zile za
mvutano unaolenga kupima urafiki. Tatu, zile ngano zinazoonesha kuharibu
urafiki. Hizi ni ngano zinazoonesha kundi moja la urafiki kuonesha hali ya
kuharibu uaminifu katika urafiki hasa kwa kuwadanganya wenzao. Nne, ngano
zinazoonesha ugunduzi yaani upande wa urafiki uliodanganywa hugundua ujanja na
uongo uliofanywa na kundi jingine katika kuharibu uaminifu. Tano, ni ngano
zinazoonesha mwisho wa urafiki. Ngano
hizi huonesha hatima ya kuvunjika kwa urafiki wa makundi na mara nyingi huishia
kutoa adhabu kwa mwanzilishi wa uhasama.
Nadharia
hii katika ngano za Kiswahili tunaweza kusema, inamaanisha kuzielewa ngano hizi
kwa kuchunguza jinsi ngano hizi zinavyoweza kuvunjwavunjwa katika vipengele
vyake na hivyo kubainisha muundo wake.
Nadharia
ya uhulutishi (hybridization). Nadharia hii ina wafuasi wengi wa
kiafrika kwa mfano Ngugi wa Thiong’o, Chinua Achebe, Frantz Fanon na
wengine. Mtazamo mkuu wa nadharia hii ni kuangalia namna ambavyo
nadharia zingine zinaweza kufaa na kushirikiana katika kuchunguza fasihi
simulizi za kiafrika. Hawa walilenga kuchunguza fasihi simulizi ya mwafrika kwa
kuangalia uzuri unaojitokeza katika kazi za waafrika wenyewe. M.M.Mulokozi ni
mfuasi wa nadhari hii kwa Tanzania. Mawazo ya wanauhulutishi yanajibainisha kwa
kutoa matamko kadhaa wanayoyatoa kuihusu fasihi simulizi ya mwafrika, kwa mfano
wanasema kuwa kuna haja ya kutojali mwonekano na uzuri wa nje wa fasihi na
kujali zaidi utendekaji ambao umejikita kwenye utendaji halisi wa msanii na
hadhira yake kifani na kimaudhui, utendekaji unatakiwa uwe na uwili
unaokamilishana yaani usielekee tu kwenye utamu bali uwe sanjali na hadhira na
mazingira yao, ni kosa kubwa kwa waafrika kuiga mambo bila kuchukua tahadhari
ya kujua kama wayaigayo yanawafaa katika jamii zao, pia fasihi simulizi si
sanaa ya kimapokeo isiyo na upya wowote bali inapaswa kutiwa ubunifu ulio hai.
MAREJEO
F.
E. M. K. Senkoro (1982) Fasihi.
Press and Publicity Centre. Dar es Salaam.
F.
Ruth (1970) Oral Literature in Africa.
Oxford: Clarendon Press
K. W.
Wamitila (2004) Kichocheo cha Fasihi,
Simulizi na Andishi. Focus Publications Limited: Nairobi
M.M.
Mulokozi (1989) Tanzu za fasihi simulizi.
Katika Mulika. Na 21
M. Msokile (
1993) Misingi ya Uhakiki wa Fasihi.
E.A.E.P. Nairobi
P.Mhando
na N.Balisidya (1976) Fasihi na sanaa za
maonyesho. T.P.H. Dar es Salaam
S. Okpewho (1992) African
Oral Literature. Backgrounds, Character, and Continuity. Indiana University
Press. U.S.A
MOTIFU YA SAFARI NA MSAKO NDIZO HUWA MWEGA MKUU WA DHAMIRA
KATIKA FASIHI YA WATOTO NA VIJANA. “MARIMBA
YA MAJALIWA”
Kwa
kujadili swali hili tutaanza kuelezea
maana ya fasihi, fasihi ya watoto, na maana ya motifu, na maaana ya dhamira.
Kisha katika kiini cha swali letu tutachambua motifu mbalimbali za safari na msako kama zilivyo jitokeza
katika kitabu. Baada ya hapo kuonyesha dhamira mbalimbali
Wataalamu
mbalimbali wameelezea maana ya fasihi. Mulokozi ( 1996:3) akimnukuu Egletoni
(1983:20-21), anasema fasihi ni sanaa ya lugha yenye ubunifu bilakujali kama
imeandikwa au laa.
Mulokozi
mwaka (1996), anasema ni sanaa ya lugha
inayoangalia maisha na mazingira halisi. Anaendelea kusema kuwa ni sanaa ya
lugha yenye ufundi wa hali ya juu ili kuweza kuwasilisha mawazo aliyonayo mtu
kwa njia inayoweza kuathiri kwa kutumia sanaa hiyo kimaandishi au kimazungumzo.
TUKI
(2004), wanasema mtoto ni mtu mwenye umri mdogo, katika maana hii hajatueleza
umri huo ni wa kuanzia miaka mingapi hadi miaka mingapi lakini kutokana
na maana hii Mulokozi (2008:338), anasema fasihi ya watoto na vijana ni ile
fasihi inayorejelea matini au kazi ambazo kimsingi hadhira yake ni watoto na
vijana, na hii ni kati ya umri wa miaka 0-10 na 11-17. Hivyo fasihi ya watoto
na vijana huhusisha kazi zinazowahusu bibadamu kati ya miaka 0-17. Na kazi hizo
zaweza kuwa riwaya, Hadithi fupi, Tamthilia au Ushahiri.
Motifu-
Ni dhana au jambo linalojirudiarudia katika kazi ya fasihi. Ambacho kinaweza
kuwa cha kifani au kinaudhui. Mfano wa motifu ni Motifu ya safari.
TUKI
(2004), dhamira ni kiini cha jambo au habari iliyosimuliwa ama kuandikwa hasa
katika fasihi
Madumulla
(2009), Dhamira ni wazo kuu katika kazi ya fasihi. Kwa ujumla wote
wanazungumzia jambo au wazo kuu katika
fasihi, Hivyo tunakubaliana na fasihi zote hapo juu. Marimba ya Majaliwa ni
hadithi iloyoandikwa na Edwini Semzaba mwaka (2008) ambayo inaelezea kuhusiana
na marimba ya Majaliwa iliyopotea. Mwandishi ameonyesha jinsi Majaliwa
alivyokuwa anatafuta marimba yake mpaka akaipata. Majaliwa alisafiri kwa
kutumia njia mbalimbali kama vile ungo, fagio, na maumbo ya samaki akizunguka
Tanzania nzima akisaka marimba ya nyuzi ishirini (20). Alianza Mafia, akaenda
Zanzibar, Tanga, Moshi na Arusha,Iringa, Mwanza, Kigoma, na miji mingine mingi.
Na Kongoti bingwa wa Taifa wa Malimba akimchenga kila mara huku akinga’nga’nia
Malimba ya Majaliwa ili amzuie kushinda na ashinde yeye na bila Marimba yenye
ishirini (20) hakuna ushindi.
Kuanzia
mwanzo hadi mwisho wa kitabu tunaona Majaliwa alisafiri sehemu mbalimbali hadi
kufikia kiwango cha kuzunguka nchi nzima huku akimsaka Kongoti ili aweze
kuilejesha Marimba yake. Safari ya Majaliwa ilianzia mafia mkoani pwani. Hii ni
baada ya kuchukuliwa Marimba yake na watu ambao awali hakuwafahamu na baadae
walikimbia kichakani (ukurasa wa 2). Kwa kuwa marimba nguvu zake ziliambatana
na nguvu ya kuzimu, usiku wa manane marehemu bibi yake mzaa mama alimjia
ndotoni na kumwambia majaliwa kuwa Kongoti Nachienga ndiye aliiba Marimba yake
kwa wasiwasi wa kushindwa wakifika Dodoma kwenye mashindano ya marimba ya
kitaifa. Katika upande wa kuzimu babu yake Majaliwa mzaa baba yake yupo upande
wa Kongoti (ukurasa 3)
Safari
ilianza rasmi usiku wa manane kisiwa cha mafia katika ufukwe wa kilindoni wa
Bahari ya Hindi. (ukurasa 5). Walisafiri huku bibi yake akiwa katika umbo la
samaki ( nguva na papa) (ukurasa 5) hadi Zanzibar ( ukurasa7-10). Akiwa huko
Majaliwa aliendelea kumsaka Kongoti bila mafanikio (ukurasa 11). Majaliwa
anaendelea na safari kuelekea Tanga. Wanatumia aina mbalimbali za usafiri kama Ungo, Ufagio, Chai maharage,
na basi mfano ukurasa (21,22 na 105). Majaliwa anakumbana na misukosuko
mbalimbali baharini hatimaye anafika Tanga, lakini juhudi zake hazimpi
mafanikio (sura ya 7-11). Majaliwa baada ya kusikia kwamba Kongoti alikuwa
anaelekea Kilimanjaro alianzisha safari ya kuelekea huko ili aweze kuitwaa
marimba yake sura ya (11-17) kwa usafari wa basi (ukurasa 46). Kutokana na
misukosuko mbalimbali Majaliwa anachelewa. Kilimanjaro alikuta mashindano
yamekwisha na Kongoti sasa anaelekea Arusha. Majaliwa nae ili kuisaka marimba
yake aliamua kumsaka Kongoti lakini pasipo na mafanikio yoyote.
Baadaye
Majaliwa alisafili kwenda Singida ( sura 26-27) baadaye Kondoa kwenda Tabora(
sura ya 27-30) Pia Tabora kwenda Shinyanga. Katika safari zote hizo Majaliwa
hakufanikiwa kutwaa marimba yake lakini hakukata tamaa aliendelea na safari ya
msako ukurasa 239.
Majaliwa
anaendelea na safari kutoka Shinyanga kwenda Mwanza baada ya kufika alishuka
kwenye ndege na kupanda daladala kuelekea Mwanza (ukurasa131) baada ya hapo
Majaliwa alisafiri kuelekea Butihama baadaye kurudi Mwanza kwa kujionea maeneo
mbalimbali ya kihistoria (ukurasa wa 138-140) Wakiwa katika usafiri wa meli
Majaliwa alivamiwa na Kongoti. Akapambana nae ili airejeshe marimba yake lakini
Marimba ile ilitumbikia ziwani (ukurasa 141) Bibi yake alipotokea akamwelezea
kisha akayafuatilia na kumwambia kuwa hayakuwa yenyewe. Wakatembelea sehemu
mbalimbali za kihistoria za Mwanza maeri ilifika Kemondo Bukoba kagera ambapo
palikuwa na mashindano pia na Kongoti angekuwa miongoni mwao alisafiri sehemu
mbalimbali za karagwe kwa basi kutokana na ulinzi mkali aliondoka kutembelea
sehemu mbalimbali za kihistoria (ukurasa 151)
Majaliwa
aliendelea na safari ya kuelekea Kigoma (ukurasa 155) ambapo alitembelea sehemu
mbalimbali za vivutio vya watalii baadaye mashindano yalifanyika hoteri ya Lake
Tanganyika ambapo alipata nafasi ya kufanya ufunguzi na hakupata pesa nyingi
hapo usiku walisafili kwa ungo kupitia Mbozi na milima ya mrengi baadaye Mbeya
ambapo mashindano yalifanyika Kileleni lodge ambapo alitumia njia mbalimbali na
kuipata marimba lakini haikuwa yenyewe (ukurasa 175) safari ya usiku ilikuwa ni
kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria kuamkia Iringa ambapo Kongoti
angatumbuiza kwenye maadhimisho ya shujaa Mkwawa (ukura wa 187) Baadaye Kidatu
Njombe, Rudewa hadi Manda. Baadae Mji wa Tunduma Mola tena Mwanjerwa alisikia
Kongoti bado anapiga marimba aliamini kuwa bado ana marimba yake (ukurasa 197)
Safari
ya Majaliwa huko Mbeya kwenda Songea kwa basi la Scandinavia (ukurasa 198)
Mashindano ya Ruvuma Lindi na Mtwara pia wakiwa Ruvuma walitembelea sehemu mbalimbali
za kihistoria (ukurasa 200-205), Baadaye Ndanda, Newala, Mtwara, Mnazi bay,
Lindi (Tengeru) (ukurasa 205) Baadaye ukumbi wa mkorosho mpya ambapo mashindano
yalifanyika lakini majaliwa hakupata nafasi ya kumsogelea Kongoti (ukurasa wa
208) kwa usafiri wa Ufagio walienda Rufiji hadi Mafia, Mkuranga,Dar es salaam,
Temeke,mwenge, Rugalo, Bagamoyo na sehemu mbalimbali za Dar es salaam (ukurasa
211).
Kutoka
Dar Es Salaam alifunga safari yake hadi Morogoro (ukurasa 212) kwa usafiri wa
basi baada ya kupita sehemu mbalimbali Majaliwa alifanikiwa kuikuta Marimba
Mjini Morogoro akiwa katika harakati za safari ya kuelekea katika shindano la
kitaifa huko Dodoma ilikuwa baada ya kubadilisha marimba katika sinia la
ukaguzi hapo tena Majaliwa alianza kujiandaa kusafiri kwa basi kwenda Dodoma
kwenye mashindano ya kitaifa pamoja na misukosuko ya kukatika kwa daraja
(ukurasa 230) Baadae aliingia Dodoma kwa kupitia Chamwino Dodoma Mjini baadaye
Milimani ambapo mashindano yalifanyika hoteli ya Milimani huko Dodoma na kuibuka
Mshindi wa kuwabwaga wenzake wote pamoja na adui yake Kongoti na kukamilisha
ndoto zake za kuwa bigwa wa Taifa.
Maana
ya ujasili Kwa mujibu wa TUK (2004), hali ya kukabili jambo hofu uhodari na
ushujaa. Ujasiri ni dhamira kuu katika kitabu hiki ambayo imejitokea katika
motifu zote na misako ambayo imeandikwa katika kitabu hiki majaliwa ameonesha
kuwa jasiri kuanzia mwanzo wa hadithi pale anapoanza kutafuta marimba yake
iliyoibwa akisaidiwa na bibi yake. Hili limeonekana katika sehemu mbalimbali
mfano:- katika ukurasa wa 72 sura ya 17 ambapo majaliwa anapambana na dereva
taski baada ya kutaka kumwibia majaliwa pesa zake wakati wakimtafuta kongoti
aliyekuwa kwenye pikipiki.
“Majaliwa akiwa ameshika jiwe lake
la rubi alimpiga nalo Yule dereva kwenye macho yake yote mawili mara mbili”
Mfano
mwingine ni pale majaliwa alipopambana na kongoti mlenzi wakinyang’anyana
marimba majaliwa alikuwa mtoto mdogo lakini aliweza kukabiliana na kongoti
ambaye alikuwa mtu mzima. Hili limeoneshwa katika ukurasa wa 141 sura ya 34.
“
Nalianza kukamatana na kuangushana na
ingawa alikuwa mtoto tu, uchungu wa kudhulumiwa marimba yake ulimjaza ari na
akachuana kishujaa”
Hivyo
basi kwa kuangalia hiyo mifano tunaona majaliwa alikuwa jasiri na mwandishi
alionesha hili kama dhamila kuu
Dhamira
nyingine ni Imani za kishirikina. Imani kwa mujibu wa Kamusi TUKI (2004), ni
mambo anayoyakubali mtu kuwa ni ya kweli na anayopaswa kuheshimu, haswa katika
dini, au itikadi. Ushikirina ni tabia ya kuamini mambo ya uchawi, mizimu, nk.
Katika kitabu hiki dhamira ya imana ya kishirikina imejijenga sana katika
motifu ya safari na msako iliyojitokeza katika kitabu hiki mfano katika kitabu
hiki mwandishi alionyesha hili pale majaliwa alipokuwa anasafiri kwa njia ya
kishirikina kama vile ungo, fagio, pia kuna wakati mwingine alikuwa anasafiri
kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa kufumba macho na kufumbua. Mfano
mwingine ni ule kusafiri kwa ungo imeoneshwa (ukurasa wa 52), Bibi alimwambia
Majaliwa apande kwenye Ungo.
“ Bibi alimwambia mjukuu wake sasa
na wewe panda kwenye ungo”
.
Pia kusafiri kwa ufagio ( ukurasa wa 105)
Majaliwa alimletea bibi fagio uliokuwa umeachwa kwenye takataka.
“ Haya
panda nyuma”
Kufumba
na kufumbua wakajikuta wako angani.
Dhamira
nyingi ni Rushwa. Rushwa ni fedha au kitu cha dhamani kinachotolewa na kupewa
mtu mwenye madaraka ya kitu fulani ili mpaji apatiwe upendeleo. Katika kitabu
hiki rushwa ilijitokeza pale ambapo Majaliwa alimpa fedha kwa sababu hakuwa na
kibali cha kuingia sehemu za utalii ili aweze kumwachia. Hili limeoneshwa
ukrusa wa 66
“ Majaliwa alipoangalia saa
iliyotundikwa ukutani na kuona ni saa tano, alibadilisha uamuzi wake na
kuongeza dola moja, hapo askari hakusema kitu”.
Hilo
pia limeoneshwa katika ukurasa wa 213 sura ya 54.
Tamaa
ni hamu kubwa ya kupata kitu au shauku au matarajio ya kupata kitu. Hili
mwandishi pia amelibainisha kwa kuanza na Majaliwa ambaye yeye alikuwa na tamaa ya kupata marimba yake
iliyochukuliwa na kongoti kiasi cha kuamua kujitosa na kuanza kutafuta kwa
kupitia hali mbalimbali ingawa alikuwa
ni mtoto. Tamaa pia imeoneshwa pale ambapo dereva teksi alitamani dora za
Majaliwa alipokuwa anamwendesha mpaka akapata upofu kwa kupigwa na Majaliwa.
Pia bibi alihadithia hadithi moja ambayo ilikuwa inaonyesha jinsi ambavyo tamaa
ni mbaya ukurasa wa 123-126.
“ Bibi akamuuliza Majaliwa hadithi
inakufundisha nini? Majaliwa anajibu Tamaa ni mbaya”. Katika ukurasa wa 72 dereva teksi
aliona pesa za majaliwa na kuzitamani hivyo akampeleka porini. Dereva
anamwabia,” toa pesa zote ulizonazo haraka”
Madhara
ya kutokuwa mtiifu .Hili pia mwandishi amelionesha katika kitabu chake pale
ambapo majaliwa alikuwa anakiuka maagizo ambayo alikuwa anapewa na bibi yake na kupata madhara. Hili
mwandishi amelionesha katika ukurasa wa 50 ambapo bibi anamwambia majaliwa.
“siku
zote utii ni bora”. ‘Si nilikukataza kula kitu chochote kupitia kinywani’
.Hapo
ndipo Majaliwa akakumbuka alikula mayai kwenye tumbo la nyangumi. Bibi akasema
“ hilo ndilo kosa ndio maana Rubi
haikufanya kazi yake name nikakupa adhabu ya kuwa peke yako usiku wote wa jana.”
Pia
Bibi alimwadithia Majaliwa Hadithi ya madhara ya kutokuwa mtiifu katika ukurasa
wa 169-171 ambayo lkimuelezea mvuvi ambaye alikosa utiifu na mwishowe akakosa
utajiri kwa ajili hiyo.
Dhamra
nyingineyo ni ile ya umuhimu wa kujua historia mbalimbali ya maeneo katika
nchi. Hili mwandishi amelionesha wazi kwani limeoneshwa na kujengwa dhamira na
motifu ya safari kwani katika safari ambazo Majaliwa alizifanya ndipo hapo
aliweza kujua historia za sehemu mbalimbali alizosimuliwa na bibi yake. Kwa
ujumla kulikuwa na hisoria ya mapango ya Amboni Tanga, Kondoa Iringa, mji wa Tabora, hisotria ya ngome kongwe,
Kaburi la Abeid Amani Karume, Wangoni. Makaburi ya watu waliokufa kwa ajili ya
Treni, Meli iliyozama ya MV Bukoba na sehemu nyinginezo.
Pamoja
na kuwepo na dhamira hizo hapo juu zilizoelezwa kwa mapana na marefu kulikuwepo
pia dhamira nyinginezo ambazo zilizokuwepo katika kitabu hiki. Dhamira hizo ni
pamoja na wizi, wivu, mashindano, kujikinga na ukimwi, chuki, nafasi ya
mwanamke katika jamii, Ukombozi, Elimu, Ukatili, Umoja na mshikamano na hali
ngumu ya maisha. Hivyo kwa ujumla tunaweza kusema kuwa mwandishi amefanikiwa
kwa kiasi kikubwa kujadili masuala mbalimbali yaliyoko katika jamii hasa jamii
yetu ya Kitanzania.
MAREJEO:
Madumulla,
S. (2009), Riwaya yaKiswahili: Mature
Educational Publishers Lited.
Mulokozi,
M. M. (1996), Utangulizi wa Fasihi ya
Kiswahili: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Dar Es
Salaam.
Semzaba,
E. (2008), Marimba ya Majaliwa.
E&D Publishers Limited:Dar Es Salaam.
TUKI
(2OO4), Kamusi ya Kiswahili Sanifu.
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili: Dar Es Salaam.
KWA KIASI KIKUBWA FASIHI HUTAWALIWA NA FANTASIA ILI
KUNOGESHA
USOMAJI. MAELEZO KWA KUTUMIA KITABU CHA MARIMBA YA MAJALIWA
Fasihi
inafafanuliwa na Wamitila (2003) kwa kueleza kuwa ni kazi ya sanaa inayotumia
lugha kwa usanii na inayowasilisha suala fulani pamoja kwa njia inayoathiri,
kugusana kuacha athari fulani na kuonyesha ubunilizi na ubunifu fulani na
zinazomhusu binadamu. Kazi hizi za fasihi huweza kuwasilishwa kwa njia ya mdomo
yaani fasihi simulizi au kwa njia ya maandishi yaani fasihi andishi. Kwa kifupi
tunaweza kusema kuwa fasihi ni tawi la kisanaa litumialo lugha kama nyenzo kuu
ili kufikisha ujumbe katika jamii lengwa.
Pia
Wamitila (2003) anaeleza kuwa fasihi ya watoto kuwa hutumiwa kuelezea fasihi
maalumu inayoandikwa kwa ajili ya watoto.Hii ni fasihi ambayo ni tofauti na
ngano na hurafa.Mifano ya kazi za watoto ni kama vile Ngome ya Mianzi ya M.Mulokozi, Yatima na Zimwi
la leo ya Wamitila na Mwendo
ya Lema.
Wamitila
(kaishatajwa) anaeleza kuwa fantasia ni sawa na njozi, njozi ni dhana
inayotumiwa kuelezea kazi ya fasihi ambayo ina sifa ambazo zinakiuka
uhalisi.Anaendelea kufafanua kuwa ni kazi yenye sifa za kindotondoto au kutaka
kuamilisha hali isiyo ya kawaida. Njozi hupatikana sana katika maandishi
yanayolenga hadhira ya watoto.Sifa za kinjozi huweza kupatikana katika fasihi
inayohusishwa na matapo mbalimbali ya kifasihi.Hutumiwa kueleza kazi za kinathari
ambazo huwa na mandhari ya ajabu, matukio magumu kukubalika katika hali ya
kawaida na hata wahusika wasioweza kupatikana katika uhalisi. Kutokana na
fasili hiyo ya Wamitila tunaweza kusema kuwa wahusika katika kazi zenye
fantasia ni wahusika kama vile mazimwi, mashetani ,majini na vitu vingine
ambavyo havidhaniwi kuwepo katika jamii, yaani haviwezi kupatikana katika
uhalisia .
Ifuatayo
ni historia fupi ya kitabu cha Marimba ya Majaliwa.
Marimba
ya Majaliwa
ni kitabu kilichoandikwa na Edwin
Semzaba (2008), kinachoelezea harakati za kutafuta marimba ya Majaliwa
yenye nyuzi ishirini, iliyoporwa na Ngongoti aliyekuwa bingwa wa kupiga
marimba.Kitabu hiki kinahusisha msako wa marimba hiyo katika mikoa mbalimbali
ya Tanzania, na hatimaye Majaliwa alifanikiwa kupata marimba yake na
kushiririki katika mashindano ya kumtafuta bingwa wa kupiga marimba huko Dodoma
ambapo Majaliwa aliibuka mshindi wa shindano hilo.
Ufuatao
ni uchambuzi wa baadhi ya fantasia
zilizojitokeza katikakazi ya fasihi kama katia kitabu cha Marimba ya
Majaliwa. Katika uchambuzi wa fantasia, tumejaribu kuziweka fantasia katika
makundi tofauti tofauti.Makundi hayo ni kama vile fantasia zinazohusu usafiri,
fantasia zinazohusu utokeaji tofauti tofauti wa bibi pamoja na umbo
lake,fantasia zinazohusu jiwe la rubi, fantasia zinazohusu utokeaji wa babu na
nyinginezo.Kwa kuanza na fantasia zinazohusu usafiri:-
Mwandishi
Semzaba ameonyesha njia mbalimbali alizokuwa akizitumia Majaliwa na bibi
kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine ambazo hazikuwa za kawaida katika
maisha halisi ya binadamu.Njia hizo za ajabu alizokuwa akizitumia ni pamoja na
:-
Kutumia ufagio, mfano (uk.27) alitumia ufagio
kueleka uwanja wa kimataifa wa mifagio, (uk.103) alitumia ufagio kwenda mapango
ya Amboni,(uk. 208) alitua uwanja wa Kigamboni kwa ufagio.
Kutumia ungo, Bibi pamoja na Wajaliwa walitumia
ungo kwenda sehemu tofautitofauti kama inavyodhihirika katika (uk.77) kutoka
Tanga kuelekea Kilimanjaro.
Kutumia njia ya kufumba na kufumbua.Katika njia hii, bibi alikuwa akiwambia
Majaliwa afumbe macho akifumbua wanakuwa wamefika sehemu au eneo lingine.Aina
hii ya usafiri inadhihirika katika (uk 77,107,107 na 209). Mfano (uk 107) bibi
alimwambia majaliwa afumbe macho baada ya Majaliwa kufumbua macho akajikuta
yumo ndani ya pango la Amboni.
Pia msanii ameonyesha jinsi bibi
Majaliwa alivyokuwa akipaa hewani kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Mfano uk. (182)…. alimwacha sehemu ya Mwandege
halafu akapaa.Hivyo usafiri aliokuwa akitumia bibi na Majaliwa kwa hali ya
kawaida katika jamii ni mambo ya kinjozi yaani hayapo katika maisha ya
kiuhalisia na wala hayatarajiwi kuwepo.
Kundi
lingine la fantasia ni namna ya utokeaji na uondokaji wa bibi
pamoja na umbo lake
Msanii
ameonesha hali isiyokuwa ya kawaida katika maisha ya binadamu kwa kumtumia
mhusika ambaye ni bibi yake Majaliwa na kufanikiwa kuonyesha hali hiyo ya
kinjozi.
Utokeaji
wa bibi pamoja na umbo lake unadhihirika kama ifuatavyo:-
Katika
uk. (5-7) tunaona bibi anajitokeza katika umbo
la samaki na kumbeba Majaliwa na kuondoka naye hadi Unguja kusini.Bibi yake
Majaliwa alijitokeza kama papa na kubadilika na kuwa nguva .Hili si jambo la
kawaida kwa binadamu kubadilika badilika bali ni mambo ya kinjozi tu.
Katika
uk. (143) mwandishi ameonesha jinsi bibi
alivyogeuka na kuwa tai mkubwa na kuruka, hali hii pia sio hali ya
kawaida kwa binadamu bali ni dhana ya ufantasia aliyoitumia msaniii ili
kukamilisha lengo lake.
Pia
mwandishi amefanikiwa kuonesha matukio mbalimbali ya kifantasia aliyokuwa
akifanya bibi yake Majaliwa na Majaliwa. Mfano
nyoka kutoka mdomoni kwa mtu uk. (58) msanii anasema, “Bibi alipanua
mdomo na kutoa nyoka ambao waliwameza wale vibwanga wote”.
Kumvisha Majaliwa nguo uk. (58) bibi alichukua kijani
akakichomeka kichwani kwa Majaliwa na Majaliwa akajiona amevaa koti,suruali na
viatu vya baridi.
Kuna ufantasia unaojitokeza katika
hadithi ambazo bibi alikuwa akimsimulia Majaliwa mfano uk. (169) Bibi anamsimulia Majaliwa hadithi ya
mvuvi aliyevua chupa, na ndani ya chupa akatoka ndege mkubwa na kuanza kuongea.
Pia michezo ya wanyama wakali, imeoneshwa na msanii katika uk.(78
na 79) ambapo ameonesha jinsi Majaliwa na bibi yake walivyokuwa wakicheza na
wanyama wakali kama vile simba na tembo huko mbugani Arusha .Dhana hii ni ya
kifantasia kwani haiwezekani kabisa katika hali halisi kwa wanyama wakali
kucheza na binadamu.
Kwa
upande mwingine msanii ameonesha dhana ya ufantasia pale ambapo walikuwa
wakiingia katika sehemu tofauti tofauti kama vile hotelini mfano waliingia
hoteli ya ngurudoto huko Arusha uk.(80), na hoteli ya Seventy seven uk.(88)
Hivyo
mwandishi ametuonesha hali zisizokuwa za kawaida katika maisha halisi ya
binadamu kama vile kubadilika badilika
kutoka binadamu na kuwa samaki,bibi kuja kwa umbo la mama yake Majaliwa, bibi
kuja kwa umbo la binti mdogo na vitu vinginevyo
kama ndege sio jambo la kawaida katika maisha ya kila siku ya binadamu.
Kundi
lingine la fantasia lililooneshwa na msanii katika kitabu hiki ni uwepo wa jiwe
la rubi, hili ni jiwe ambalo Majaliwa alipewa na bibi yake kwa
masharti. Jiwe hili lilimsaidia Majaliwa
kula chakula katika sehemu mbalimbali
alizokuwa akisafiri akitafuta marimba yake ingawa jiwe hili lilikuwa na
masharti.Masharti aliyopewa Majaliwa ni kutokula kitu kwa kupitia
mdomo.Mwandishi ameonesha jinsi Majaliwa alivyotumia jiwe hilo, hata alipokiuka
masharti bibi yake alimpa tena jiwe kama lile.Uwepo wa jiwe hili unadhihirika
katika kurasa kama vile (21,102,110,143).Majaliwa alitumia jiwe hili kwa kula
pale tu alipotamka maneno kadhaa na akujikuta tayari ameshiba bila kutumia mdomo
na kinywa.
Kundi
linguine la mambo ya ajabu ajabu ni nmna ya utokeaji wa babu.Mwandishi
ameonesha kuwa mpinzani wa Majalia, Ngongoti alikuwa akipata nguvu za kusafiri
kwenda mbali pamoja na kumtoroka Majaliwa kwa kutumia nguvu za kimiujiza
alizokuwa akisaidiwa na babu.Nguvu za babu zilikuwa kipingamizi kilichomfanya
Majaliwa kushindwa kufanikisha haraka zoezi la kupata Marimba yake.Msanii
ameonesha jinsi babu alivyokuwa akijitokeza na kutuma vikwazo kama vile:-
Vibwengo uk.(53). Mwandishi anaeleza, Majaliwa
aliona kundi kubwa la vibwengo likwaajia kutoka kushoto, kulia na mbele yao.Pia
uk. (27,58 ,93 na194) unaonesha jinsi babu alivyotuma vibwengo kumkabili bibi
na Majaliwa.
Pia
babu alimtokea Majaliwa katika umbo la
Mamba akiwa na nia ya kumuangamiza lakini bibi alimsaidia, haya
yanajitokeza katika uk.wa (49). Zote hivi ni fantasia kwani si hali ya kawaida
kwa vitu kama hivi kujitokeza kwa umbo la binadamu na binadamu kujibadilisha na
kujitokeza katika hali tofautitofauti katika maisha halisi ya binadamu.
Fantasia
nyingine alizozionesha msanii ni kama vile, Majaliwa alipofika Ukerewe aliona mawe mawili
makubwa juu ya mlima ambapo jiwe moja la juu lilikuwa linazungukazunguka.
uk.(146).Hali hii katika mazingira ya kawaida si halisi na wala hatutegemei
kuona jiwe likizunguka lenyewe bila mtu kuligusa.
Baada
ya kupitia baadhi ya fantasia katika kitabu ch Marimba ya Majaliwa ,
ufuatao ni mchango wa fantasia katika
kazi hiyo;
Kujenga dhamira : Msanii ametumia dhana ya fantasia
kama vile uwepo wa jiwe la rubi kujenga dhamira tofauti tofauti kama vile
kuwafanya watoto wawe na adabu na utii, kuwafanya watoto wafikiri zaidi
mazingira ya uwezekano katika jamii . Vilevle fantasia za utokeaji wa babu huwafanya watoto wawe na woga juu ya mambo
mbalimbali na wawe na mawazo juu ya tamaduni mbalimbali za watu wa kale.
Kujega taharuki: hapa fantasia hujenga shauku kwa
watoto au msomaji kutaka kujua nini kitaendelea baada ya kukutana na kikwazo
fulani.Mfano fantasia ya kuingia hoteli ya Ngurudoto na hoteli ya Seventy seven
kimiujiza inajenga taharuki ya kutaka kujua kwamba, je baada ya kupambazuka
Majaliwa atashikwa au la.Pia hali ya utokeaji wa babu kama mamba pale mtoni
alipokuwa akinawa majaliwa,msomaji hupata taharuki ya kutaka kujua kama
Majaliwa atamezwa na yule mamba au la.Fantasia ya kupaa kwa ungo na kutua juu
ya mlima Kilimanjaro, msomaji hupata taharuki ya kutaka kujua kuwa Majaliwa
atasalimika kwenye barafu au la.
Pia
kutua na kucheza na wanyama wakali mbugani, huzua shauku kwa msomaji ya kutaka
kujua wataliwa na wanyama hao au la na watasalimikaje na wanyama hao.
Fantasia
humjengea mtoto au msomaji taswira tofauti tofauti juu ya mambo yasiyokuwa ya
kawaida. Mfano fantasia ya utokeaji wa bibi katika sura tofautitofauti,utokeaji
wa babu,uwepo wa jiwe la rubi na usafiri uliotumika hujenga taswira ya
mambo kama hayo kutokea katika jamii. .Mtoto hujenga taswira juu ya uwepo wa
vitu kama hivyo katika maisha ya kila siku ya jamii.
Fantasia huamilisha uwepo wa mambo
fulani fulani katika jamii ili kutaka kuthibitisha mambo hayo. Mfano fantasia za utokeaji wa bibi na babu na upinzani kati
yao, hutaka kuamilisha kuwa suala la ugomvi kati ya watu waliokufa yanaweza
kuwapata watoto au watu wao wa karibu waliobaki duniani kwa namna tofauti
tofauti za ajabu. Hivyo tunaweza kupata funzo kuwa ugomvi si kitu chema katika
jamii.
Fantasia huibua migogoro : msanii ametumia dhana hii ya
fantasia katika kitabu hiki ili kuibua na kukuza migogoro.Hali hii ya kukuza
migogoro au kisa ni namna ambayo mtunzi hutumia ili kukifanya kisa chake kiwe
na mawanda mapana.Mfano fantasia za upinzani wa babu dhidi ya bibi kwa maumbo
tofauti kama vile umbo la vibwengo na umbo la mamba, hali hii imekuza kisa cha
msanii na kuwa na mawanda mapana kwani humlazimu msanii kubuni zaidi namna ya
kumuepusha muhusika wake asiangamie.Pia fantasia ya usafiri kama vile kutumia
ungo,ufagio na nyinginezo, msanii amezitumia ili kujenga na kukuza migogoro
katika kazi yake ili uwe na mawanda mapana zaidi.
Fantasia hufanikisha msuko wa
vitushi,mfano
msanii ameweza kuhusianisha fantasia
kama vile usafiri wa kutumia njia mbalimbali na hadithi mbalimbali alizokuwa
akimsimulia Majaliwa na inaonesha wazi kuwa kutokana na kutumia fantasia
kumemsaidia kukamilisha msuko wa vitushi kama vile alivyomsimulia majaliwa
hadithi tofati wakiwa safarini. Mfano wakiwa juu ya mlima Kilimanjaro.
Pia
fantasia huburudisha, husisimua na kutia
watoto hamasa.Mwandishi amefanikiwa kuonesha fantasia tofauti tofauti za
kusisimua na kutia hamasa kama vile bibi alivyokuwa akimtokea Majaliwa, bibi na
Majaliwa kucheza na wanyama na nyinginezo. Hali hii huburudisha na kumsisimua
mtu aisomapo.Pia wasomaji huburudika kutokana na matukio ya ajabu ajabu
yaliyojitikeza na namna yanavyoendelezwa
na msanii.
Hivyo
tunaweza kuhitimisha kuwa mwandishi wa kitabu cha Marimba ya Majaliwa,
amefanikiwa kuonesha jinsi fantasia zinavyojitokeza katika fasihi.Msanii
ameonesha fantasia hizo zilivyotumika katika usakaji au utafutaji wa Marimba
katika sehemu mbalimbali nchini Tanzania.Utokeaji wa fantasia katika kazi ya
fasihi huwa ni ubunifu wa mtunzi kwa lengo la kuifanya hadhira anayoiandikia,
mathalani ya watoto ihamaki na kufikiri
zaidi sababu za uwezekano wa mambo kama hayo katika jamii.
MAREJEO
Semzaba, E. (2008), Marimba ya Majaliwa.
E&D Publishers Limited:Dar es Salaam
Wamitila,
K. W. (2003) Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia,Nairobi :English
Press
MAANA YA RIWAYA NA AINA ZA RIWAYA
Katika
kuandika makala hii hili, sehemu ya kwanza tutaangalia maana ya riwaya kwa
mujibu wa wataalamu, historia ya riwaya kwa ufupi na sifa za zake. Sehemu ya
pili tutaangalia kiini cha swali yaani aina za riwaya kwa mujibu wa wataalamu
wa fasihi. Sehemu ya tatu tutaangalia hitimisho na kumalizia na marejeo.
Riwaya
imefasiliwa na wataalamu mbalimbali miongoni mwao ni kama vile,
Encyclopedia Americana (EA), Jz. 20 (1982:510f)
wakinukuliwa na Mulokozi (1996) wanasema, riwaya kuwa ni hadithi ya kubuni
inayotosha kuwa kitabu. Maelezo haya yanaibua utata kwani hayafafanui kitabu
kinapaswa kuwa na urefu kiasi gani. Matharani kwa mujibu wa UNESCO katika
Mulokozi (1996) kitabu ni chapisho lolote lenye kurasa 48 au zaidi. Ama urefu
wa kitabu hautegemei idadi ya kurasa tu pia unategemea ukubwa wa kurasa (upana
na kina) ukubwa wa maandishi na mpangilio wake.
Encyclopedia
Britanica EB, Jz.8, (1985:810) wakinukuliwa na Mulokozi (1996) wanaeleza kuwa,
riwaya ni masimulizi marefu ya kinathari yaliyochangamana kiasi, yenye
kuzungumzia tajriba ya maisha ya binadamu kwa ubunifu. Udhaifu wa hoja hii ni
kwamba wamejikita katika kigezo cha urefu, lakini hatujui urefu huo ni wapaswa
kuwa kiasi gani. Lakini Mphahelele (1976:45) akinukuliwa na Mulokozi (1996) anaeleza kuwa riwaya fupi
huwa na maneno kati ya (35,000 hadi 50,000) na riwaya ndefu huwa na maneno kati
ya (50,000 hadi 75,000).
Pamoja
namaelezo hayo ya Mphahelele (1976) imeonekana bado kuna utata katika kigezo
cha urefu. Hivyo Wamitila (2002) Senkoro
(2011) na hawakubaliani na kigezo cha
kufasili riwaya kwa kutumia kigezo cha urefu. Mfano Senkoro anaeleza kuwa ,
“Ikiwa tutakichukua kipimo cha jumla ya
maneno (75,000)
kuwa kielelezo
cha riwaya basi itaonekana kuwa tuna
riwaya chache
mno katika fasihi kwa hali hii
nadhani sifa ya
mchangamano ni nzuri zaidi kuelezea
maana ya
riwaya” (uk. 56)
Naye
Wamitila anendelea kuelezea kuhusiana na suala urefu kuwa,
“Kigezo hiki cha urefu hakifai
tunapoziangalia kazi
za
fasihi ya Kiswahili...Mfano kazi mbili za E. Kezilahabi,
“Nagona
naMizingile” hazina idadi kubwa ya maneno lakini
ni riwaya”.
Hivyo,
Wamitila (2002) na Senkoro (2011) wanaelekeana kufanana katika kufasili maana
ya riwaya ambapo wanaeleza kuwa, riwaya ni kisa mchangamano ambacho huweza
kuchambuliwa kupimwa kwa mapana na marefu kifani na kimaudhui. Riwaya ni kisa
au mkusanyiko wa visa, nyenye urefu unaoviruhusu vitambe na kutambaa mahali
pengi na kuambaa vizingiti vingi vya maisha kama apendavyo mwandishi wake.
Riwaya basi ni hadithi ndefu ya kubuni, yenye visa vingi, wahusika zaidi ya mmoja,
na yenye mazungumzo na maelezo yanayozingatia kwa undani na upana, maisha ya
jamii. Riwaya hutoa picha ya jumla ya maisha ya mtu toka nyumbani hadi katika
kiwango cha taifa na dunia nzima. Senkoro (2011).
Hivyo
kutokana na fasili za wataalamu hawa tunaweza kufasili riwaya kuwa ni
masimulizi ya kubuni ya kinathari yenye msuko au mpangilio fulani wa matukio au
ploti inayofungamana na wakati au kusawili wakati na yenye visa vingi
vivavyotendeka katika wakati fulani na yenye mawanda mapana yenye mchangamano wa
dhamira, visa na wahusika.
Baada
ya kutoa fasili mbalimbali za wataalamu wa fasihi kuhusu maana ya riwaya, sasa
tuangalie kwa ufupi chimbuko la riwaya;
Riwaya
ilizuka kutokana na maendeleo ya mageuzi ya kiutamaduni. Suala la ukoloni na uvumbuzi pia liliumba hali ambazo
zilihitaji kuelezwa kwa mawanda zaidi ya
yale ya ngano na hatithi fupi. Hapo hapo kuzuka kwa miji na viwanda
pamoja na maendeleo ya wasomaji yalifanya riwaya nyingi ziandikwe. Uchangamano
wa maisha ya jamii kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni wenyewe ulizusha haja ya kuwa na utanzu wa
fasihi ulio na uchangamano kifani na kimaudhui. Kupanuka kwa usomaji, hasa
wakati wa mapinduzi ya viwanda huko Ulaya, kuliwafanya waandishi waandike
waandiko marefu kwani sasa walikuwapo wasomaji hasa wanawake waliobaki
majumbani wakati waume zao walipokwenda viwandani, wasomaji ambao muda wao
uliwaruhusu kusoma maandiko marefu marefu ijapokuwa hii lilikuwa jambo la
baadaye sana wakati wa kina Charles Dickens. Hii historia fupi ya chimbuko. Senkoro (2011:55)
Baada
ya kuangalia historia fupi ya chimbuko la riwaya ni vyema tukaangalia nduni
bainifu za riwaya kwa kuziainisha katika aya moja. Kwa mujibu wa Wamitila (2002) sifa
hizo ni kama zifuatazo;
Uwazi
na uangavu, kazi husika ya fasihi isiwasumbue na kuwatatiza wasomaji kuzielewa,
muwala na muumano, kazi ya riwaya lazima iwe na mshikamano au mtiririko mzuri
wa visa au matukio kuijenga kazi ya kifasihi, uchangamano wa visa yaani kutokea
kisa zaidi kimoja, wingi wa maana kuhusiana na sifa ya uchangamano na ukamilifu
ni kule kuwako kwa elemeti zote muhumiu na za kimsingi katika kazi ya fasihi.
Baada
ya kuangakulia sifa au nduni bainifu za riwaya tuangalie aina za riwaya kwa
mujibu wa watalamu mbalimbali;
Katika
uainishaji wa aina za riwaya, wataalamu wametumia vigezo mbalimbali vya
uainishaji kama vile msingi wa kidhamira ambao kwa kiasi kikumbwa sifa za
kimaudhui, kifani, kihistoria na kiitikadi. Katika uainishaji wa aina za riwaya
kwa kutumia vigezo hivyo wataalamu wamefanana kuainisha baadhi ya aina za
riwaya. Mfano Mulokozi (1996), Wamitila (2003) na Madumulla (2009) aina walizofanana kuainisha ni kama
zifuatazo;
Riwaya
saikolojia
ni aina ya riwaya inayododosa nafsi ya
mhusika, fikra, hisia mawazo, imani, hofu, mashaka, matumaini na athari ya
mambo hayo kwake binafsi na labda
kwa jamii mfano “Kichwa Maji” ya E.Kezilahabi, “Kipimo cha Mianzi” ya Feud na
“Kiu” ya M.S. Mohammed.
Riwaya
ya kisosholojia au jamii ni riwaya ambayo inasawiri maisha ya kawaida ya jamii kwa
kuchunguza matatizo yake, yawe kifamilia kitabaka, kiuchumi, kisiasa au hata
kiutamaduni mfano “Titi la Mkwe” ya A.
Banzi, “Kurwa na Doto” ya M.S. Farsi na “Rosa Mistika” ya E. Kezilahabi.
Riwaya historia ni aina ya riwaya ambayo msingi
wake kuhusu matukio fulani katika jamii ya mwandishi, tukio hili huwa ni kubwa na la muhimu kijamii,
laweza kuwa la kikabila au la
kitaifa mfano “Uhuru wa Watumwa”
ya J. Mbotela, “Miradi Bubu ya Wazalendo” ya Luhumbika na “Zawadi ya Ushindi”
ya B. Mtombwa.
Riwaya ya uhalifu ni riwaya ambayo hujihusisha na
uhalifu wa aina mbalimbali kama vile ujambazi, uuaji, magendo na utapeli. Mfano
“Kwa sababu ya Pesa” ya Simbamwene na “Sanda ya Jambazi” ya H. Jajab.
Riwaya ya upelelezi ni aina ya riwaya ambayo huwa na
vitu viwili yaani kosa /uhalifu na upelelezi wa uhalifu huo hadi mhalifu
anapopatikana, hivyo wahusika wake ni wahalifu, wadhurumiwa na wapelelezi
wakiwemo polisi “Mzimu wa Watu wa Kale” ya M.S. Abdallah na “Duniani kuna Watu”
ya M.S. Abdulla.
Baada
ya kuonesha aina za riwaya ambazo zimeainishwa na wataalamu hawa wote sasa tuangalie aina za riwaya ambazo wanafanana Wamitila na Mulokozi aina hizo ni kama zifuatazo;
Riwaya barua ni riwaya ambayo huwa na muundo wa barua kuanzia mwanzo
hadi mwisho mfano “Pamela” ya
S.Richardson na “ Barua Ndefu kama Hii”
Riwaya ya vitisho ni riwaya yenye visa vya kusisimua
damu na mara nyingi visa hivyo huambatana na matukio ya ajabu na miujiza mfano “Mirathi ya Hatari”
ya Mung’ong’o na “Vipuli vya Figo” ya E.
Mbogo.
Riwaya teti ni riwaya ambayo huathiriwa na
kuchimbuka kutegemea jinsi mhusika mkuu anavyosawiriwa. Mhusika huyu huukejeli
mfumo wa kiutawala uliopo katika jamii yake. Riwaya hii huonesha vituko ambavyo
ni vigumu kukubalika vinavyotokea katika jamii mfano “Unfortune Traveler”
ya Daniel Defoi.
Riwaya ya majaribio, ni riwaya inayojadili mkondo wa
nafasi na riwaya kweli. Riwaya ya mjadara nafsi hutungwa bila kuzingatia kanuni
za kawaida za uandishi wa riwaya, watunzi wa riwaya hii hudai kuwa kumbo la
kawaida ya riwaya hii haitoshelezi mahitaji ya karne hii huwakilisha ukweli wa
maisha. Mfano, “Mtunzi wa Hukumu” ya Kasri na “Bina-Adamu” na Musaleo” za
Wamitila.
Baada
ya kuonesha aina za riwaya ambazo zimeainishwa na Mulokozi pamoja na Wamitila
sasa tuangalie aina za riwaya ambazo zimeainishwa na Wamitila na Madumulla.
Riwaya hizo ni kama zifuatazo;
Riwaya ya kitawasifu, ni riwaya ambayo ina muundo
unafanana na muundo wa tawasifu kwa kuyachunguza maisha ya mtu fulani na kwa
nafsi ya kwanza. Mfano riwaya ya “Uhuru wa watumwa” J. Mbotela na “Maisha Yangu
baada ya Miaka Hamsini” ya S.Robert.
Riwaya ya wasifu, ni riwaya ambayo mwandishi
huandika kwa lengo la kumhusu mtu fulani, mfano “Wasifu wa Siti Binti Saad” ya
S. Robert.
Riwaya ya kifalsafa, ni riwaya ambayo inashughulikia
masuala ya kifalsafa. Mada ya kifalsafa huchukua sehemu muhimu katika riwaya ya
aina hii kuliko wahusika, mandhari, msuko au mtukio. Mfano, “Nagona na
Mzingile” ya E kezilahabi na “Umleavyo” ya Haji Gorra Haji.
Baada
ya kuonesha aina za riwaya ambazo zimeainishwa na Wamitila na Madumulla,
tuangalie zile ambazo zimejadiliwa na Mulokozi na Madumulla ambazo
hazijaainishwa na Wamitila.
Riwaya
ya mapenzi ni riwaya yenye kusawiri uhusiano wa kimapenzi kati mvulana na
msichana. Mfano “Kweli Unanipenda” “Mwisho wa Mapenzi” za Simbamwene.
Riwaya ya ujasusi ni wa upelelezi wa kimataifa.
Majasusi ni wapelelezi wanaotumwa na; nchi, serikali au waajiri wao kwenda
katika nchi nyingine kuchunguza siri zao hasa siri za kijeshi, kiuchumi na
kisayansi ili taarifa hizo ziwanufaishe wale waliotumwa mfano “The thirty nine
steps” ya E. Msiba. “Mzimu wa Watu wa Kale”.
Baada
ya kuonesha ufanano wa uainishaji wa aina za riwaya kwa mujibu wataalamu hawa tuangalie aina za riwaya ambazo
zimeainishwa na mtaalamu mmoja mmoja bila wengine kuziainisha aina
hizo.Tukianza na Wamitila ameainisha aina za ruiwaya kama zifuatazo;
Riwaya changamano; ni riwaya ambayo ina muundo mgumu
na inayohitaji umakini kuielewa. Kwa kawaida msuko wa riwaya hii huwa tata.
Inawezekana pakawepo na matumizi mapana ya mbinu rejeshi, upana mkubwa wa
wahusika na mandhari, matumizi mengi ya lugha ya kitamathali, mfano; “Mzingile”
ya E. kezilahabi, “Zirail na Zirani” ya W.E Mkufya.
Riwaya sahili; ni dhana inayotumiwa kuelezea aina
za riwaya ambayo ina muundo rahisi na inaweza kueleweka kwa urahisi. Kwa mfano;
riwaya ya “Kaburi Bila Msalaba” ya P . Kureithi.
Riwaya tatizo; ni riwaya ambayo inajishughulisha
na tatizo au mgogoro fulani katika jamii. Huweza pia kuelezea aina ya riwaya
ambayo inachunguza tasnifu au swala fulani la kisaikolojia. Mfano; “Kuli” ya
Shafi A.shafi na “Mafuta” ya K. Mkangi.
Riwaya kampasi; ni riwaya ambayo mandhari yake ni
chuo kikuu. Hata hivyo hii imepanuliwa na kuhusishwa na kazi za kuchekesha au
zenye mwelemeo wa kitashititi. Kazi za aina hii hukusudia kufichua udhaifu
uliopo katika tabia za wanachuo. Mfano; “Small world” ya David Lorge.
Riwaya ya kiambo; ni riwaya ambayo inatilia mkazo
kwenye mandhari, usemi au muundo wa kijamii na desturi za mahali maalumu.
Mandhari na mahali huathiri njia mbalimbali za kuhisi na kuwaza kwa wahusika
wanaopatikana kazi ya aina hii.
Riwaya ya kidastopia hii husawili jamii isiyokuwa ya kawaida na isiyokuako kwa
wakati maalumu bali inafikirika tu. Katika jamii hiyo sheria za kawaida za
kijamii zimebadilishwa kwa namna inayowafanya watu wengi waishie kutaabika na
kuteseka sana. Mfano wa riwaya hizi ni kama vile “ Kusadikika” ya Shabani
Robert na “Walenisi” ya Katama Mkangi.
Riwaya ya kimonolojia
ni riwaya ambayo sauti inayotawala ni moja. Sauti hiyo ni ya mwandishi.
Wahusika wanaopatikana katika riwaya hii hudhibitiwa kwa kiasi kikubwa na sauti
ya mwandishi. Mfano “Walenesi” na “Mafula” za Katama Mkangi.
Riwaya ya kipolifoni; ni riwaya ambayo inahusishwa na
urejeleaji ambapo kila wahusika
wanapozungumza au kuongea sauti zao mbalimbali zinawakilisha mikabala
mbalimbali kiitikadi. Mfano “Dunia mti mkavu” ya S.A Mohamed.
Riwaya ya kisasa; ni riwaya inayohusu wanasiasa na
maisha yao wanasiasa. Hudhamiria kuyafichua mambo yanayotendeka kinyume na
picha inayoonekakana waziwazi. Mfano; “Nyota ya Huzuni” ya George Liwenga na
“Njozi Iliyopotea” ya C.G. Mng’ong’o.
Riwaya ya kitarihi ni riwaya ambayo inajihusisha na
mawanda makubwa ya kiwakati na kimandhari.Wahusika wengi walioteuliwa kuakisi
hali mbalimbali za kijamii na kiuchumi za wakati maalumu. Mfano;Riwaya ya “Habari za Wakilindi”
Riwaya ya Kitasnifu ni riwaya inayojihusisha na tatizo
fulani la kijamii hasa kwa nia ya kuwahusisha
wasomaji. Katika hali fulani inayowapata wahusika na kwa njia hiyo
huwachochea kuwazia njia ya kusuluhisha tatizo hilo Mfano; “Njozi Iliyopotea”
ya M.Mng’ong’o na “Nyota ya Huzuni” ya G.Liwenga.
Riwaya ya kiutopia hii ni riwaya ambayo inasawiri
jamii anayoiona mwandishi kama jamii kielelezo na aghalabu huhusisha sifa za
Kifantasia au kinjozi. Mfano wa riwaya hii ni kama, “Siku ya Watenzi Wote” ya
Shaaban Robert
Riwaya ya kiurejelevu hii ni riwaya inayojirejelea.
Aghalabu katika usimulizi wake, riwaya
ya aina hii huishia kutoa maoni kuhusu usimulizi wake na njia za kubuni
na kutunga riwaya.Tunaweza kusema hii ni riwaya inayofichua mbinu zake za
kiutunzi. Mfano “Musaleo” ya K.W.Wamitila
Riwaya kinzani ni riwaya inayotumiwa kuelezea
ambayo imekwenda kinyume na matarajio au kaida za uandishi wa riwaya. Mfano,
kuwa na muundo wa kimajaribio wahusika kukosa motisha, kuwako kwa matendo
yasiyoweza kuungwa kimantiki.
Riwaya ya utetezi
hii hutumiwa kuielezea riwaya ambayo inahusu matatizo ya kijami,
kiuchumi pamoja na dhuluma inayowapata wanyonge au wasiokuwa na uwezo katika
jamii fulani. Hivyo riwaya hii hukusudia kurekebisha hali iliyopo katika jamii.
Mfano “Walenisi” na “Mafuta” ya Katama
Mkangi na “Kuli’ na “Vuta
n’kuvute” za Shafi A.Shafi.
Pia
kuna baadhi ya aina za riwaya ambazo
zimejadiliwa na Mulokozi ambazo
hazijajadiliwa na Wamitila na Madumulla. Aina hizo za riwaya ni kama zifuatazo;
Riwaya chuku
ni riwaya ambayo hueleza vituko na masahibu yasiyo kuwa ya kawaida, ni
riwaya ambayo haizingatii uhalisia na
mara nyingi masahibu yake huambatanana mapenzi.Mfano “Alfu lela Ulela” ya G.
Bocci ccio na “Kusadikika” ya S.Robert”
Riwaya ya kingano, ni riwaya yenye umbo na mtindo wa
ngano mathalani huweza kuwa na wahusika wanyama,visa vyenye kutendeka nje ya
wakati wa kihistoriA.Mfano “Lila na Fila” ya Longman na “Adili na Nduguze” ya S.Robert
Riwaya istiara ni riwaya mafumbo ambayo umbo lake
la nje ni ishara au kiwakilishi tu cha jambo jingine. Mfano “Kusadikika” ya S.Robert ambayo inasawili utwala wa mabavu na “Shamba la Wanyama” ya Kawegere.
Riwaya tendi ni riwaya yenye mawanda mapana kama
tendi aghalabu riwaya hii husawili matendo ya ushujaa na masuala mazito ya
kijamii yenye kuathiri historia ya taifa husika. Mfano “Vita na Amani” ya Leo
Tolstoi na “Chaka Mtemi wa Wazuru” ya Thomas M.
Riwaya ya kisayansi ni riwaya inayotumia taaluma ya sayansi kama msingi wa matukio, masahibu
na maudhui, mathalani riwaya hii hubashiri namna sayansi itakavyo athiri
maendeeo ya mwanadamu katika karne zijazo. Mfano “Safari Kiini cha Dunia” ya
Jules Vernes.
Kuna
baadhi ya aina ya riwaya ambazo zimejadiliwa na Madumulla ambazo hazijadiliwa
na Mulokozi na Wamitila. Ambazo ni kama zifuatazo;
Riwaya ya kimaadili ni riwaya ambayo ina nia ya
kufundisha maadili fulani mfano “Kufikirika” ya S Robert. Ni riwaya inayotoa maadili kwa jamii.
Riwaya ya kimapinduzi ni riwaya ambayo inajadili migogoro
na maisha ya binadamu kwa kutafakari kwa mantiki na kina kuhusu mambo ambayo
urazini wake hauonekani kwa urahisi. Mfano “Umleavyo” ya Haji na Kichwa Maji”
ya E.Kezilahabi.
Hivyo
kutokana na uainishaji huu wa aina mbalimbali za riwaya kutoka kwa wataalamu
hawa tumeona kuwa wanatofautiana katika vigezo vya uainishaji ambapo tunaona
wanaainisha aina mbambali za riwaya. Kutokana na uainishaji huo tunaweza
kuhitimisha kwa kusema kuwa aina hizo zote za riwaya zinaweza kuangukia katika
aina kuu mbili za riwaya ambazo ni riwaya ya dhati na riwaya pendwa. Riwaya
pendwa ni riwaya ni riwaya ambazo hutungwa kwa lengo la kuburudisha na
kumstarehesha msomaji mfano, riwaya za kimapenzi, kimahaba, kiuharifu,
kiupelelezi na kijasusi. Wakati riwaya ya dhati ni riwaya ambazo huchimbua na
kuchambua masuala mbalimbali ya kijamii, yaani hutafuta chanzo chake sababu
zake mpaka kikatokea athari na suluhisho lake. Hivyo tunaweza kusema kuwa aina
za riwaya ambazo hukosekana katika aina mojawapo ya riwaya dhati huwa
katika riwaya pendwa.
MALEJEO.
Madumulla,
S.J. (2009) Riwaya ya Kiswahili: Nadharia Historia na Misingi ya Uchambuzi.
Dar es Salaam:
Mture Educational Publishers Ltd.
Mulokozi,
M.M. (1996) Utangulizi wa Fasihi ya
Kiswahili. Dar es Salaam: TUKI.
Senkoro,
F.E.M.K. (2011) Fasihi. Dar es
Salaam: KAUTTU.
Wamitila,
K.W. (2002) Uhakiki wa Fasihi: Misingi na
Vipengele Vyake. Nairobi: Phoenix
Publishers Ltd.
Wamitila,
K.W. (2003) Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Publicatins
Ltd.
MTINDO WA MWINGILIANOMATINI KWENYE
KAZI ZA FASIHI.
UCHAMBUZI WA TENDI.
Makala hii ina lengo la kutaka kujua kama tendi za
Kiswahili huwa na mwingiliano matini
na kubainisha vipengele
vilivyoingiliana katika utanzu huu na dhima zake. Waandishi wa tendi
mbalimbali za Kiswahili, wamekuwa wakitumia mtindo wa kuchanganya vipengele
mbalimbali vya kisanaa katika kazi moja. Mbinu hii inatazamwa na makala haya
kuwa ni mwingilianomatini katika tendi za Kiswahili. Mathalani, mwandishi anayeandika
au simulia tendi za Kiswahili, hujikuta akichanganya matini za nyimbo,
semi, hadithi ndani ya
hadithi, maigizo, matumizi
ya ishara, ngoma na
kadhalika. Kuchanganya huko
kwa vipengele tofauti katika
kazi moja ni
kitu ambacho kimezoeleka
sana miongoni mwa wanafasihi. Kipengele hiki kinahitaji
kuandikiwa ili kuweza kuweka bayana kuwa katika tendi kunaweza kuwa na sifa
mbalimbali za tanzu nyingine na
kuziorodhesha ili zijulikane wazi. Hivyo makala haya yatakuwa na lengo la
kuthibitisha uwepo wa mwingiliano huo.
Utangulizi
Mwingilianomatini katika kazi za fasihi ni
dhana ambayo imekuwa
ikijitokeza sana kwa sababu
mbalimbali za kifasihi. Wakati mwingine
mwingiliano huu hubainishwa kabisa
na wataalamu wa fasihi simulizi kama
mtindo wa kawaida katika kumbo za fasihi. Kwa mfano, Mulokozi
(1989) anasema kwamba mojawapo ya
sifa kuu ya
fasihi simulizi ni
vipera vyake kuingiliana
katika utendaji. Pamoja na mtindo huo
kuwa wa kawaida
katika fasihi, bado
sababu zake hazijabainishwa wazi katika uhakiki wa kazi za fasihi.
Kwa mantiki hiyo, kuna
haja ya kuchunguza
sababu zake ili
kupanua uelewa katika
taaluma ya fasihi. Makala haya
yana lengo la kuzionesha sababu hizo za kuingiza vipengele mbalimbali vya
kisanaa katika fasihi kwa kuchunguza tendi.
Pengine,
tuanze kwa kujiuliza swali, mtindo ni nini? kisha tutafasili dhana ya
mwingiliano matini, tendi, kisha tutaangalia vipengele ambavyo vimeingiliana
katika tendi za Kiswahili na dhima zake na mwisho ni hitimisho.
Tukianza
na fasili ya mtindo; Senkoro (2011) anasema mtindo katika kazi ya fasihi ni ile
namna ambayo msanii hutunga kazi hiyo na kuipa sura ambayo kifani na kimaudhui
huainisha kanuni au kaida zilizofuatwa kama ni(za kimapokeo) au ni za kipekee.
Wamitila K.W (2008) anasema mtindo ni
sifa ya upekee ambayo huitambulisha kazi ya mtunzi au msanii fulani.
Kwa
ujumla fasili hizi hazipishani sana, ukizichunguza utagundua kuwa mtindo hujihusisha
na namna ambayo msanii huitunga kazi yake ambayo huwa na upekee wa namna
fulani; upekee huu ndio unaoweza kuwatofautisha
waandishi. Hivyo basi kwa kutumia mtazamo wa kimtindo tunaweza kufasili
mwingilianomatini kama alivyofasili Senkoro (2011) kuwa ni mbinu ambayo huonyesha kutumiwa kwa utanzu
mmoja wa fasihi katika kutolea au kuwasilisha utanzu mwingine. Kwa mfano si
jambo geni kukuta wimbo au kipande cha wimbo ndani ya ngano au hadithi. Hivyo
basi tunaweza kusema kuwa mwingilianomatini ni ule uwepo wa sifa mbalimbali za
matini moja au zaidi katika kazi fulani ya fasihi kama vile matumizi ya nyimbo,
matumizi ya barua, ngoma, masimulizi ya hadithi ndani ya hadithi, misemo,
nahau, majibizano, vicheko, picha na michoro na kadhalika. Baada ya hapo tuangalie
tendi ni nini? Jibu la swali hili ni muhimu ili kupata uelewa wa awali katika hoja
za makala haya. Zipo maana kadhaa
zinazotolewa na wanafasihi mbalimbali
kuhusu dhana ya tendi.
Mulokozi
(1996) anafafanua tendi kuwa, ni utungo wenye kusimulia matukio ya kishujaa
yenye uzito wa kijamii au kitaifa. Matukio haya yaweza kuwa ya kihistoria
lakini tendi nyingi huchanganya historia
na visakale au visasili. TUKI
(2004) wanasema tendi ni utanzu unafaa kusherekewa kishujaa. Hii
inaonyesha kuwa tendi zinahusu matukio ya kishujaa yaweza kuwa ya kweli
au ya kubuni, na yenye funzo fulani kwa jamii.
Kutokana
na fasili ya tendi tunayopata kupitia maoni ya wataalamu hawa tunabaini kuwa
utendi ni mojawapo ya tanzu za kazi za kifasihi. Utanzu huu unaweza kuwa katika
umbom la kiusimulizi au la kiuandihi. Kwa mantiki hiyo, tendi kama zilivyo
tanzu nyinginezo za kifasihi huwa na mitindo anuai. Mojawapo ya mittindo yake
ni suala la mwingiliano matini.
Data ya
makala haya imepatikana
kutoka katika sampuli
ya kitabu cha Utenzi
wa Nyakiiru Kibi kilichoandikwa
na Mulokozi (1997). Uteuzi wa kitabu hicho
kama sampuli umefanyika kwa nasibu. Unasibu huo umetokana na imani kuwa
mbinu hii ya mwingilianomatini hujitokeza katika tendi zote. Hivyo hakukuwa
na haja ya kuweka
vigezo vingi vya
uteuzi. Lakini, kwa
ujumla makala imeteua kitabu hicho
kwa kuzingatia kigezo cha matukio yake kuwa
na ujumbe kwa jamii, lugha
rahisi, muundo sahili, na kadhalika. Utenzi huu unasimulia historia ya
kuanzishwa kwa utawala wa ukoo wa Babito katika nchi ya Kiziba, wilaya ya
Bukoba, karne ya 15. Babito walikua ni wahamiaji wa Kiluo kutoka
Uganda.Walifika Kiziba kutokea Bunyoro nchini Uganda, ambako walikuwa tayari ni
watawala. Historia ya Babito katika maeneo haya inaonyesha namna watu wa jamii
na lugha mbalimbali hapo kale walivyokua na ushirikiano mzuri katika kujenga
utaifa na ustawi wao. Siasa za ukabila na ubaguzi hazikua na nguvu. Mhusika
mkuu katika andiko hili ni Nyakiiru. Huyu anasimuliwa kama mhusika shujaa.
Nyakiiru alikua ni kiongozi wa kundi la Babito lilofika Kiziba kama mwaka 1945;
ambapo alishirikiana na Kanyamaishwa, ambaye alikuwa ni mototo wa mfalme wa
Kiziba aliyeitwa Ntumwa, kumwua mfalme huyo na hivyo kujichukulia madaraka ya
utawala.
Hadithi
ya utenzi huu imetokana na masimulizi ya wazee ambayo yamehifadhiwa katika
vichwa vya watu na kupokezwa kwa mdomo tangu karne ya 15. Hata hivyo yako mambo
kadha ya msingi ambayo yanajitokeza takribani katika masimulizi yote. Mambo
hayo ndiyo mwandishi amejaribu kuyatumia kama kiini cha utenzi huu na amejaribu
kuyapanga kisanaa ili kupata hadithi nzuri na yenye mshikamano na mtiririko
mzuri unaofaa, na wenye mafunzo fulani kwa vizazi vya leo. Hivyo utenzi huu
hausimulii historia kavu, bali unasimulia hadithi ya kusisimua inayotokana na
historia iliyochanganyika na visakale ambayo ni masimulizi yanayohusu mashujaa
wa kale ambayo yamechanganya ubunifu ndani yake na yaweza kuwa ya kweli au ya
kubuni. Utenzi huu umekusudiwa usomwe na vijana. Hivyo lugha yake imerahisishwa
kidogo ili ieleweke vizuri kwa walengwa.
Mwega wa Kinadharia
Makala haya
yataongozwa na mwega wa
kinadharia wa mwingilianomatini. Ili
hadhira ya fasihi ielewe kazi yoyote ya fasihi lazima ihusishe vipengele
vingine nje ya muktadha
wa usomaji au
usimulizi ule (Mshengyezi,
2003). Dhana ya kuingiza vipengele
hivi ndiyo huitwa
mwingilianomatini. Wataalamu
wanaounga
mkono mawazo ya nadharia hii wanamtaja mwasisi wa nadharia hii kuwa ni Mikhail
M. Bakhtin ambaye alikuwa mwanaisimu na mhakiki wa kazi za fasihi aliyeishi
kati ya mwaka 1895-1975 (Njogu na Wafula, 2007). Njogu na Wafula wanazidi
kusema kuwa Bakhtin
aliamini kwamba kazi
ya fasihi ina sauti mbalimbali
zinazoingiliana na kupiga mwangwi
katika kazi nyingine zilizotangulia, zilizopo au
zitakazokuja baadaye.
Ufafanuzi huo pia uliwahi kutolewa na
Wamitila (2006) aliposema
kuwa Bakhtin anaamini
kuwa utanzu wa riwaya una uwezo
wa kuingiza vipengele vya tanzu nyingine lakini ukabakia na sifa
zake kama utanzu.
Hali hiyo ndiyo
pia hujitokeza katika
tendi mbalimbali za Kiswahili
ambazo zina mwingiliano
na vipengele vingi
sana katika kazi moja.
Kwa ufafanuzi wa
Wamitila, utanzu wa
fasihi kuwa na vipengele
vingine ndani yake hakuondoi
hadhi ya utanzu
huo. Kwa ujumla, tunaposema kuingiliana
kwa matini katika
kazi za fasihi
tunamaanisha kazi moja ya
kifasihi kuwa na sifa za tanzu nyingine ndani yake. Kabla hatujaenda kuona
vipengele hivyo vilivyojitokeza katika tendi hebu tuangalie kwanza sifa za
tendi za Kiswahili.
Sifa
za Tendi za Kiswahili
Molukozi
(1996) kama alivyomnukuu Finnegan
(1970:108) anasema kuwa utanzu huu hautokei sana katika Afrika, pamekua na mjadala mrefu kuhusu fani
hii. Wataalamu kama Okpewho (1979)
Johnson (1986) Mulokozi (1987) na wengine wamethibitisha kuwa utendi ni fani
iliyoenea sana katika Afrika, na wamejeribu kuonyesha baadhi ya sifa zake.
Finnegan alibainisha sifa nne za tendi simulizi:
Ø Nudhumu: Utendi aghalabu ni utungo
wa kishairi.
Ø Urefu: Anasema ni utungo mrefu.
Ø Upatanifu: Anasema ni utungo ambao una visa
vilivyounganika kimantiki.
Aidha
Mulokozi anaendelea kusema kuwa zaidi ya sifa za utendi
alizoelezea Finnegan, ambazo wengi wanaona hazitoshelezi, uchunguzi wao
umedhihirisha kuwa utendi una sifa zifuatazo:
Ø Hutolewa kishairi
Ø Huhusu matukio muhimu ya kihistoria
au kijamii;
Ø Huelezea habari za ushujaa na
mashujaa; hii inamaanisha kuwa husimulia juu ya maisha na matendo ya kishujaa
ya mbabe wa utendi, kwa mfano kuzaliwa kwake, maswaibu yake, safari zake,
uongozi wake kwa watu wake, na kifo chake.
Ø Matini (maneno) yake kwa kawaida
hutungwa papo kwa papo (utendi hautungwi kabla ya kuhifadhiwa kichwani kwanza
ili badaye utolewe kwa ghibu).
Ø Hivyo, hutawaliwa na muktadha wa
utungaji na uwasilishaji wake kwa jamii.
Baadhi
ya tendi muhimu za Kiafrika ni Sundiata
(au Sunjata) (Mali, Gambia, na) Mwindo (Zaire), Silamaka (Mali) na Mvet
(Gabon). Katika Afrika Mashariki, tunao ushahidi kuwa tendi ziko au zilikwepo
katika jamii zifuatazo: Wachaga (Mlire); Wahehe (Mukwavinyika); Wanyambo na
Wahaya (Kachwenjanja, Mugasha); Wakwere na Wazinza. Anasema hata hivyo,
uchunguzi bado hujakamilika, na huenda zipo jaamii nyingine zenye utanzu huu.
Hatuwezi kupinga hoja za mtaalamu huyu wa fasihi kwani hoja zake zinaonekana
kuwa na ushawishi kuwa tendi zilikwepo na pia zina sifa kama hizo alizobainisha
hususani kuhusu mashujaa na matukio ya
kishujaa; yaweza kuwa ya kweli au ya
kubuni au ya kihistoria. Hii ni kwa sababu tendi ni sanaa inayoambatana na hali
fulani ya kijamii, hasa ile hali yenye vuguvugu la mapambano, na yenye asasi
(kama vile ufalme) zinazoweza kuidhamini
sanaa ya utendi. Hii ni sanaa ambayo hufa, kwa vile mazingira yanayoilea na
kuirutubisha hayapo tena, hivyo ni
muhimu kuzirekodi na kuzihifadhi zile tendi chache tulizo nazo kabla
hazijatoweka au kusahaulika kabisa na kupotea katika jamii. Baada ya kuona sifa
hizo za tendi za Kiswahili sasa tuangalie
vipengele vilivyojitokeza katika utanzu huu.
Tanzu Zinazojitokeza katika Tendi za
Kiswahili
Tanzu zinazojitokeza katika
tendi ni nyingi, lakini hapa
tutatumia vipengele vichache tu
vinavyojitokeza katika tendi za Kiswahili. Katika Utenzi wa Nyakiiru Kibi
kuna vipengele au sifa mbalimbali za
tanzu nyingine ambazo mwandishi
ameziingiza katika utanzu huu, tanzu
hizo ni kama hizi zifuatazo:
Picha au Michoro mbalimbali
Makala
yanatumia dhana ya picha na mchoro yakimaanisha uwakilishi wa sura ya mtu/watu
au kitu/vitu au mahali kwenye
karatasi au kitu
chochote kinachoweza
kuandikwa juu yake. Sura
hiyo inaweza kuwa
imechorwa, imechongwa au tengenezwa. Katika utanzu huu picha zinaonekana
katika jalada, pia katika ukurasa wa 1,2, 3, 7,8, 9,10,11, 12, 15 19, 20, 23,
24,25, 26, 28, 30, 33,39,44,50,54, 55, 60, 61, 64, 65,66, 69,75,83,87, 88,90 na
91. Mwandishi amejaribu kutumia michoro na picha katika utanzu huu ambako
inasaidia kutoa ufafanuzi wa kina juu ya matukio yaliyojitokeza katika utenzi
huu na vile vitu vilivyotumika katika utenzi huu na maeneo mbalimbali
yaliyohusika au husishwa katika kukamilisha matukio au utendekaji wa matukio
mbalimbali na picha za watu mbalimbali.
Kwa mfano katika jalada la kitabu mwandishi ameonesha mchoro wa ngoma
ikimaanisha ngoma ni chombo muhimu cha kijadi katika jamii na picha za vibuyu
hii ikidhihirisha kuwa kuna mambo ya kijadi yaliyokua yakitendeka katika jamii
zetu na hii inaonesha uzalendo kwa kuenzi utamaduni wetu; pia katika kurasa za
mwanzoni kabisa kunaonekana picha za watoto wamekaa wanasoma vitabu ikionesha
kuwa ni ishara ya kuhamasisha watoto wajijengee utamaduni wa kujisomea vitabu,
bado katika kurasa hizo kuna michoro ya ramani ambazo zinaonyesha maeneo
yaliyozungumziwa katika utenzi huu; hii inasaidia wasomaji kuelewa kwa urahisi
kile kilichozungumziwa katika kazi hii na kuweza kuvuta hisia zaidi na
kujijengea taswira za ulimwengu mpya. Aidha tukiangalia katika ukurasa wa
10,25,44,50 na 88 tunaweza tukaona jinsi mwandishi ameonesha picha za baadhi ya
matukio yaliyokua yanatendeka mfano upigaji wa ngoma, Nyakiiru akipambana na
chui, mapambano katika ukurasa wa 88 ambako Nyakiiru alitoka na jeshi lake
akaenda kushambulia maadui Bugandika na watu wakauana sana; kwa kuangalia picha
hizo zinavuta hisia za huzuni na wakati mwingine zinatujengea ujasiri kutokana
na matukio ya kishujaa yaliyotokea. Katika tendi simulizi, dhana ya picha
hujitokeza kwa sifa kadhaa za mwonekano wa wahusika wa tendi zinazofafanuliwa na
msimulizi mbele ya hadhira. Kwa mfano, wadudu
watapewa sifa ya jitu kubwa
lenye uwezo wa kufanya maajabu makubwa kijiji kizima, kwa mfano katika ukurasa wa 75 katika ubeti wa 724 na725 mwandishi amechora
picha zinazoonesha jinsi senene walivyoweza kutishia kijiji kizima cha Baziba.
724
Senene kwenye mashamba 725 Senene
miti kishika
Matawi
yanavunjika Senene
kwenye miamba
Kwenye
mapaa ya nyumba Matunda yanaanguka
Na mashina kupembea! Senene
wakatambaa!
Hivyo
kipengele hiki cha michoro na picha mbalimbali ni moja ya sifa za utanzu
mwingine ambazo tunaweza kusema zimeingizwa katika tendi, na michoro hii
imesaidia kufanya matukio yaweze kueleweka kwa urahisi pale ambako
hayakueleweka vizuri aidha yamepelekea kuleta uhalisia wa matukio na visa hivyo
kwa hadhira na jamii nzima. Hivyo
michoro hukazia uelewa na kufikisha ujumbe kwa urahisi na kuimarisha maudhui,
uhalisia wa jambo na huleta mvuto kwa wasomaji na kuchochea udadisi kwa
hadhira.
Hadithi ndani ya Hadithi
Hadithi
ndani ya hadithi ni dhana
inayomaanisha simulizi moja
kuingiliwa na nyingine. Kwa mfano, mwandishi kama msimulizi mkuu wa
hadithi anampa nafasi mhusika
katika hadithi kusimulia hadithi nyingine. Katika dhana
hii kunakuwa na
hadhira tofauti kutokana
na idadi ya usimulizi.
Mathalani, tunaposoma
hadithi halafu ndani
ya hadithi hiyo
tukakuta mhusika mwingine ndani ya hadithi hiyo
akiwasimulia wengine, hapo tunakuwa na hadhira ya aina mbili. Sisi kama wasomaji tunakuwa
hadhira, na wale
wanaosimuliwa na mhusika katika
hadithi nao pia
ni hadhira nyingine.
Kwa mfano, ndani ya hadithi ya
kitabu cha Nyakiiru Kibi kuna wasimulizi wawili. Mmoja ni mwandishi
mwenyewe akisimulia historia ya
kuanzishwa kwa utawala wa ukoo wa Babito katika nchi ya Kiziba ambapo naye
anasema hadithi hii imetokana na masimulizi ya wazee yaliyohifadhiwa kwenye
vichwa vya watu. Msimulizi mwingine ni
Nyakiiru wa hadithini na Kanyamaishwa wakimsimulia Mtukufu wa Omukama wa Jamala
kuhusu maisha yao na walikotokea na jinsi walivyokua wanaishi na kazi waliyokua
wanaifanya toka utotoni, ujuzi
walionao na nasaba yao kwa
ujumla. Hapa tunaona jinsi kipengele hiki kilivyojitokeza katika tendi hii na
Nyakiiru na Kanyamaishwa wamekua kama wasimulizi na Mtukufu Omukama kawa kama
hadhira katika ukurasa wa 67 ubeti wa 634 hadi 641.
Pia
usimulizi mwingine unaonekana ukurasa katika
wa 80 ubeti wa 775 hadi 780 ambako kuna masimulizi juu ya safari ya
Nyakiiru na Kanyamaishwa wanaelekea Ikulu kwa Sulutani. Hata katika ukurasa wa
6 mwandishi amejaribu kuingiza masimulizi katika ubeti wa 55 ambako inaelezwa
habari za kuwepo kwa Sulutani enzi za zamani ambaye ilikuwa mkali kupindukia.
Hivyo masimulizi haya yanasaidia kuingiza vionjo mbalimbali katika tendi na kuendeleza uwepo wa matukio
mbalimbali katika tendi hii huwafanya hadhira wasichoke kufuatilia matukio
yanayoelezwa katika tendi na kuongezea
ufahamu wa mambo mbalimbali na kuyahusianisha na mazingira yao ya kila siku.
Hiki nacho ni kipengele ambacho pia kinajitokeza katika kazi za kifasihi kama vile tendi kwa
sababu katika kila tukio huenda kukawa na tukio jingine ndani yake au
kinachohusiana na tukio hilo,hivyo mwingiliano wa matukio hayo ndiyo
unaopelekea uwepo wa mtindo wa mwingiliano matini katika tendi za Kiswahili.
Maigizo
Maigizo ni
matendo ya kumithilisha
kitu au tabia
fulani kwa nia
ya kufikisha ujumbe kwa
jamii. Matendo yanayoweza kuigizwa ni kama vile uchawi, ulevi, ugomvi, matambiko, uganga, michezo ya ngoma,
kusalia miungu, mapambano, uwindaji,
unyanyasaji, kuzaliwa kwa mtoto na
kadhalika. Mambo hayo hufanywa
na wahusika wa kimaigizo mbele ya
hadhira ili kufikisha ujumbe. Matendo yanayofanywa
na wahusika wa
kimaigizo siyo halisi
kwa kuwa wahusika wa kifasihi sio
watendaji wake halisi, bali wahusika huvaa tu uhusika kama nguo kwa
muda ili kuwakilisha
watendaji halisi katika
jamii.
Aidha,
maigizo ni kipengele mojawapo
cha sanaa za
maonesho chenye sifa
zifuatazo: dhana inayotendeka, uwanja
unaotendewa, watendaji, hadhira (watazamaji), kusudio la kisanaa,
muktadha wa kisanaa na ubunifu (Mulokozi, 1996). Katika tendi mara nyingi fanani hulazimika kuingiza
matini ya maigizo
katika usanii wake.
Endapo matukio yanayotokea
katika kisa chake
yanaweza kuigizika basi
anayehadithia hulazimika kuigiza.
Kwa mfano, msimuliaji
wa hadithi akisimulia hadithi
yake yenye mhusika au wahusika wanaoimba basi msimuliaji
huyo hujikuta akiimba
mbele ya hadhira.
Huu ni uigizaji.
Kuna matendo mbalimbali ambayo yameigizwa katika utenzi
huu ambayo yanatokea katika jamii kama vile uwindaji, mambo ya uganga au
matumizi ya waganga jadi, wazee wa jadi na imani za kishirikina mfano katika
ukurasa wa 18 katika ubeti wa 156 mwandishi anaonyesha jinsi jamii ya Kiziba
ilivyokuwa inaamini kutokana na maajabu yanayotokea katika jamii mfano Mtoto wa
Malikia alivyotangulia kuota meno ya juu, waliamini kuwa ile ni ishara ya kutokea kwa balaa badae; Pia kuna maigizo ya
matambiko ambako familia ya Mfalme iliamua kutambikia baada ya kuona mwanao
ameanza kuota meno ya juu wakahisi huu ni mkosi au kisirani katika familia yao
kwa mfano katika ukurasa wa 47 ubeti wa 439 mwandishi anasema;
439 Sala wakazitongoa
Tambiko
wakazitoa
Zipate
kuwafikia
Miungu wenye afua.
Aidha
uigizaji uliendelea katika mambo
mengine yanatokea katika jamii kama vile unywaji wa pombe (ulevi) ambapo
inaoeshwa kuwa jamii ilikua inakunywa pombe ili kupunguza mawazo au kusahau
maswaibu yanayowakumba na wakati
mwingine kuongeza ujasiri wa kutenda jambo fulani kwa mfano katika ukurasa wa
409 na 412 anaonyesha akina Nyakiiru
na Kanyamaishwa walivyokuwa
wanakunywa pombe mpaka wanalewa kisha
wanachukua silaha zao wanaenda mawindoni.
409 Wote wamekwishalewa
Na
hawakujitambuwa
Mutalala kazidiwa
Wengine kuwapitia.
Maigizo
mengine ya sherehe ambako tunaona familia ya mfalme ilikuwa inasherekea
kuzaliwa kwa mtoto wa Malkia. Haya tunayaona katika ukurasa wa 9 ubeti wa 75 na
76 wanajamii wakihamasishwa kusherekea kwa kupita ngomezi (la mgambo).
75 Likipigwa la mgambo 76 “Malkia
mtukufu
Likilia lina jambo Kazaa mwana nadhifu
“Ikuluni kuna mambo Mwingine hafui dafu
Kajifungua malkia Kunawiri kazidia.”
Kipengele
hiki cha maigizo huwa kinajitokeza sana katika kazi za kifasihi ikiwemo tendi
kwa lengo la kuweka msisitizo wa yale
matukio yanayotendeka katika jamii na
kuleta uhalisia aidha wakati mwingine kuifanya jamii iamini kuwa matukio hayo
yapo na bado yanatokea katika jamii na kujifunza kupitia matukio hayo. Hivyo
kuwepo kwa kipengele hicho kinawakilisha mwingilianomatini katika tendi.
Semi
Semi ni
tungo au kauli
fupifupi za kisanaa
zenye kubeba maana
au mafunzo muhimu ya
kijamii. Semi zinajumuisha
tanzu kama vile
methali, vitendawili,
mafumbo, misimu, lakabu
na kauli-tauria (Mulokozi,
1996). Fasili hii ya Mulokozi
haitofautiani sana na ile ya M’Ngaruti
(2008) anayesema kuwa semi
ni tungo
au kauli fupi
za kisanaa zinazobeba
maana au mafunzo ya kijamii. Katika tendi watunzi
wengi huingiza semi mbalimbali kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii fulani au
wakati mwingine hutumika katika kuonya au kukataza jambo na kutoa tahadhari.
Katika utenzi huu pia tunaona mwandishi ameingiza semi mbalimbali kama
tunavyoziona katika kurasa zifuatazo 35,
37, 38, 48, 58 na 68. Semi hizo ni kama
zifuatazo;
Ø Misuli ya dume katika
ukurasa wa 35 ubeti wa 307.
Ø Usiku wa kiza katika
ukurasa wa 35 ubeti wa 310.
Ø Wakata nguu na nyanda katika ukurasa wa 36 ubeti wa 320.
Ø Giza ni mama wa nuru katika ukurasa wa 37 ubeti wa 331.
Ø Uongozi si udhuru katika ukurasa wa 37 ubeti wa 333.
Ø Penye mamba pana mto katika ukurasa wa 38 ubeti wa 345.
Ø Penye moshi pana moto katika ukurasa wa 38 ubeti wa 345.
Ø Maisha yangu ni yako katika ukurasa wa 58 ubeti wa 554.
Ø Adui zako ni zetu katika ukurasa wa 68 ubeti wa 648.
Hizo
ni baadhi ya semi ambazo zimejitokeza katika utenzi huu, hii ni dhahiri kuwa
semi hizi hutumiwa katika kazi za kifasihi kwa lengo la kutoa ujumbe fulani,
kuhamasisha suala fulani, kulinganisha vitu fulani na kutahadharisha jambo
fulani. Mbali na hayo baadhi ya semi hukusudia kuleta mtiririko wa matukio
utakaounganisha sehemu katika visa vyao.
Matumizi ya Nahau
Katika
utenzi huu pia matumizi ya nahau nayo yamejitokeza, ambako ni moja ya sifa za
tanzu nyingine zilizoingizwa katika tendi. Nahau ni moja ya semi ambazo zina mafumbo ndani
yake na zina lengo la kutoa ujumbe filani kwa njia ya kutumia maneno mengine
tofauti na kitu kinachozungumziwa. Hivyo jamii hutumia nahau kwa lengo la
kukosoa au kuelezea kitu au sifa na tabia za mtu kwa namna ya tofauti. Mara
nyingi si rahisi kuweza kutambua maana ya hizo nahau kama miongoni mwa
wanajamii wanaotumia nahau hizo. Hivyo wakati mwingine huwa ni vigumu kupata maana zake kwa haraka. Katika tendi
nahau nazo zinatumika katika kukamilisha maudhui na kuongeza sifa za wahusika
waliotumika. Miongoni mwa nahau hizo tunaziona katika kurasa na beti mbalimbali
kwa mfano “Kaingia kwa mabavu” katika
ukurasa wa 6 ubeti wa 60, “Mashavu yamemtuna” katika ukurasa wa 34 ubeti wa
297, “Damu inatuchemka” katika
ukurasa wa 34 ubeti wa 303, “kukata maini, kubwaga moyo, kumtia mtu
simanzi”, “ana mguu mmoja” katika ukurasa wa 4 ubeti wa 33, “jicho lake ni jua” katika ukurasa wa 24
ubeti wa 17, “sauti yake ni radi”
katika ukurasa wa 2 ubeti wa 27. Nahau hizi zimebeba mengi ndani yake ambayo
yanalenga kufikisha ujumbe kwa jamii na pia zinasaidia kuweza kutambua
muonekano wa kitu fulani na kufikirisha
jamii.
Matumizi ya vilio na vicheko
Halikadhalika
katika katika tendi huwa kuna maswaibu mbalimbali ambayo huibua hisia kwa
wahusika ambazo zaweza kuwa za furaha au huzuni
na kupelekea vilio au vicheko. Vicheko huwa vinaweza kuashiria mambo
mengi katika jamii kama yafuatayo: furaha, kebehi au kejeli, mzaha au dharau.
Kwa upande wa vilio navyo vyaweza kuashiria furaha, huzuni au majonzi, matatizo
au mikosi, maumivu, uchungu na hasira. Katika utenzi huu vilio na vicheko
vimetumika kwa mfano katika ukurasa wa 18, 20, 23, 25 na 34. Katika ubeti wa 34 ukurasa wa 820 mwandishi anaonesha
vijakazi walivyokua wanalia Mukama alipouwawa.
820 Nao vijakazihao
Wakatoka mbiombio
Wakalia “Yoo! Yoo!
Mukama
wamemuua!”
Hivyo
vilio na vicheko navyo vinadhihirisha kuwepo kwa mtindo wa mwingilianomatini
katika tendi na dhima nyingi kwa jamii
kama vile kuonyesha hali aliyo nayo mtu kutokana na jambo fulani lililompata
mfano furaha au huzuni na kadhalika.
Matumizi ya Taharuki
Taharuki
ni ile hali ya kutamani kujua kuwa tukio fulani au jambo fulani linaishiaje au
nini hatima yake. Ni hali ya kutaka kujua nini kitakachofuatia au kitakachotokea
baada ya tukio fulani kuisha.Watunzi wengi wa kazi za kifasihi huunda kazi zao
kwa kuingiza matukio yanayopelekea taharuki kwa hadhira. Hii huongezea ari kwa
hadhira ya kutaka kujua ni nini kitakachofwatia mwishoni na kufwatilia kwa
umakini mkubwa kisa au hadithi nzima. Haya yamejidhihirisha katika utenzi huu
pale Malkia anataharuki ni nini kitakachofwatia baada ya kuona mwanae kaanza
kuota meno ya juu. Kwa mfano katika ukurasa wa 17 ubeti wa 153, 154 na 155.
Hivyo tendi nyingi za Kiswahili huusisha matumizi ya taharuki; hii huleta hamu
ya kuendelea kufwatilia hatima ya kisa fulani.
Matumizi ya Majigambo au Vivugo
Hizi
ni ghani za kujisifia. Kwa kawaida hutungwa na kughanwa na mhusika mwenyewe.
Kivugo hutungwa kwa ufundi mkubwa, kwa kutumia mbinu kama sitiari, vidokezi,
ishara, takiriri na wakati mwingine hata vina ( Mulokozi 1996:81). Mara nyingi
hufanywa na wanaume yakifungamana na tukio maalumu katika maisha yake, kwa
mfano kuingia vitani, kupambana na maadui kama vile wanyama wakali, kushinda
jambo na kadhalika. Kipengele hiki halikadhalika hakijaachwa nyuma kwani katika
tendi lazima pawepo na matukio mengi ya kishujaa waliyoyafanya watu na hivyo
hujigamba mbele za watu kudhihirisha ushujaa wao, kwa mfano katika ukurasa wa 6
ubeti wa 57 hadi wa 61, 68, 75, 76, 109,
386 hadi 390, na 639 hadi 641. Katika beti hizi zote mtunzi ameonesha majigambo
mbalimbali yaliyokua yanafanywa na wahusika, mfano ubeti wa 396 na 397 Nyakiiru
na Kanyamaishwa wanajigamba mbele ya Sultani.
396 “Ni vyema kuyasikia 397 “Nimezoea vita
Maneno ya
ushujaa Hupiga
bila kusita
Mimi pia
nakwambia Kazi
yangu ni kuteta
Si mzembe
kwa kuua. Mateto
nina yajua.
Hitimisho
No comments:
Post a Comment