Wednesday, November 25, 2015

PROFESA BAREGU AHOJI BUNGE KUCHANGIWA NA MAKAMPUNI, TAASISI ZA UMMA


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), Profesa Mwesiga Baregu amesema anatilia shaka hatua ya Taasisi muhimu kama Bunge kukusanya michango kutoka kwa Taasisi za umma ili kuendeshea shughuli zake, ikiwamo hafla ya uzinduzi wa Bunge mjini Dodoma.
Aidha, Profesa Baregu ameshangazwa na hatua ya Rais John Magufuli kupokea fedha hizo na kuzibariki kutumika katika kununulia vitanda katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili bila kuhoji malengo na msingi wa mhimili huo wa kutunga sheria kuchangiwa fedha hatua ambayo msomi huyo amedai kuwa ni kumwingiza Rais kwenye mtego wa ufisaji wa kimfumo.
“Bunge ni taasisi nyeti sana kuruhusu kuchangiwa pesa na watu au taasisi ambazo linapaswa kuzisimamia. Mara kadhaa wakuu wa mashirika haya hutakiwa kuhojiwa ikiwemo kuwasilisha matumizi yao mbele ya Kamati za Bunge; Je, kweli Bunge litakuwa na nguvu ya kuzisimamia endapo linapokea michango kutoka kwenye Taasisi hizo?” amehoji Profesa Baregu.
Profesa Baregu ameelezea kitendo cha Bunge kukusanya michango kwa ajili ya hafla kuwa ni ufisadi wa kimfumo ambao haustahili kuvumiliwa. Aidha msomi huyo amesema anategemea kuwa kwa umakini alionao Rais Magufuli hatalifimbia macho hili na atawataka Bunge wajieleze ni kwa namna gani wameingia kwenye ufisadi huu wa mfumo na ikiwezekana kuwachukulia hatua wote waliohusika.

No comments:

BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

 BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm

Logo

Logo Design by FlamingText.com