Tuesday, June 2, 2015

Kazi haramu 66,000 za wasanii zakamatwa

Wizi wa kazi za wasanii umetajwa kuwa bado ni tatizo katika nchi ya Tanzania suala ambalo linasababisha serikali kukosa mapato na kudidimiza ukuaji wa maisha ya wasanii nchini.
Wasanii wa Tasnia ya Filamu Tanzania JB na King Majuto
Hayo yameelezwa leo mjini Dodoma na naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janet Mbene wakati akijibu swali kutoka kwa Mbunge wa viti maalumu (CCM) mkoa wa Singida, Bi Martha Mlata ambaye alitaka kujua jitihada za serikali katika kutokomeza wizi wa kazi za wasanii na maslahi yao.
Ambapo akijibu swali hilo Mh Mbene amesema kuwa serikali mpaka sasa imeweka mkakati wa kuandaa muswaada ambao utasaidia kudhibiti wingi wa uingiaji na usambaaji wa kazi za muziki ambapo kupitia mpango wa serikali mpaka sasa wamefanikiwa kukamata CD NA DVD 30988 kwa kazi za ndani 35166 kwa kazi za nje.

Mh Mbene amesema kuwa kamati imeandaa mpango wa kuishirikisha TRA na KOSOTA kwenye mpango wa usambazaji na uuzaji wa kazi za wasanii unaofanywa na wasambazaji ili kudhibiti mapatoya serikali ukiwemo mpango wa utoaji wa semina elekezi kuhusu masuala ya ulinzi wa kazi za filamu na muziki nchini.
Hata hivyo amesema maandalizi ya kuanzisha sheria ya hati miliki bado yanaendelea kwa ushirikiano na waaigizaji mawakili stamp zilizotolewa na mamlaka ya mapato Tanzania TRA tangu urasimishaji wa kazi za sanaa ulipoanza ni milioni nne laki tano sabini kwa muziki na milioni 18 420000 kwa kazi za filamu
TAGS: EATV PAGE

No comments:

BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

 BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm

Logo

Logo Design by FlamingText.com