Tuesday, June 2, 2015

Milion 2 wapatiwa vitambulisho vya taifa

Mamlaka ya vitambulisho vya taifa nchini Tanzania NIDA imewahakikishia wananchi kuwa vitambulisho inavovitoa ni salama na haviwezi kughushiwa kwa namna yeyote.
Naibu waziri wa mambo ya ndani - Pereira Silima
Akizungumza kwenye kongamano la kimataifa la mamlaka ya vitambulisho vya taifa barani Afrika leo jijini Dar es salaam afisa habari wa NIDA Thomas William amesema kuwa Technolojia iliyotumika kwenye utengenezaji wa vitambulisho hivyo ni ya kisasa na inayotoa fursa ya vitambulisho hivyo kutumika kwa ajili ya huduma nyingine za kijamii.
William amesema mpaka sasa takribani watu mil 2 wamepatiwa vitambulisho nchini lengo likiwa ni kuwapatia watu mil 25 ambapo wamesema wengi waliopatiwa vitambulisho hivo ni wanafunzi wa elimu ya juu nchini ili kuondoa kero wakati wakuomba mikopo.
TAGS: EATV

No comments:

BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

 BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm

Logo

Logo Design by FlamingText.com