Friday, February 26, 2016

Makamba, Ndalichako, Mahiga, Kitwanga wapewa masaa



ambapo wamepewa muda mpaka saa 12 jioni wawe wamesharejesha fomu hizo
Mawaziri wanaotakiwa kurejesha fomu za tamko la rasilimali pamoja na hati ya ahadi ya uadilifu ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Charles Kitwanga na Waziri wa Nchi (OMR – Muungano na Mazingira), Bw. January Makamba. Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga ambaye anatakiwa kurejesha hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako ambaye anatakiwa kutoa tamko la rasilmali na madeni.
“Mheshimiwa Rais ameelekeza mawaziri ambao hawajajaza tamko la rasilmali au hati ya ahadi ya uadilifu wafanye hivyo na kuzirejesha kabla saa 12 jioni na Waziri ambaye atashindwa kutekeleza agizo hili atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake,” amesisitiza Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu amesema wakati akifungua mafunzo ya Mawaziri na Naibu Waziri kuhusu Mwongozo wa Maadili ya Viongozi wa Umma na Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu yaliyofanyika Ikulu jana (Alhamisi, Februari 25, 2016) alikabidhiwa majina ya Mawaziri na Naibu Mawaziri ambao hawajawasilisha Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Kamishna wa Maadili.


SOURCE EATV PAGE

Monday, February 22, 2016

Salamu zenu wadada wenye tabia hii

;
~Yaanike matiti yako kwenye mitandao wee,
yabane vizuri na vaa vinguo vya ajabu ili
yaonekane...
~Jaa kiburi wanavyokusifia wanaume wazinzi
kuwa wewe ni mzuri na umependeza...
~Vaa visiketi vyako vya kubana na kuacha
vimapaja vyako nje wanaume wasio na huruma
wakusifie kisha wakulaghai na kuzini na wewe...
~Zitoe mimba hizo wanazokupa endelea na huo
mchezo mpaka pale utakapoona kuua sio maagizo
ya Mungu na wakati huo umeshaua kizazi.
~Fanya vituko vyote mtaani na kwenye mitandao
ya kijamii si bado unalipa?! Kila picha inatoka
vizuri ukiipiga.
Ikifika muda wa kuolewa na wale waliokuwa
wanakuambia wewe ni mrembo baada ya
kuwaanikia matiti yako na mapaja yako hadharani
alafu hawakutaki tena Usianze kumlaumu Mungu
na kuwaambia watu wewe unamikosi na umelogwa
Na nyie wakaka mnaowakwa na maroho ya uzinzi
ndani yenu tembeeni wee na kila mdada
mnayemwona barabarani na mitandaoni maana
guest zipo nyingi tu na hayo mageto ya kupanga
yapo si wazazi wenu hawaoni mnafikiri na Mungu
hawaoni ila ikifika Muda wakuoa n mkao wa vimeo
msianze kukatisha watu tamaa, eti hakuna
mwanamke aliyetulia wa kuoa wote ni walewale
wakati wewe mwenyeweni afadhali ya walewale, kila
mdada ukimwona unatamani uujue utupu wake.
Cha kufanya; Mrudie Mungu sasa sio usubiri
yakufike shingoni na
shetani akutupe nje ya zizi ndio uanze kutafuta
kila mtumishi akuombee wakati unaharisha tumbo
lisiloisha.

 

Sunday, February 21, 2016

UCHAGUZI UGANDA>>>>DKT BESIGYE KASEMA HAYA

Mmoja wa wapinzani wakuu katika uchaguzi mkuu uliofanyika Alhamis wiki hii nchini Uganda, Dkt Kizza Besigye, amepinga matokeo ya uchaguzi huo.
Dkt. Besigye ambaye amekuwa akizuiliwa nyumbani kwake tangu siku ya Ijumaa amesema kuwa raia nchini Uganda wameshuhudia udanganyifu mkubwa katika uchaguzi huo, ambao haujahi kufanyika katika taifa hilo.
Kanali huyo mstaafu ameuelezea uchaguzi huo kuwa si halali na kuwa ni sawa na mapinduzi ya kijeshi.
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa jana, Rais wa muda mrefu wa taifa hilo Yoweri Kaguta Museveni, alitangazwa mshindi.
Rais Museveni ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka thelathini sasa, alipata zaidi ya asilimia 61 ya kura huku Besigye akijipatia asilimia 35 ya kura.
Waangalizi wa kimataifa wamesema kuwa uchaguzi huo uliandaliwa katika mazingara ya hofu na kudhalalishwa.

 SOURCE STAR TV

Friday, February 19, 2016

SHULE KUMI ZILIZOFANYA VIZURI KATIKA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2015>>


Baraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2015 yanayoonesha kiwango cha ufaulu kushuka kwa asilimia 0.80.

Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema kuwa jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka 2014 ambapo ufaulu ulikuwa 68.33%.

Msonde amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84) na wavulana wakiwa 124,871 (71.09).

BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

 BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm

Logo

Logo Design by FlamingText.com