Baraza
la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne
wa mwaka 2015 yanayoonesha kiwango cha ufaulu kushuka kwa asilimia 0.80.
Akitangaza
matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema
kuwa jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa wote
waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka
2014 ambapo ufaulu ulikuwa 68.33%.
Msonde
amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996 sawa
na asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84)
na wavulana wakiwa 124,871 (71.09).
Amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.85 ikilinganishwa na mwaka 2014.
Aidha
kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, Dkt Msonde amesema watahiniwa
31,951 sawa na asilimia 64.80 wamefaulu ikilinganishwa na watahiniwa
29,162 (61.12) waliofaulu mwaka 2014.
Kwa
upade wa ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa
wa shule, Msonde amesema waliopata daraja la kwanza ni 9,816 sawa na
asilimia 2.77, daraja la pili ni 31,986 sawa na asilimia 9.01, daraja la
tatu ni 48,127 sawa na asilimia 13.56.
Aidha
waliopata daraja la nne ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 na waliopata
daraja la sifuri (waliofeli) ni 113,489 sawa na asilimia 32.09.
Watahiniwa
waliopata ufaulu mzuri wa kati ya daraja la kwanza hadi la tatu ni
94,941 sawa na asilimia 24.73 wavulana wakiwa 56,603 sawa na 29.99 na
wasichana 38,338 sawa na asilimia 19.63.
SOURCE:::: RHEVANMEDIA.COM
No comments:
Post a Comment