Siku mbili baada ya sintofahamu ndani ya Ukawa baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa kujitokeza hadharani kumpinga mgombea wao Edward Lowassa, amekiri kuwa yeye ndiye aliyewasilisha wazo la kumpokea katiaka chama hicho.
Akiongea jana katika mahojiano maalum na Star TV, Dk. Slaa alieleza kuwa wazo alipokea kutoka kwa Askofu Josephat Gwajima wazo la kumkaribisha Edward Lowassa ndani ya Chadema na kumpa nafasi ya kugombea urais siku moja baada ya jina la mgombea huyo kukatwa na kamati ya maadili ya CCM katika mchakato wa kura za maoni.
Dk. Slaa ambaye alimuelezea Askofu Gwajima kama rafiki yake wa muda mrefu, alieleza kuwa baada ya kupokea wazo hilo kutoka kwa askofu huyo na baadae akalifikisha kwenye chama chake na kumueleza Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu.
“Nililipeleka wazo hilo la Mshenga Freeman Mbowe na alikuwa na Tundu Lissu,” alisema.
Alifafanua kuwa wakati anawasilisha wazo hilo, tayari Chadema walikuwa wamemchagua yeye kuwa mgombea urais na walikuwa wameshampeleka nje ya nchi kwa nia ya kujifunza zaidi.
Hata hivyo, hali inaonesha kuwa baada ya chama hicho kulifanyia kazi wazo hilo, Dk. Slaa aligeuka kuwa kikwazo kikubwa kwa kuweka masharti ambayo kwa mujibu wake hawakuyatimiza.
Dk. Slaa alitangaza kujiuzulu siasa za vyama vya siasa hivi karibuni kwa madai kuwa hakubaliani na uamuzi wa Chadema kumsimamisha Edward Lowassa kuwa mgombea urais kwa kuwa anatuhuma za sakata la Richmond.
SOURCE DAR24
No comments:
Post a Comment