AMA kweli Mbongo-Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Mama Kijacho, Zarinah Hassan ‘Zari
The Boss Lady’, sasa ni wa kimataifa zaidi ambapo wakati mwanamama huyo
akijiandaa kujifungua, tayari mtoto ajaye ameandaliwa chumba maalum cha
kulala na gharama za kumuona kwa atakayehitaji picha hasa za kwenye
vyombo vya habari, itakuwa si chini ya Sh. milioni 20.
Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Mama Kijacho, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
CHANZO KUTOKA WCB
Kwa mujibu wa chanzo
makini ambacho kipo ndani ya Wasafi Classic Baby (WBC), Diamond na Zari
wameamua kutenga chumba maalum cha mtoto wao atakapozaliwa.
Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa katika pozi na lafiki yake.
MASHARTI YA KUMWAGA
Ilidaiwa kwamba, chumba
hicho kitakuwa mahususi kwa mtoto tu na wala hakuna mtu mwingine atakaye
ruhusiwa kuingia kumuona bila malipo zaidi ya mama, baba na familia yao
ambao nao wataingia kwa sharti la kutopiga picha.
“Naona Zari anampeleka
Diamond kimataifa kila kukicha maana nimeshuhudia chumba kina ‘full’
mazagazaga ya mtoto na nilipouliza nikaambiwa hicho ni chumba cha mtoto
wa Zari mara tu atakapozaliwa.
“Wanasema mtoto atakuwa na chumba chake maalum na hataruhusiwa mtu mwingine kulala wala kumuona.
“Kwa watu wa media (vyombo vya habari) lazima watoe si chini ya milioni 20 kwa picha na interview (mahojiano) na Zari.
KAMA KANYE NA KIM
“Wameamua kufanya hivyo
ili kuendana na wasanii wengine wa Marekani kama Kanye West na Kim
Kardashian au Jay Z na Beyonce ambao wamekuwa wakifanya hivyo.
ULINZI USIPIME
“Nimeshuhudia hadi vitu
vya mtoto na kitanda chake tayari vimeshaandaliwa mara tu mtoto
atakapokuja atakuwa katika chumba hicho ambacho kipo ndani ya mjengo
wao, Madale (Tegeta, Dar). Unaambiwa ulinzi utakuwa mkali usipime.
“Wamejipanga mtu yeyote
asimuone mtoto huyo kuanzia siku anajifungua kwani wanategemea kuweka
ulinzi wa hali ya juu kuanzia hospitalini hivyo hata wanahabari
wakihitaji lolote juu ya mtoto huyo watatakiwa kulipa kiasi hicho cha
fedha,” kilitiririka chanzo hicho.
BABA KIJACHO ANASEMAJE?
Baada ya kunyetishiwa
mchongo huo, gazeti hili lilimtafuta Baba Kijacho, Diamond ili
kuthibitisha ishu hiyo ambapo alisema ni kweli wameshaandaa chumba
maalum kwa ajili yake, mara tu atakapozaliwa na kwamba haitaonekana sura
yake kwani kutakuwa na bei maalum kwa yoyote atakayehitaji kumuona.
“Yeah! Ni kweli kuna
chumba chake maalum na pia haitaonekana sura yake maana kutakuwa na bei
maalum kwa magazine au televisheni itakayohitaji kuwa na ‘exclusive’ ya
kuonesha sura yake kwa mara ya kwanza.
“Bei ya mtu kumuona au
kwa vyombo vya habari, hiyo itategemea na ukaribu wetu na chombo husika
kitakachokuwa kikihitaji kurusha habari ya mtoto wetu,” alisema Diamond
anayesumbua na kibao chake kipya cha Nana.
DIAMOND PRESHA TUPU
Diamond kwa sasa yupo
kwenye presha kubwa ya kuomba mashabiki wake wampigie kura kwa wingi
katika Tuzo za MTV (Mama’s) baada ya kuteuliwa kuwania Vipengele vya
Msanii Bora wa Kiume Afrika, Mtumbuizaji Bora wa Kiume Afrika na Nyimbo
Bora ya Kushirikiana Afrika.
ZARI ATAJIFUNGUA LINI?
Kwa upande wake, Zari anatarajiwa kujifungua mtoto wa kike kuanzia Agosti, mwaka huu na kuendelea.
No comments:
Post a Comment