DOKTA Chale ambaye
anaandika makala za afya katika gazeti ndugu la hili la Ijumaa,
ameanika chanzo cha mastaa wengi kupata ugumba ambapo pamoja na vyanzo
vingine, ameyataja madawa ya kuongeza maumbile ya mwili na ya kujichubua
yanasababisha tatizo hilo.
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Akizungumzia madawa hayo
pasipo kuyataja majina (yamezagaa mitaani), dokta Chale alisema baadhi
ya madawa hayo yana kemikali ambazo hupenya hadi kwenye figo na
kuzisababishia madhara ambapo moja kwa moja hawezi tena kupata mtoto.
Alisema amekuwa akisikia
kila kukicha katika vyombo vya habari mastaa wakijieleza kuwa
wamehangaika sana kupata watoto lakini imeshindikana pasipo kujua madawa
hayo ndiyo chanzo hivyo ni vyema wakachukua tahadhari.
“Kwa wale ambao bado
hawafikirii kuzaa ni vyema wakawa makini na madawa haya ya kuongeza
maumbo yao. Yanaathiri figo na zikishaathirika mwanamke hawezi tena
kupata ujauzito.
“Ni vyema wakawaona
madaktari kwa ajili ya ushauri kabla hawajaanza kuyatumia maana baadhi
ya dawa hizi zinaingizwa nchini bila kukaguliwa kama zinafaa kwa
matumizi ya binadamu,” alisema Dokta Chale.
Miongoni mwa mastaa
ambao wamesharipotiwa kuwa na tatizo la kukosa watoto kwa muda mrefu ni
pamoja na mbunge mtarajiwa, Wema Sepetu ‘Madam,’ Judith Wambura ‘Jide,’
Rehema Chalamila ‘Ray C’ (pichani), Mainda Suka, Jacqueline Wolper na
Jokate Mwegelo ‘Kidoti.’
SOURCE' KAHAMA_FM
No comments:
Post a Comment