Thursday, May 7, 2015

Jackie Chandiru avunja ndoa ya mtu


Siku chache tu baada ya msanii wa muziki Jackie Chandiru wa nchini Uganda kufunga ndoa na mumewe ambaye ni raia wa kigeni Van Vliet, imegundulika kuwa, mwanaume huyo tayari alikuwa na ndoa na mrembo Adut Mawien.
msanii wa muziki Uganda Jackie Chandiru akiwa na mumewe huku kulia mumewe akiwa na mrembo Adut Mawien
Taarifa hizi zimeibuka na kuwaacha midomo wazi mashabiki wa Jackie, hasa kutokana na kurasa za mitandao ya kijamii za mumewe huyo mpya, kuendelea kuwa na picha na kumbukumbu za Adut ambaye ni mwanamitindo kutoka Sudan Kusini ambaye mpaka sasa, hakuna kithibitisho kuwa waliachana.
Kuibuka kwa taarifa hizi, kunamrudisha Jackie katika historia ya kutoka na waume za watu, rekodi zikionesha kuwepo kwa ugomvi mkubwa kipindi cha nyuma kati yake na mke wa Caleb Alaka, mwanaume ambaye aliingia naye penzini licha ya kuwa ni mtu mwenye familia.

No comments:

BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

 BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm

Logo

Logo Design by FlamingText.com