Miezi
michache tu baada ya kumlaumu mamake mzazi kwa kumroga na kumfanya
apoteze fomu yake, Emmanuel Adebayor anayeichezea timu ya Tottenham
inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza, amejitokeza na kufichua
jinsi familia yake ilivyomfanya afilisike bila shukrani.
Kupitia ukurasa wake wa facebook, Adebayor ameeleza kuwa
"Nimekuwa
nikiziweka taarifa hizi kwa muda mrefu lakini leo nimehisi kuwa ni
muhimu kuwaeleza nanyi pia. Ni kweli kuwa masuala ya familia hayastahili
kuwekwa hadharani lakini nafanya hivi ili familia nyingine nazo zipate
funzo kupita yaliyonisibu, Aliandika.
Anasema wakati alipokuwa na
umri wa miaka 17, aliutumia mshahara wake wa kwanza kuijengea familia
yake nyumba.Kama mnavyojua nilipokea tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika wa
mwaka, mwaka 2008.
Nilimpandisha mama yangu jukwaani kumshukuru
yeye kwa mambo yote. Mwaka ule ule nilimleta London kwa ajili uchunguzi
wa afya yake.
Wakati binti yangu alipozaliwa niliwasiliana na mama yangu kumweleza lakini alikata simu na sikujua ni kwanini.
Ukisoma
maoni yangu ya hivi karibuni watu wanasema mimi na familia yangu twende
tupate ushauri kwa muhubiri maarufu wa dini ya kikristo T.B Joshua.
Emanuel Adebayor
Mwaka 2013 nilimpa mama yangu pesa ili aende kupata ushauri kwa mhubiri huyo nchini Nigeria.
Alipaswa
kukaa huko kwa wiki moja, lakini siku mbili tu alipofika nilipokea simu
kwamba ameondoka. Zaidi ya hayo nilimpa mama yangu pesa nyingi
kuanzisha biashara ya kupika chakula pamoja na bidhaa nyingine.
Kiuhalisia niliwaruhusu kuweka jina langu na picha yangu kwenye biashara hiyo ili waweze kuvutia wateja.
Ni kitu gani kingine mtoto wa kiume anaweza kufanya ndani ya uwezo wake kusaidia familia yake?
Miaka
kadhaa iliyopita, nilinunua nyumba huko East Lagon nchini Ghana kwa
dola milioni 1.2 za kimarekani. Nikaona ni vyema dada yangu mkubwa Yabo
Adebayor kuishi katika nyumba hiyo. Vile vile nilimruhusu kaka yangu
Daniel naye aishi kwenye nyumba hiyo.
Miezi michache baadae
nilifukuzwa kwenye nyumba niliyokuwa naishi ikianibidi kwenye hiyo
nyumba yangu. Kilichonishangaza niliona magari mengi kwenye barabara.
Kwa kweli dada yangu aliamua kuikodisha hiyo nyumba pasipo kunieleza.
Alimfukuza Daniel kwenye hiyo nyumba. Mfahamu
kwamba nyumba hiyo ina vyumba 15. Nilipompigia dada yangu anipe
ufafanuzi alichukua karibu nusu saa kunishambulia na kunitukana kwenye
simu. Nilimpigia mama yangu anaelezee kisa kizima naye akafanya kama
dada yangu alivyofanya. Hivyo ni kama dada yangu alivyosema sina
shukrani.
Kaka yangu Kola Adebayor, anaishi nchini Ujerumani kwa
miaka ishirini na mitano sasa,safari zake zote za kurejea nyumbani mara
nne ametumia gharama zangu,kama hiyo haitoshi ninawasomesha watoto wake
na kuwalipia gharama zote kuhusiana na elimu yao.
Nilipokuwa
nchini Monaco ,alinifuata na kutaka pesa za kuanzishia biashra yake
.Mungu pekee ndiye ajuaye nilimpa kiasi gani cha kufungulia biashara
yake,kama ukimuuliza biashara hiyo iko wapi leo?
Masahibu
hayakuishia hapo,kaka yetu Peter alipoaga dunia nilimtumia Kola kiasi
kikubwa cha pesa ili arejee nyumbani,cha kushangaza hakutokea msibani
ama siku ya maziko.na leo kaka yule yule (Kola) anawaambia watu kuwa
chanzo cha kifo cha kaka yetu Peter ni mimi,linawezekanaje hili? Kaka
huyu huyu alikwenda kwenye gazeti la"The Sun" na kueleza habari za uongo
kuhusiana na familia yetu ili kujipatia fedha.
Wakatuma barua pia
katika klabu ya mpira ya Madrid nikafukuzwa.nilipokuwa nchini humo pia
nilipata wazo kuwa ni vyema kuwa na familia ya wana soka,hivyo
nikahakikisha kaka yangu Rotimi anajiunga na chuo cha mafunzo ya mpira
huko Ufaransa. Miezi michache tu,wachezaji ishirini na saba wa chuo hiyo
aliwaibia simu za mkononi wachezaji ishirini na mmoja .Sikuongea
chochote kuhusiana na kaka Peter Adebayor ,kwasababu hayuko nasi leo
hii,Mungu ailaze mahala pema peponi ,amina.
Dada yangu sasa, Lucia
Adebayor amekuwa na tabia ya kuwaambia watu kuwa baba yetu amenitaka
nimchukue dada huyu na kumpeleka ulaya,lakini sababu kubwa hasa ni nini
ya kumpeleka huko ulaya? Kila aliyeko hapa yupo kwa sababu.
Nilirejea
nyumbani Ghana nilipata taarifa za kaka yangu anaumwa sana,niliendesha
gari kwa kasi sana kuelekea Togo ili kukutana naye na kumpa msaada
anaostahili,nilipowasili huko mama yangu akanikatalia kumwona na
kunieleza kuwa ninachopaswa kufanya ni kumpa mama yangu pesa nay eye ata
maliza kila kitu.
Mungu pekee ndiye ajuaye siku ile ile
nikampatia mama yangu kiasi cha pesa alichokitaka,lakini cha ajabu watu
wanalalama kuwa sikufanya lolote kuokoa maisha ya kaka yangu Peter.je
mimi ni mpumbavu kiasi gani niendeshe gari mpaka Togo bure bila ya
sababu?
Nikaandaa mkutano wa kifamilia mwaka 2005 ili tumalize
tofauti zetu na matatizo yanayotuzunguuka.nilipowauliza maoni yao
wakanitaka kuwajengea nyumba kila mmoja wao na mishahara mikubwa kila
mwezi kwa kila mmoja wao.
Leo hii niko hai wamejimilikisha kila
kilicho change je nikifa itakuwaje?kwa sababu zote hizi,itanichukua muda
mrefu mno kuweka mikakati na misingi yangu barani Africa.kila wakati
ninajitahidi kuwasaidia wahitaji,familia yangu wao huhoji kila
nifanyacho na wote huona nimefanya uamuzi mbaya.
Ikiwa leo
ninaandika haya,sina lengo la kuwaanika watu wa familia yangu.ninataka
familia zingine za kiafrika kujifunza kutokana na ninayoyapitia mimi.
Asanteni sana.
SOURCE www.bbc.com
No comments:
Post a Comment