Thursday, April 16, 2015

Wema: Kumuimba Msichana Uliyeachana Naye ni Ushamba


Wema: Kumuimba Msichana Uliyeachana Naye ni Ushamba
Staa Mrembo Kutoka Bongo Movies, Wema Sepetu ‘Madam’, amesema ni ushamba kwa wasanii wa muziki kuwatungia nyimbo za majungu wasichana wanaoachana nao kimapenzi.

Wema amesema wasanii wengi wa muziki wamekuwa na tabia ya kishamba ya kutunga nyimbo zenye maneno ya kuudhi, wakiwalenga waliokuwa wapenzi wao.
“Ni ushamba wa mapenzi, haiwezekani mlikuwa mnafurahia wote mapenzi yenu, lakini mkiachana anakutungia nyimbo za kukuponda, hakuna neno la kuzungumzia hilo zaidi ya kuita ushamba kwa wasanii wa aina hiyo,’’ alisema Wema.
Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti la Mtanzania kutoka studio moja kubwa ya kurekodi muziki nchini, kuna wimbo wa wasanii wawili waliowahi kuimba pamoja na wimbo wao ukawa gumzo kwa mashabiki wa muziki huo, ambao wanamalizia kurekodi wimbo unaodaiwa unamzungumzia  mrembo huyo.
16.04.2015 -  Tags:  WEMA 

No comments:

BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

 BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm

Logo

Logo Design by FlamingText.com