Raia wa Tanzania wanaoishi Afrika Kusini sasa wanadaiwa kushika silaha
tayari kwa mapambo dhidi ya vikundi vya raia wa Taifa hilo
vinavyoshambulia wahamiaji wa Kiafrika.
Taarifa kutoka kwa Watanzania hao zimeeleza hatua hiyo imefikiwa baada
ya kupatikana kwa taarifa zinazodai kuwa wenzao wawili wameuawa katika
machafuko ya jiji la Durban ambayo chanzo chake ni mashambulizi
yanayofanywa na raia wan chi hiyo dhidi ya wageni.
Mmoja wa Watanzania anayeishi Cape Town Pius Mbawala alieleza kuwa
taarifa za mauaji ya wenzao zimewasikitisha sana na kwamba hadi sasa
hakuna kiongozi yoyote wa ubalozi wa Tanzania aliyewasiliama nao ili
kujua hali za usalama wao tofauti na balozi za nchi nyingine.
Mbalawa alisema kwa muda mrefu sasa maofisa wa ubalozi wa Tanzania
nchini humo wamekuwa na uhusiano wenye shaka na Watanzania walioko huko
tofauti na wanavyopaswa kujua ukazi wao kwenye Taifa hilo.
Alisema Raia wa Tanzania wanaoishi nchini humo wamejiunga katika makundi
madogo madogo kulingana na maeneo wanayoishi kwa ajili ya kujilinda
wenyewe na kila kundi hivi sasa limejihami kwa silaha.
SOURCE--- DUNIA KIGANJANI BLOG
No comments:
Post a Comment