Tuesday, April 21, 2015

Hakuna mtanzania alieuawa vurugu za A.Kusini-Membe


 Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe amesema mpaka sasa hakuna mtanzania aliyefariki kutokana na vurugu wanazofanyiwa raia wa kigeni nchini Afrika Kusini.
 


 Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, waziri Membe amesema Tanzania imesikitishwa na vurugu hizo ambazo zimeathiri maisha ya takribani watanzania 23 ambapo 22 kati yao serikali imepanga kuwarudisha nyumbani muda wowote kuanzia sasa.
Aidha waziri Membe amekiri taarifa za kuwepo kwa watanzania watatu waliofariki nchini humo ingawa amesema vifo vyao havitokani na vurugu hizo kwani kila mmoja amekufa kwa sababu yake ikiwemo uhalifu, kupigwa gerezani pamoja na kuugua.
Mh. Membe amewataka watanzania waishio nje ya nchi kujiandikisha kwenye balozi za Tanzania kwani kwa kufanya hivyo itasaidia sana serikali kutatua matatizo yao kwa njia rahisi pindi yawatokeapo.
Wakati huohuo mh.Membe amevitaka vyuo na mashule nchini kutoa elimu itakayowawezesha vijana na jamii kujiajiri pindi wamalizapo elimu zao kwani vurugu nyingi husababishwa na ukosefu wa ajira.

SOURCE:   EATV

No comments:

BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

 BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm

Logo

Logo Design by FlamingText.com