Fonolojia
ni tawi la isimu linalojishughulisha na kuchunguza mifumo ya lugha mbalimbali
za binadamu. Fonolojia hujihusisha au hujishughulisha na jinsi sauti za lugha
zinavyotumika katika kujenga maneno ambayo huwakilisha maana.
Michakato
ya kifonolojia ni mabadiliko ya kifonolojia yatokanayo na kubadili maumbo ya
kifonolojia na kuwa ya kifonetiki. Mfano katika lugha ya Kingereza
/spin/→[spin] “zunguka ukiwa sehemu ileile. Kupitia misingi ya fonolojia kuna
michakato na sheria zinazohusu fonolojia; ifuatayo ni michakato ya kifonolojia
inayojidhihirisha katika taaluma ya kifonolojia
.
.
Michakato
ya udondoshaji wa vitamkwa, kupitia hatua hii ya udondoshaji wa vitamkwa
hutokea pale ambapo maumbo mawili yakiwa yamegotanishwa irabu ya mwisho ya umbo
la kwanza inadondoshwa na toni pia hubadilika. Mfano katika lugha ya Ci-Ruuri kuna
omwaa’na + omujomu→omwa’a’mujomu
mototo mzuri motto mzuri
michakato
ya ubadilishaji wa maumbo ya kifonolojia kuwa ya kifonetiki, kupitia mchakato
huu wa ubadilishaji wa maumbo hayo tunapata maumbo ya kifonetiki ambayo huwa na
kitamkwa ambacho kinaangaliwa kiupekee. Mfano /pin/ huu ni uwakilishi wa
kifonolojia na kifonetiki ambapo tunapata umbo la [ph in] ambapo sauti huwa na mpumuo mkubwa.
Mchakato
wa uchopekaji wa vitamkwa, hapa tunapata hili katika lugha ya Kihispania ambayo
huchopekwa kitamkwa [∑] kabla ya konsonanti ya mwanzo wa neon katika mfuatano
wa #K.
Vilevile
zipo sheria mbalimbali zinazotumika katika fonolojia ili kupata maumbo
mbalimbali katika fonolojia. Sheria hizo ni kama zifuatazo;
Sheria
za kifonolojia zaweza kuwa za lazima au za hiyari, sheria za hiyari ni zile
ambazo zinaonyesha kwamba kuna uwezekano wa maumbo yanayohusika kutamka
vinginevyo yaani kila mmoja ya maumbo ya nje na ya umbo la ndani hubadilika. Mfano katika
Kiswahili umbo la ndani la neon miaka ni /mi + aka/ lakini umbo la nje la neon
hili hutamkwa [mya:ka]
Sheria
ya lazima ni sheria ambayo haina budi kutumika iwapo tunataka kupata umbo
linalokubalika. Mfano wa umbo la /vi+ungu/ [vyungu].
Sheria
za kifonolojia huweza kujenga tabdili, katika sheria hii kwa mfano ukiwa na
mwandamo wa X,Y,Z inawezekana baadhi ya lugha kubadili nafasi za sauti kuwa na
YXZ au XZY.
Sheria
za kifonolojia zinaweza kuunga vitamkwa muungano wa irabu mbili huungana na
kuzaa irabu moja lakini irabu inayozaliwa haifanani na irabu yoyote kati ya
hizo zilizoungana. Kenstowiics na kisseberth (1979:374) wanaita irabu hiyo
irabu fidi.
Kutokana
na sheria za kfonolojia ni dhahiri kuwa fonetiki na fonolojia kama matawi ya
isimu ya lugha ambayo misingi yake hutegemeana na yanavyohusiana. Vilevile
fonetiki na fonolojia huwa na misingi yake, ambapo msingi wa fonolojia ni
upambanuzi na uchanganuzi wa kitamkwa kama kipengele knchofanya kazi tofauti na
kingine katika mfumo wa lugha mahususi ambapo msingi wa fonetiki ni namna sauti
ilivyojengeka katika lugha husika.
Sheria
inayohusu utamkaji wa irabu juu inayotamkiwa nyuma hubadilika kuwa kiyeyusho
kinachoendandana nayo iwapo mbele yake kutakuwa na irabu ya chini inyotokea mara
tu baada ya mpaka wa mofimu.
MAREJEO.
D.P.B Massamba (2012), misingi ya fonolojia, Taasisi
ya Taaluma ya Kiswahili, Chuo Kikuu Dar-es-salaam.
No comments:
Post a Comment