OR-TAMISEMI inatangaza majina ya
wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya Pili
(Second Selection) kwa mwaka 2016. Jumla ya wanafunzi 3,918 wakiwemo
wasichana 2,413 na wavulana 1,505 wamechaguliwa kujiunga na Kidato
cha Tano awamu ya pili kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na
wanafunzi ambao hawakuripoti awamu ya kwanza.
Kati
ya wanafunzi waliochaguliwa 1,864 wakiwemo wasichana 1,099 na wavulana
765 sawa na asilimia 47.58 watajiunga na masomo ya Sayansi na
Hisabati; na wanafunzi 2,054 wakiwemo wasichana 1,314 na wavulana 740
sawa na asilimia 52.42 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na
Biashara.
Wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2015 wanatakiwa kuripoti
katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa
kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili atakuwa
amepoteza nafasi hii.
Orodha ya
wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka
2016 inapatikana kwenye tovuti ya OR-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
Imetolewa na Katibu Mkuu, OR-TAMISEMI
BOFYA LINK HAPA KUYAPATA http://tamisemi.go.tz/form_five_selection/second/
No comments:
Post a Comment