OR-TAMISEMI inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga
na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2016. Wanafunzi
waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali. Jumla
ya wanafunzi 65,720 wakiwemo wasichana 29,457 na wavulana 36,263
wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi. Kati ya
wanafunzi waliochaguliwa 34,064 wakiwemo wasichana 13,466 na wavulana
20,598 sawa na asilimia 52 watajiunga na masomo ya Sayansi na
Hisabati; na wanafunzi 30,897 wakiwemo wasichana 15,445 na wavulana
15,452 sawa na asilimia 47 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na
Biashara na wanafunzi 759 wakiwemo wasichana 220 na wavulana 539 sawa na
asilimia 1 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Ufundi.
Wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2016 wataanza muhula wa
kwanza tarehe 11 Julai, 2016 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya
shule. Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa
wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 24 ambayo
ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi
mwingine aliyekosa nafasi.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi mwaka 2016 pamoja na fomu
za kujiunga (joining instructions) inapatikana kwenye tovuti ya
OR-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
Imetolewa na Katibu Mkuu,
OR-TAMISEMI
Tumia link hii kupata matokeo http://tamisemi.go.tz/form_five_selection/
No comments:
Post a Comment