Thursday, December 10, 2015

JE, WALIONAJE BARAZA LA MAWAZIRI HAPA TANZANIA BAADA YA RAIS DR. MAGUFULI KULITANGAZA?

Rais John Pombe Magufuli ametangaza baraza lake la mawaziri muda huu, amesema Wizara nyingi wameunganisha na atakuwa na wizara 18, na watakuwa na mawaziri 19 tu, na baadhi ya wizara zitakuwa na Manaibu waziri huku zingine hazitakuwa na manaibu waziri hao.
Magufuli: Baraza nitakalolichagua halitakuwa na semina elekezi, kama ni semina watajipa huko huko ndani, wenyewe.
WIZARA MBALIMBALI ALIZOTANGAZA NA MAWAZIRI WAKE
Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora - Simbachawene na Angela Kairuki"
Wizara ya ofisi ya Rais, Utumishi na utawala bora ina mawaziri wawili ambao ni Mh. Simbachawene na Kairuki
Ofisi ya waziri Mkuu,Sera,Bunge,Kazi,vijana,ajira na walemavu,Waziri Jenista Mhagama,Naibu waziri Dk.Possy Abdallah.
Wizara ya Mambo ya Nje na EAC/ Kimataifa - Augustino Mahiga, Naibu Waziri - Dk. Suzan Kolimba
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi, Waziri wake ni Wiliam Lukuvi na Naibu wake ni Angelina Mabula
Wizara ya Elimu Waziri bado hajapatikana, Naibu Stella Manyanya
Waziri wa Afya jinsia na watoto: Ummy Mwalimu, Naibu wake Kigwangalla
Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi. Waziri: Mwigulu Nchemba Naibu Waziri: William Tate Ole Nashon
Wizara ya ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano,Waziri bado hajapatikana,Naibu waziri Eng.Edwin Amandus Ngonyani.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na michezo, Nape Nnauye
Waziri wa Fedha na Mipango Waziri bado hajapatikana, Naibu Waziri wake ni Dk. Ashantu Kijachi.
Ofisi ya Makamu wa Rais/Muungano na Mazingira,Waziri January Makamba,Naibu waziri Luhaga Mpina.
Wizara ya Nishati na Madini Waziri ni Sospeter Muhongo na Naibu Waziri wake ni Medard Kalemani.
Wizara ya Katiba na Sheria Waziri ni Harrison Mwakyembe
Wizara ya Mambo ya Nje,Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Waziri ni Augustine Mahiga N/Waziri Susan Kolimba
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Waziri ni Husein Mwinyi
Wizara ya Mambo ya Ndani, Waziri ni Charles Kitwanga.
Wizara ya Sayansi, Teknolojia, Elimu na Ufundi Waziri bado hajapatikana na Naibu Waziri wake ni Stela Manyanya.
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Waziri wake ni Charles Mwijage

No comments:

BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

 BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm

Logo

Logo Design by FlamingText.com