Wednesday, September 9, 2015

ASKOFU GWAJIMA AMJIBU SLAA, ASEMA YEYE NA MAASKOFU HAWAJAPEWA RUSHWA ( SOMA ALIYONGEA LIVE JANA)


Askofu Gwajima ametisha mkutano wa waandishi wa habari mchana wa leo na kujibu tuhuma za yeye kuwa mshenga, alizotuhumiwa na Dr. Slaa
Tunakujuza yale aliyeongea mchana huu na waandishi wa habari kutoka hotel ya Landmark iliyopo Ubungo jijini Dar es salaam.
Gwajima: Kuwa hapa kimsingi ni kutolea ufafanuzi maneno yaliyotolewa na rafiki yangu Dr. Slaa katika hotel ya Serena.
Gwajima: Slaa alisema maneno mengi ila yaliyonigusa ni kusema kwamba Askofu Gwajima alinambia Maaskofu 30 wa RC wamehongwa.
Gwajima: Maneno haya ndio yalinigusa sana kwasababu mimi ni Askofu na hawa waliosemwa ni Maaskofu.
Gwajima: Katika maneno yake alikuwa akinitaja mimi kama rafiki yake, na mimi siwezi kumkana rafiki, ukweli ni rafiki yangu.
Gwajima: Ni rafiki yangu aliyekosea na kwaajili ya kukosea kule ni vizuri nianze urafiki wetu mimi na yeye unaanzia wapi.
Gwajima: Urafiki wangu mimi na Slaa ulianza wakati ule akiwa katika harakati za ukombozi, akitafuta ukombozi wa Watanzania.
Gwajima: Wakati ule wa ukombozi alipata matishio mengi ya kukamatwa, kuuwawa, akaniomba mimi nimsaidie kumpa watu salama
Gwajima: Kwahiyo nikampa walinzi, nikampa mtu anaitwa Edwin, Six, Colonel na mtu mwingine anaitwa ili kumsaidia kumlinda

Gwajima: Nikampa walinzi waliokuwa loyal kwangu, wanaaminika kwangu na waliokuwa wananilinda mimi.
Gwajima: Walinzi hao niliompa wakalinda nyumbani kwake kwa miaka mitano iliyopita.
Gwajima: Nimetanguliza hayo ili ufahamu ninayoongea ninayajua toka kwa jikoni kwa Slaa, chumbani, nitayoongea ni ya uhakika
Gwajima: Nimekupa utangulizi huo ili uone credibility yangu kumuongelea Dr. Slaa kwamba ninamjua na urafiki wetu.
Gwajima: Lakini nalazimika kusema Dr Slaa amekuwa muongo, nasikitika kusema hivyo kwa mtu niliyekuwa nampenda na kumheshimu
Gwajima: Hebu nikuoneshe matukio ya uongo ya Dr. Slaa.
Gwajima: Tukio la kwanza la uongo ni kwamba Dr. Slaa alisema amehama CHADEMA kwaajili ya ujio wa Lowassa, lakini si kweli.
Gwajima: Huo ni uongo wa mchana saa 8, na sishangai uongo huo kutajwa na Padri aliyekimbia utumishi wa Mungu.
Gwajima: Mwigulu Nchemba alisema mtumishi wa Mungu akimuacha Mungu basi mapepo yatamuingia kichwani mara 7 zaidi
Gwajima: Kwahiyo basi bila shaka sasa mapepo hayo ndiyo yamemuingia Dr. Slaa kichwani mara 7 zaidi.
Gwajima: Si kweli kuwa Slaa alihama CHADEMA kwasababu ya ujio wa Lowassa kwakuwa ujio wa Lowassa CHADEMA ulianza na Slaa
Gwajima: Dr Slaa alikuja kwangu kuniomba nimsaidie namna yoyote kumpata Lowassa, maana tukimpata huyo tutashinda uchaguzi
Gwajima: Nikaanza kumsaidia Dr. Slaa, nikafanya kila linalowezekana ili Mh. Lowassa atue CHADEMA.
Gwajima: Nataka nikiri kwamba kwenye lile aliloniita mshenga alikosea jina tu, ila alipatia kwakuwa mshenga anajua yote.
Gwajima: Mimi kusaidia kumleta Lowassa CHADEMA ni kazi ya Mungu, Biblia inasema "Heri wapatinishi wataitwa wana wa Mungu"
Gwajima: Kwa desturi wanasiasa huwa hawaelewani, hadi wapate mtu wa kuwaleta pamoja maana muda wowote wanaweza kugeukana.
Gwajima: Nilisimama katikati kwakuwa nilikuwa mtu sahihi kwa wakati ule, kuwaleta wanasiasa hawa pamoja, kukomboa Taifa letu.
Gwajima: Mimi nikawakutanisha pamoja Slaa na Lowassa, ikafika siku Dr Slaa mwenyewe akaniita twende tukamuone Mwenyekiti
Gwajima: Tukaenda kuonana na Mwenyekiti, kukawa na maongezi ya muda mrefu sana, baadaye wakakubaliana vizuri.
Gwajima: Nataka niongee kwenye platform ya mtumishi wa Mungu maana wanasiasa wanaweza kudanganya.
Gwajima: Niliwaomba watu wa CHADEMA kwamba mimi siko kamati kuu ila waniruhusu niingie nihakikishe Lowassa amefika salama
Gwajima: Siku zote wanaogombea vyeo huanzia kwa waganga lakini ni jambo zuri kama mtu ameanzia kwenye nyumba za ibada
Gwajima: Mtu hatakiwi aone kama jambo hili ni baya, ni zuri sana, baadala ya kuanzia kwa waganga ameanzia nyumba za ibada
Gwajima: Mtu huyu ameanzia nyumba za ibada, ndio maana baraka zinamfata kila anakokwenda.
Gwajima: Usiku ule Lowassa akaingia kamati kuu na mimi nikiwemo kamati kuu kuhakikisha kama amefika salama .
Gwajima: Lowassa akapokelewa pale nje ya ukumbi na Dr Slaa, Mwenyekiti wa chama, Prf Baregu na wengineo, na akaingia ndani
Gwajima: Lowassa akaongea, akahutubia, wote wakasimama kwa pamoja wakapiga makofi wakakubali wakampokea
Gwajima: Basi mimi nikafurahi nimeimaliza kazi ya kuwa mpatanishi ya watu ambao kwa 'nature' ya kawaida wasingeelewana.
Gwajima: Dr Slaa anatoka kwenye mkutano mkuu CHADEMA, mkewe akamtupia mizigo nje, kwakuwa hataki kuacha 'ufirst lady'
Gwajima: Mimi asubuhi nikafika nikamkuta Slaa amenyong'onyea sana, nikampa pole ila sikumwambia kuwa nimeambiwa umefukuzwa
Gwajima:Slaa akasema jana usiku nimekutumia meseji kuwa nimejitoa kwenye siasa kuanzia leo kwakuwa familia yangu inavunjika
Gwajima: "Nataka niwaoneshe meseji aliyonitumia Slaa" Askofu Gwajima anaonesha waandishi meseji aliyotumiwa usiku saa 7:19
Gwajima: Nataka Dr. Slaa kama anakana atoke hapa aseme kama sio meseji yake halafu aone mambo ya mshenga yatakavyoendelea.
Gwajima: Akanambia nimekutumia meseji kwamba mke wangu wangu amekataa. Nataka kukuonesha kuwa sio Dr. Slaa mnayemjua.
Gwajima: Ndio maana watanzania wote mnashangaa kwamba Dr. Slaa anaweza kufanya mambo haya, sio yeye nini ni mama, hataki.
Gwajima: Nakuonesha tu kwamba ni muongo Dr. Slaa kusema amehama CHADEMA kwaajili ya ufisadi wa Lowassa, NO ni uongo.
Gwajima: Nikamuona amechoka sana na nikawa naelewa mama amekataa, nikampa moyo kuwa nitamfuta mke wake niongee naye
Gwajima: Mwanamke ambaye ana hali hii sasa ndio anayemuongoza mume wake, kama ingetokea kuingia Ikulu, Ikulu pangekalika?
Gwajima: Mwanamke ambaye anamuambia mumewe hutoki ndani. Kwahiyo Dr. Slaa si yeye kuna tatizo linatokea hapo.
Gwajima: Dr. Slaa alisema watu kwenye mkutano wa CHADEMA waliletwa na malori. Nataka mmupime nyie kama ni Mkweli au Muongo.
Gwajima: Huyu mtu anayesema uongo wa mchana mchana hivi, anasema sasa Gwajima alinambia maaskofu wa katoliki wamepewa hela
Gwajima: Katoliki ni kanisa credible kuliko makanisa mengi duniani, kanisa katoliki ndio mama mlezi wa imani ya kikristo.
Gwajima: Maaskofu wa kanisa katoliki wana credibility, sasa kitu gani kinafanya Dr. Slaa awazushie maaskofu hawa.
Gwajima: Lengo kuu kubwa la Dr. Slaa ni kuondoa credibility ya maaskofu ili hawa maaskofu wasiaminike na waumini wao.
Gwajima: Maaskofu hawa wamemsomesha, sasa leo maaskofu 30 wa katoliki anawasingizia kuwa wamepewa rushwa na Lowassa.
Gwajima: Kwa unayemjua Slaa kama mkweli unaweza kuamini ni kweli, lakini nimekuonesha yanayofanya asiseme kweli kwa sasa.
Gwajima: Dr. Slaa wa leo sio Dr Slaa wa mwaka mmoja uliopita, we are talking about a different story
Gwajima: Anatukana Maaskofu wa Protestant, Maaskofu wa katoliki na sisi wapentekoste anatutukana. Nani anamtuma Dr Slaa?
Gwajima: Jiulize Askofu huyu unayemtukana naye ni mpiga kura, unapofika wakati wa kupiga kura akupigiye kura wewe?
Gwajima: It's a simpe reason kuwa kuna mtu aliye nyuma anayemtuma akawatukane hawa.
Gwajima: Maaskofu hawa wanaotukanwa na waumini wao wanasikia maaskofu wametukanwa, watampa kura huyu aliyewatuma atukane?
Gwajima: Mimi naomba watafakari kwa namna ya upya strategy hiyo imeshashindwa wajipange kwa namna ya upya,hii imeshindikana
Gwajima: Kama nilivyosema hiyo ndio ilikuwa risasi ya mwisho ndani ya bunduki yao.
Gwajima: Bahati mbaya ile silaha waliyotumia imepeleka mbele halafu ikamkosa mtu, nyuma ikatema moto halafu ukawaunguza wao
Gwajima: Sasa mimi nasema Maskofu wa katoliki hawakupewa rushwa, wala KKKT hawakupewa rushwa, wala mimi sijapewa rushwa.
Gwajima: Akasema walikuwa wanazunguka nae kwenye ndege. Mimi nina ndege yangu na hakuna sheria inayozuia mimi kubeba yoyote
Gwajima: Kama mnatukana Maaskofu, yule mnayetaka ashinde naye ataonekana anatukana Maaskofu, mnaharibia
Gwajima: Kama Dr. Slaa atakuwa amenijibu, nitasema alipokwenda Afrika kusini na aliokutana nao na mizigo iliyopatikana
Gwajima: Shujaa yoyote duniani ni yule anayeweza kufa kwa anachokiamini,nilikuwa ICU pia kwakuwa nilisimamia nilichokiamini
Gwajima: Mtapomuongoza tena atukane Maaskofu, Maimamu, Masheikh, nitalipua bomu na moshi utatoka na macho hamtofungua tena
Gwajima: Dr. Slaa alisema Maaskofu tutubu eti yeye ni muadilifu kuliko sisi, mimi najiuliza yeye ni mtakatifu kuliko sisi?
Gwajima: Dr. Slaa jiulize utakatifu wako, ulikuwa padre, ukaacha wito. Kuacha wito pekee yake tayari ni tatizo
Gwajima: Kitendo cha kuacha wito tu inatakiwa utubu,lakini zaidi ya hapo ukaoa.
Gwajima: Nitaporudi tena kama akiongea, nitaleta watoto aliowazaa ,aliwazaa tarehe ngapi na uhusiano wake wa kuacha upadre.
Gwajima: Hiyo ya watoto sitoleta leo, namsubiri atoke kwenye pango aseme, namsubiri.
Gwajima: Hayo ya kuoa simlaumu lakini akaamua kuacha mke na watoto na kuwatelekeza, akaenda kuoa mke wa mtu mwingine tena
Gwajima: Halafu anawaambia Maaskofu watubu, ni kosa hilo Dr. Slaa.
Gwajima: Mama Rose Kamili akaenda kuweka zuio mahakamani, kwahiyo hadi sasa Josephine na Dr. Slaa haipo ndoa.
Gwajima: Hebu waza kwamba mtu ambaye hamjafunga ndoa ana uwezo wa kukuzuia usiingie CHADEMA, mkifunga ndoa itakuwaje?
Gwajima: Nataka nihitimishe, anayemuongoza Dr. Slaa akome tena akome kabisa.
Gwajima: Nashukuru wanahabari, nawashukuru Maaskofu, watu na matukio watapita ila Tanzania itabaki. Mungu ibariki Tanzania
SOURCE EATV

No comments:

BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

 BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm

Logo

Logo Design by FlamingText.com