Monday, July 6, 2015

Viongozi wajadili mzozo wa Burundi

Ghasia zimesababisha maelfu ya watu kuitoroka nchi hiyo
Ni mkutano wa tatu wa dharura kujadili mzozo na mkwamo wa kisiasa nchini Burundi uliosababisha maelfu ya raia kuitoroka nchi hiyo.
Viongozi hao wakiwemo mwenyekiti na mwenyeji wa jumuiya, rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, na Yoweri Museveni wa Uganda, ambao tayari wamewasili kwenye kikao hicho, wanajadili na kuwasilisha mapendekezo ya ripoti mbili kuhusu mgogoro wa Burundi.

Ripoti hizo ni pamoja na ya kikosi cha pamoja cha kimataifa cha Usuluhishi wa mgogoro wa Burundi, kinachojumuisha, Umoja wa Afrika, na Umoja wa mataifa, jumuiya hiyo ya Afrika mashariki, pamoja na kikosi cha kimataifa kuhusu eneo la maziwa makuu. Pamoja na ripoti ya baraza la mawaziri wa Afrika Mashariki.
nullRais Nkuruzinza anawakilishwa na mawaziri wake
Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza hatohudhuria mkutano huo wakati akisubiria matokeo ya uchaguzi wa ubunge uliofanyika tarehe 29 Juni na badala yake amewakilishwa na mawaziri wa mambo ya nje na wa mambo na ndani pamoja na waziri wa Afrika mashariki na msemaji wa rais.
Viongozi wa Rwanda na Kenya pia hawahudhurii kikao hicho, badala yake wanawakilishwa na mawaziri wa mambo ya nje.

Source BBC

No comments:

BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

 BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm

Logo

Logo Design by FlamingText.com