Thursday, July 2, 2015

YALIYOJILI KATIKA BUNGE LA TANZANIA LEO........ KIKAO KILIAHIRISHWA MARA MOJA BAADA YA WABUNGE WA UPINZANI KUTOKA NJE......BUNGE - TBC | JULY.02.2015

Kwa kile wanachokiita wanaburuzwa, Wabunge wa UKAWA kwa pamoja wamegoma kuendelea na bunge na wote kuamua kusimama baada ya kupinga uwasilishaji wa dharula wa Miswada mitatu muhimu ya Gesi, Petroli na Uziduaji "Extractive Industries".

Ni baada ya John Mnyika kuomba Muongozo juu ya uvunjaji wa kanuni za bunge. shuguli za leo zimekiuka kanuni kwani miswada imewekwa ikiwa sambamba. anasema hoja ikishatolewa ni lazima ijadiliwe iamuliwe ndo itolewe hoja nyingine, lakini leo zipo hoja tatu kwa pamoja.

Mnyika kasema na huu Muongozo sitaki useme utautolea ufafanuzi siku nyingine kwa maana hatuwezi kuendelea kufanya kazi ambazo zimevunja kanuni.

Wanapinga kuwasilishwa kwa dharula na kwa pamoja
Miswada yenye manufaa makubwa kwa nchi.

Miswada wanayo pinga na iliyo wasilishwa kwa pamoja ni;

1.Muswada juu ya Petroli, 2015 (The Petroleum Act, 2015):

2.Muswada juu ya Usimamizi wa Mafuta na Gesi, 2015 (The Oil and Gas Revenues Management Act, 2015):

3.Muswada juu ya tasnia ya Uziduaji Tanzania (The Tanzania Extractive Industries Act, 2015): The Tanzania Extractive Industries Act, 2015.

Hata baada ya Spika kuwataka watoke nje kama hawataki kuendelea, Wamegoma na kusimama na kuanza kupiga kelele hadi Spika akaahirisha bunge. UKAWA wamesema mwanaharamu hapiti leo.

Bonyeza HAPA kusikiliza kilichoendelea bungeni.

No comments:

BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

 BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm

Logo

Logo Design by FlamingText.com