HII ni dunia ya mambo
mengi! Mkazi wa Kigogo -Luhanga jijini Dar, aliyefahamika kwa jina la
baba Juma, Jumamosi iliyopita alijikuta akitimuliwa ukweni sanjari na
mkewe, Mwanahamisi Njama kwa madai amekuwa akishindwa kutoa ushirikiano
wakati wa kuchangia chakula kwenye familia ya mkewe.
Katika sakata hilo, baba
Juma inasemekana amekuwa akiishi ukweni hapo ambapo masuala ya msosi
wanachangia kwa zamu na familia nzima kila mmoja na siku yake.Kwa mujibu
wa chanzo chetu, zamu ya wanafamilia wengine ikifika hununua chakula
chenye mvuto kinywani, kama samaki wa Mwanza (sangara, sato) na
mapochopocho mengine lakini zamu ya Mwanahamisi, mumewe hutoa pesa ya
matembele jambo linalodaiwa lilikuwa likiwakera wanafamilia hao.
Kufuatia kero hiyo, kwa
mujibu wa chanzo, wanafamilia hao inadaiwa waliamua kumvalia njuga baba
Juma na kumtimua yeye na mkewe na mtoto wao Juma mwenye miaka miwili.
Ni wakati mtafaruku huo
wa ‘aondoke huyo’ ukiwa umepamba moto, chanzo chetu hicho kilipiga simu
Ofisi za Global Publishers, Kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ na
kupasha mchezo kamili na akusema kuwa timbwili hilo lilikuwa
likiendelea ‘laivu’....Bila kuchelewa, mmoja wa makachero wa OFM kwa
kutumia pikipiki iendayo kasi, ndani ya dakika chache alifika eneo la
tukio na kukuta baadhi ya wanafamilia hao wakiendelea kuwafanyia
timbwili Mwanahamisi na mumewe ikiwemo kuwapa vichapo huku wasamaria
wema wachache wakijaribu kutuliza.
Bila kuchelewa, paparazi
wetu alianza kuwafotoa picha wanafamilia hao huku Mwanahamisi akijaribu
kuokoa maisha yake kwa kukimbia huku amembeba mwanaye.Mwanahamisi
alisikika akisema hawezi kuhama nyumbani hapo kwa vile nyumba hiyo ni ya
baba yake mzazi hivyo ni bora wamtenge kwenye misosi lakini si
kumfukuza kabisa.
Utetezi wake ulipingwa vikali na wanafamilia hao hasa mama yao mdogo aliyefahamika kwa jina la mama Hashimu.
Baada ya varangati
kuzidi, Mwanahamisi aliona ni heri ambebe mwanaye na kukimbia naye huku
mumewe akimfuata kwa nyuma na kwenda kusikojulikana.
Mke wa baba Juma nae akitimuliwa pamoja na mwanaye.
Katika hali ya
kushangaza, wanafamilia hao walimgeukia paparazi wetu na kutaka
kumfanyia vurugu ikiwemo kujaribu kuvunja kamera yake lakini wakagonga
mwamba.Katika sakata hilo, mwanadada mmoja aliyekuwa amesahau kuchana
nywele, akiwa amejifunga kanga moja kifuani, nyingine kiunoni huku hana
viatu, alimporomoshea matusi paparazi wetu ambayo aliyarekodi.
Kwa vile kisa kilisikika
wakati wa mzozo, gazeti hili lilifanya jitihada za kuzungumza na
wanafamilia hao ili kusikia kutoka kwao lakini ilishindikana baada ya
kukosa ushirikiano kutokana na hasira za kupigwa picha.
Tags:Faraji blog
No comments:
Post a Comment