Mahakama ya juu nchini Marekani
imetoa uamuzi uliompendelea mwanamke mmoja wa kiislamu ambaye alienda
mahakamani baada ya kunyimwa kazi katika kiwanda cha kushona nguo
kutokana na vazi lake la hijab.
Kampuni hiyo ilikataa kumuajiri
Samantha Elauf mwaka 2008 kama msaidizi wa mauzo kwa kuwa vazi lake la
hijab lilikuwa linakiuka sera za kampuni hiyo ambayo ilikuwa inapinga
wafanyikazi kuvaa kitu chochote kichwani.Elauf hakuelezwa kuhusu sera hiyo ya mavazi.
Elauf aliwasilisha malalamishi yake na tume ya kuhakikisha kuwa kuna usawa wa utoaji wa ajira.
Katika ya kura 8-1,majaji hao walitoa ushindi dhidi ya kampuni ya Abercrombie and fitch kwa niaba ya mtafuta ajira samantha Elauf.
Source BBC SWAHILI
Share with your friends
No comments:
Post a Comment