Friday, June 26, 2015

Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi ameuawa katika mapambano na polisi katika kijiji cha Kibande wilayani Buhighwe mkoani Kigoma.


Kamanda Mtui akionesha bunduki iliyokamatwa
Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi ameuawa katika mapambano na askari polisi katika kijiji cha Kibande wilayani Buhighwe mkoani Kigoma baada ya polisi kutaka kuwakamata majambazi watatu waliokuwa wakijiandaa kufanya uhalifu katika tukio hilo ambalo lilipekea bunduki moja ya kivita na risasi 72 kukamatwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma kamishna msaidizi wa polisi Ferdinand Mtui amesema mtu huyo hajatambulika, na kwamba majambazi wengine wawili walifanikiwa kutoroka katika tukio hilo lililotokea katika kijiji hicho cha kibande ambacho kipo mpakani na nchi ya Burundi.
Wakati huohuo risasi 599 za bunduki ya kivita aina ya SMG zimeokotwa katika eneo la Nyawela mjini Kibondo baada ya fundi ujenzi Remijius Robson kuzibaini zikiwa zimefukiwa chini wakati akichimba msingi wa nyumba hali iliyomlazimu kutoa taarifa polisi.

No comments:

BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

 BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm

Logo

Logo Design by FlamingText.com