Kutangaza hapa piga : 0655912580
Kwa upande wa burudani wiki hii ilikuwa ni shoo ya
mchumba wa Nasibu Abdul ‘Diamond’ Zarinah Hassan ‘Zari’ iitwayo Zari All
White Party aliekinukisha usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar na ile ya Instagram Party ambayo ilimhusu mrembo
Wema Sepetu aliyokinukisha jijini Mwanza ambapo mashabiki wa warembo
hao warushiana maneno.Kwa mujibu wa chanzo cha gazeti la Risasi kilidai kuwa Zari amepata sapoti kubwa kutoka kwa mpenzi wake wa sasa Diamond kwani walikuwa wanafanya shoo pamoja hivyo alikuwa na kibarua cha kuwakusanya mashabiki wote wa Diamond waende kwenye shoo yake ili Wema asipate watu.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, kwa upande wa Wema, yeye alikuwa na kibarua kizito cha kuwakusanya marafiki zake hususan mastaa wa Bongo Movies wasiende kwa Zari na badala yake waende Mwanza kwenye Instagram Party.
“Ni mnyukano wa aina yake, Wema alikuwa na kibarua kizito kuwashawishi Bongo Movies waikache shoo ya Zari waende Mwanza kwenye Instagram, bahati nzuri alifanikiwa kwani wasanii wengi walimuunga mkono,” kilisema chanzo hicho
Hadi jana jioni, kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, Timu ya Zari (Team Zari) na ile ya Wema (Team Wema) zilikuwa zikirushiana matusi huku kila mmoja akionesha hisia zake.“Hakuna kwenda kwa Zari, twendeni kwa Wema Mwanza, watakaokwenda kwa Zari ni wapuuzi kabisa,” ilisomeka moja ya komenti ya mdau wa timu Wema huku timu Zari ikijibu:“Wajinga wakubwa watakaokwenda kwa Wema, mpango mzima ni kwa Zari na Diamond pale Mlimani City.”
Ili kuzidi kupata data zaidi, wanahabari wetu walimtafuta mdau mkubwa wa kuwashawishi watu, mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambaye aliweka bayana kuwa wao kama Bongo Movies, wanamuunga mkono Wema.
“Niweke wazi tu kwamba sisi tutakwenda kwa Wema, hii shoo ya Zari na Diamond itatupitia kushoto kwa kweli,” alisema Steve.
Kwa upande wake Kajala Masanja alikuwa tofauti na waigizaji wenzake ambapo alipokea kwa mikono miwili mwaliko wa Zari na kuanza kuihamasisha Team Kajala kwenda kwenye shoo hiyo.
Jitihada za kumpata Zari aweze kufungukia mvutano huo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kuita bila majibu lakini bahati nzuri Wema alipatikana na kufunguka:“Mimi kama mimi nakwenda katika shoo inayonihusu ya Instagram, hiyo ya Zari siijui. Sijashawishi mtu ila watu wameamua kuniunga mkono, siwezi kuwazuia na hao wanaofikia hatua ya kutukana pia siwezi kuwazuia,” alisema Wema.
Source. Bongo Movie Blog
No comments:
Post a Comment