Thursday, May 7, 2015

NINI MASHABIKI WASEMA BAADA YA KAJALA KUHUDHURIA "THE ZARI WHITE PARTY"?


Kajala: Niacheni na Maisha YanguKufuatia baadhi ya mashabiki kumlaumu kwa kitendo chake cha kuhudhuria shoo ya Zari All White Party, staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja amefunguka kwa ukali kuwataka watu kumuacha na maisha yake kwa sababu hayawahusu.
Akiongea na gazeti la Risasi la leo, Kajala  alisema  amekuwa mvumilivu kwa muda mrefu lakini kitendo cha watu kutaka kumpangia nini cha kufanya au wapi pa kwenda, kimevuka mipaka maana hawajui alipotoka wala anakokwenda.
“Watu wanazidi sasa, wanataka kunipangia wapi pa kwenda na wapi siyo pa kwenda, kwani kwenda kwa Zari kuna tatizo gani,  kwa hiyo mtu akiwa na tofauti na Wema, kila mmoja lazima atofautiane na huyo mtu? hayo mambo ya  wapi jamani, watu wasinipangie  maisha ya kuishi,” alisema Kajala.
06.05.2015 -  Tags:  KAJALA 

No comments:

BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

 BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm

Logo

Logo Design by FlamingText.com