Idadi
kubwa ya wanawake wanaofanya biashara ya ngono Mjini Kahama wamedaiwa
kugoma kutumia dawa ya kupunguza makali ya virusi vya ukimwi licha ya
kupima na kubainika wanaishi na maambukizi ya ugonjwa huo badala yake
hutumia kula nyama ya kitimoto kwa madai inapunguza kasi hiyo kuliko
dawa za ARV.
Hali
hiyo imeelezwa jana Mjini Kahama na afisa maendeleo ya jamii Mjini
Kahama Fanuel Ruben ambaye amesema ofisi yake imefanya ukaguzi kwenye
madanguro yanayotumiwa na wanawake hao kwa biashara ya ngono na kubaini
wapo wasichana kati ya miaka 15 hadi 20.
Ruben
amesema baada ya kubaini hiyo wamewachukua wasichana na kuwafanyia
vipimo wengi wao wamebainika kuwa na ujauzito na maambukuzi ya virusi
vya ukimwi hali iliyoonyesha wanafanya ngono bila kutumia kinga ya
maambukizi ya magonjwa ya kuambukiza.
Hata
hivyo amesema wasichana hao baada ya kuwafanyia uchunguzi wamegoma
kutumia dawa za kupunguza makali kwa madai wenzao wanaoishi na virusi
vya ukimwi hutumia nyama ya kitimoto badala ya dawa hiyo.
Kufuatia
hali hiyo Ruben amesema ameandaa mkakati wa kuwachukulia hatua wale
wote wanaofanya biashara ya ngono huku wakijua wao ni waathirika wa
ugonjwa huo kwa kuwa ipo sheria mpya inayokataza mwathirika wa virusi
vya ukimwi kuwaambukiza wenzake kwa makusudi.
SOURCE FARAJA BLOG
No comments:
Post a Comment