Saturday, May 16, 2015

Boko Haram yateka mji wa Marte

Maafisa wa serikali ya Nigeria katika jimbo la Borno Kaskazini mwa Nigeria wanasema kuwa wanamgambo wa kiislamu wa kundi la Boko Haram wameuteka tena mji ulioko mpakani wa Marte.
Gavana na jimbo la Borno anasema kuwa wanamgambo hao wameudhibiti kabisa mji huo na kusema kuwa hilo ni pigo kubwa kwa wanajeshi wa Nigeria.

Naibu gavana huyo aliuambia mkutano wa wanahabari kuwa Boko Haram walikuwa wamefukuzwa kwenda kwa msitu wa Sambisa miezi ya hivi majuzi lakini baadhi yao walikuwa wamejificha miongoni mwa jamii ambapo wamekuwa wakipanga mashambulizi.
''Ni jambo la kutamausha na kuogopesha mno kwa maelfu ya raia wakaazi wa eneo hili kuwa Boo Haram waliokuwa wamejificha miongoni mwetu wamefanya mashambulizi tena na kuuteka mji wa Marte'' alisema Mustapha Zanna
Mji huo wenye umuhimu mkubwa kiuchumi kw eneo zima la kaskazini mwa Nigeria uko katikati ya njia ya kibiashara inayotoka Cameroon na Chad.
Marte umebadilisha utawala kutoka kwa majeshi ya serikali na wapiganaji wa Boko Haram mara kadha kati ya mwaka wa 2013 hadi sasa.

Wapiganaji hao walikuwa wamefifia baada ya muungano wa majeshi ya Nigeria, Niger, Chad na Cameroon kukabiliana nao kuanzia mwezi Februari mwaka huu.
Hata hivyo Boko Haram ambayo sasa imekula kiapo cha kuiunga mkono kundi la wapiganaji wa Islamic state ambao wanashikilia maeneo makubwa ya Iraq na Syria, imeanza kuonesha dalili za kufufuka.
Wapiganaji hao wa Jihad wamewauawa takriban watu 55 karibu na mji wa Maiduguri kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi mitatu.
Harakati za miaka 6 ya kundi hilo la wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram zimepelekea kuuawa kwa watu elfu kumi na tano 15,000 mbali na kusababisha takriban watu miloni moja u nusu kutoroka makwao.

No comments:

BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

 BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm

Logo

Logo Design by FlamingText.com