Rais
wa Burundi Pierre Nkurunziza amewapongeza wanajeshi wazalendo waliozuia
mapinduzi na kurejesha hali ya usalama na utawala huru mjini Bujumbura.
Rais Nkurunziza amewataka waburundi wazalendo kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi utakaofanyika mwezi juni.Rais huyo alikuwa Mjini Dar es Salaam Tanzania siku ya Jumatano kuhudhuria mkutano wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki kundi la wanajeshi waasi walipotangaza ''Mapinduzi'' dhidi ya serikali yake.
Viongozi watatu miongoni mwa makamanda6 wa jeshi waliounga mkono tangazo hilo la ''mapinduzi'' ilikupinga muhula wa tatu wa rais huyo tayari wamekamatwa.
Baada ya kurejea kutoka Tanzania rais Nkurunzinza alielekea Kaskazini mwa Bujumbura eneo alikotokea kabla ya kurejea katika kasri la rais lililoko katika mji mkuu wa Bujumbura.
Katika taarifa iliyochapishwa mtandaoni rais Nkurunzinza alisema kuwa ''
kuna amani na utangamano katika asilimia kubwa ya Burundi na hata katika mji mkuu wa Bujumbura ila tu watu wachache waasi ndio waliokuwa na hamu ya kuvuja damu''
''Jeshi la taifa lilionesha ukomavu wake lilipokabiliana na wasaliti hao''
''Shari msingi wa demokrasia yetu changa ilindwe isiyeyuke''
Nkurunziza aliahidi kulipiza kisasi dhidi ya ''yeyote aliyejaribu kuwasha moto wa uhasama baina ya waburundi''
Wengi wao wafuasi wa chama chake ambao walimshangilia kwa kurejea kwake huko .
Mwandishi wa BBC aliyeko huko Ruth Nesoba anasema japo asilimia kubwa ya mji huo ulikuwa na amani, katika sehemu zingine kulikuwa na waandamanaji walioweka vizuizi barabrani wakipinga kuwania kwake kwa muhula wa tatu.
Polisi wa kupambana na ghasia walikuwa wakikabiliana nao kwa kuwafyatulia mabomu ya kutoa machozi.
Miongoni mwa makamanda waliokamatwa kwa kuchochea uasi ni pamoja na waziri wa zamani wa ulinzi Cyrille Ndayirukiye.
Wawili hao walikamatwa baada ya ufyatulianaji wa risasi nje ya jumba walimokuwa.
Kiongozi wa uasi huo meja jenerali Godefroid Niyombare,aliyetangaza ''mapinduzi'' hayo siku ya jumatano hajakamatwa japo alinukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa atajisalimish.
''Nitajisalimisha kwa utawala, natumai hawataniua'' alisema meja jenerali Niyombare.
SOURCE WWW.BBC.UK.COM
No comments:
Post a Comment