Tuesday, April 21, 2015

Ligi Kuu kuendelea Jumatano Simba VS Mgambo taifa


Tuesday , 21st Apr , 2015
Ligi kuu Soka Tanzania Bara inatarajia kuendelea hapo kesho ambapo Simba watawakaribisha Mgambo Shooting ya jijini Tanga uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam huku Coastal Union wakikaribishwa na Polisi Moro uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.



Akizungumza jijini Dar es salaam, Afisa habari wa Shirikisho la Soka Nchini TFF, Baraka Kizuguto amesema, wameamua kuweka mechi hizo karibu karibu ili kuhakikisha ligi inamalizika Mei tisa mwaka huu ambao ni muda uliopangwa.
Kizuguto amesema, ratiba hiyo itazihusisha timu mbalimbali ambapo Ijumaa Yanga watawakaribisha Ruvu Shooting uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na siku ya Jumatatu Yanga itakutana tena na Polisi Moro Uwanja wa Taifa na baada ya hapo itaelekea Tunisia kucheza na Etoile du Sahel katika mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora.
Kizuguto amesema, mechi ya Jumatatu watakayocheza Yanga na Polisi Moro itakuwa ni mechi ya mzunguko wa 23 ambayo itaanza mwishoni mwa wiki baada ya timu zote kumaliza mzunguko wa 22.
SOURCE EATV

No comments:

BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

 BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm

Logo

Logo Design by FlamingText.com