Thursday, November 13, 2014

Fonolojia,michakato na sheria za kifonolojia



Fonolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na kuchunguza mifumo ya lugha mbalimbali za binadamu. Fonolojia hujihusisha au hujishughulisha na jinsi sauti za lugha zinavyotumika katika kujenga maneno ambayo huwakilisha maana.
Michakato ya kifonolojia ni mabadiliko ya kifonolojia yatokanayo na kubadili maumbo ya kifonolojia na kuwa ya kifonetiki. Mfano katika lugha ya Kingereza /spin/→[spin] “zunguka ukiwa sehemu ileile. Kupitia misingi ya fonolojia kuna michakato na sheria zinazohusu fonolojia; ifuatayo ni michakato ya kifonolojia inayojidhihirisha katika taaluma ya kifonolojia
.
Michakato ya udondoshaji wa vitamkwa, kupitia hatua hii ya udondoshaji wa vitamkwa hutokea pale ambapo maumbo mawili yakiwa yamegotanishwa irabu ya mwisho ya umbo la kwanza inadondoshwa na toni pia hubadilika. Mfano  katika lugha ya Ci-Ruuri kuna
 omwaa’na + omujomu→omwa’a’mujomu
mototo           mzuri            motto mzuri
michakato ya ubadilishaji wa maumbo ya kifonolojia kuwa ya kifonetiki, kupitia mchakato huu wa ubadilishaji wa maumbo hayo tunapata maumbo ya kifonetiki ambayo huwa na kitamkwa ambacho kinaangaliwa kiupekee. Mfano /pin/ huu ni uwakilishi wa kifonolojia na kifonetiki ambapo tunapata umbo la [ph in]          ambapo sauti huwa na mpumuo mkubwa.
Mchakato wa uchopekaji wa vitamkwa, hapa tunapata hili katika lugha ya Kihispania ambayo huchopekwa kitamkwa [∑] kabla ya konsonanti ya mwanzo wa neon katika mfuatano wa #K.
Vilevile zipo sheria mbalimbali zinazotumika katika fonolojia ili kupata maumbo mbalimbali katika fonolojia. Sheria hizo ni kama zifuatazo;
Sheria za kifonolojia zaweza kuwa za lazima au za hiyari, sheria za hiyari ni zile ambazo zinaonyesha kwamba kuna uwezekano wa maumbo yanayohusika kutamka vinginevyo yaani kila mmoja ya maumbo ya nje na  ya umbo la ndani hubadilika. Mfano katika Kiswahili umbo la ndani la neon miaka ni /mi + aka/ lakini umbo la nje la neon hili hutamkwa [mya:ka]
Sheria ya lazima ni sheria ambayo haina budi kutumika iwapo tunataka kupata umbo linalokubalika. Mfano wa umbo la /vi+ungu/ [vyungu].
Sheria za kifonolojia huweza kujenga tabdili, katika sheria hii kwa mfano ukiwa na mwandamo wa X,Y,Z inawezekana baadhi ya lugha kubadili nafasi za sauti kuwa na YXZ au XZY.
Sheria za kifonolojia zinaweza kuunga vitamkwa muungano wa irabu mbili huungana na kuzaa irabu moja lakini irabu inayozaliwa haifanani na irabu yoyote kati ya hizo zilizoungana. Kenstowiics na kisseberth (1979:374) wanaita irabu hiyo irabu fidi.
Kutokana na sheria za kfonolojia ni dhahiri kuwa fonetiki na fonolojia kama matawi ya isimu ya lugha ambayo misingi yake hutegemeana na yanavyohusiana. Vilevile fonetiki na fonolojia huwa na misingi yake, ambapo msingi wa fonolojia ni upambanuzi na uchanganuzi wa kitamkwa kama kipengele knchofanya kazi tofauti na kingine katika mfumo wa lugha mahususi ambapo msingi wa fonetiki ni namna sauti ilivyojengeka katika lugha husika.
Sheria inayohusu utamkaji wa irabu juu inayotamkiwa nyuma hubadilika kuwa kiyeyusho kinachoendandana nayo iwapo mbele yake kutakuwa na irabu ya chini inyotokea mara tu baada ya mpaka wa mofimu.




MAREJEO.
D.P.B Massamba (2012), misingi ya fonolojia, Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili, Chuo Kikuu Dar-es-salaam.



                                                                                                       

No comments:

BREAKING NEWS; MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

 BFYA LINK HAPA CHINI KUYAPATA>>>>> http://41.59.85.98/results/2018/acsee/acseex.htm

Logo

Logo Design by FlamingText.com